Bei ya mafuta imefika 105 USD kwa pipa. Tanzania tutafute mafuta yetu, kuna siku tutalia na kusaga meno

Bei ya mafuta imefika 105 USD kwa pipa Tanzania tutafute mafuta Yetu.

Kufuatia Mzozo unaoendelea kati ya Ukraine na Urusi bei ya mafuta imepanda na kuvuka dola mia moja kwa mara ya kwanza tangu miaka saba iliyopita, ambapo ongezeko hilo limesababishwa na hofu baada ya mzalishaji mkubwa Urusi kufanya mashambulio nchini Ukraine. Urusi ni mzalishaji muhimu wa mafuta baada ya Saudi Arabia.
Bei ya mafuta ghafi barani Ulaya imefikia dola 105 na senti 79 kwa pipa.

View attachment 2130874

The price of oil has reached 105 USD per barrel.

Following the ongoing conflict between Ukraine and Russia oil prices have risen to more than $ 100 for the first time in the last seven years, an increase caused by panic after a major Russian producer carried out an attack in Ukraine.

Russia is the largest oil producer after Saudi Arabia. The price of crude oil in Europe has reached $ 105 and 79 cents per barrel.

View attachment 2130875

Source: ITV and CNBC
Tesla
 
hata ikiwezekana itakuwa gharama mno kuishinda hata gharama ya kuagiza mafuta nje
Sio rahisi, gharama ni mwanzo kwenye kiwanda tu, shida gesi yenyewe aishauziwa mtu hatuimiliki tena sisi, ila ingekuwa inachimbwa na sisi tunaprocess sisi mbona lita la wese lingegonga hata 1500, shida ni hapo mwanzo tu, unaweza ukakuta kiwanda kinahitaji dola bilioni 3-5 hivi.
 
Tutafute mafuta yetu ,wakati hapa tuna gas Bei ya umeme ipo juu Sasa hata tukiyapata mafuta hatutapata unafuu wowote
 
Kama kweli tz tulikuwa na trillions za cubic metres za gas na mara ghafla tunasikia kuwa ilishauzwa yote na inatupasa kuinunua kwa 'wenyewe' ili kuzalisha umeme na kutumia majumbani, unadhani itakuwaje kwa mafuta?

Na najiuliza, inakuwaje Uganda wamevumbua mafuata lakini badala ya kuwekeza kwenye kuyasafisha ili wakamate soko la maziwa makuu badala yake wanawekeza matrillion ili wayalete yakiwa ghafi hadi Tanga ili kuyasafirisha ...wanayapeleka wapi na kesho uanaona trucks zimebeba yaliyosafishwa kuwarudishia.
Tuna tatizo sehemu kwa mtu mweusi
 
Gharama za kujenga kiwanda cha kuchakata mafuta ghafi ni kubwaaaa sanaaaaa
Nigeria wenyewe ndo wanasubiri Dangote amalize kiwanda ndo waanze kuchakata licha ya kuwa wapo hapo kwenye sekta ya mafuta kwa miaka mingi sanaaaa
 
Back
Top Bottom