Bei poa domain registration & internet service provider?

Mambo Jambo

JF-Expert Member
Jul 11, 2008
1,100
81
Wakulu wa jamvi habari za siku.

Nina shida mbili ambazo nitahitaji ushauri wenu, Hapa Tanzania ni kampuni gani inayotoa service ya Domain Registration kwa bei nzuri na ambayo siyo yakubabaisha na vile vile ni ISP gani ambaye anatoa huduma nzuri vilevile kwa matumi ya kawaida connection ya PC moja tu.

Asantenti.

MJ
 
Check WIA, Africa online, Simba net, ila kwa uzoefu wangu mdogo ni kwamba itakuwua expensive
 
Wakulu wa jamvi habari za siku.

Nina shida mbili ambazo nitahitaji ushauri wenu, Hapa Tanzania ni kampuni gani inayotoa service ya Domain Registration kwa bei nzuri na ambayo siyo yakubabaisha na vile vile ni ISP gani ambaye anatoa huduma nzuri vilevile kwa matumi ya kawaida connection ya PC moja tu.

Asantenti.

MJ

Mambo Jambo

Kuhusu domain name, nakushauri usajili ccTLD ya .TZ, ambayo utasajili mara moja tu, na kulipa Administrative Fee (kabla TZ-NIC hawajaanza kazi rasmi) ndogo tu, ya USD 25. Hiyo si Domain Name Registration. Kwa mfano, domain name itakuwa COMPANYNAME.CO.TZ, ambapo utaprovide details za shughuli yako, fomu itajazwa na kutuma kwa registrar wa .CO.TZ domain names, na muda si mrefu, utapata huduma hiyo.

Nikuuliza, hiyo Domain Name, una (1) website ambayo inaambatana nayo, na (2) tayari una mahali ambapo unataka kuhost website yako? Ukijibu maswali hayo mawili, tutasonga mbele.

Kuhusu ISP, siku hizi inategemea na matumizi yako. Kuna wanaotumia CDMA connection za Zantel, 2.5G (wenyewe wanaita 3G) connections za Zain na Vodacom, na kuna ISPs kama vile RAHA.COM, Africa Online, na kadhalika.

Mimi ninatumia huduma ya InfiNet Lite, kutoka kwa Africa Online, ambayo ni unlimited usage, kuanzia saa 1 usiku hadi 1 asubuhi, ninalipa USD 48.00 kwa mwezi. Modem yake, ambayo inatumia teknolojia ya iBurst (hybrid kati ya WiFi na WiMAX), inauzwa kwa bei ya USD 320. Lakini ukishanunua, hiyo ni mali yako, unaweza kumwuzia mtu yeyote ukitaka, na kufunga akaunti yako.

Zantel wanatumia CDMA ambayo itakupa fast data rates, lakini iko based on per megabyte downloads, wakati Africa Online ni unlimited, sidaiwi bandwidth.

Chaguo ni lako.

Kwa mawasiliano zaidi nipigie +255-786-019019 au +255-715-019119.

./MwanaHaki
 
Thanks MwanaHaki

Huduma ya InfiNet Lite, kutoka kwa Africa Online, ambayo ni unlimited usage, kuanzia saa 1 usiku hadi 1 asubuhi, ambayo unalipa USD 48.00 kwa mwezi haitakuwa poa kwangu, kwa kuwa mimi nataka service nitakayotumia mchana kuwasiliana na wauza mkaa wenzangu.

Thanks kaka.
 
Back
Top Bottom