Beef Zilizowahi kutikisa tasnia ya Bongo Fleva

Niki wa pili vs Nikki Mbishi

Weusi coy vs Tamaduni Music

Hii ya Nikki wa pili na Nikki Mbishi Inawezekana ikawa ilisababishwa na jina la Nikki?? maana kuna nyimbo ya Nikki Mbishi anauliza iweje kuna Nikki wa Pili wakati Nikki wa kwanza hajulikani??
 
Inasemekana FID Q alitumia beat ya Langa bila ruhusa yake

Nimekupata mkuu. ila kwenye suala la beat bado sijaelewa vizuri nani ni mmiliki halali wa beat!! kipindi Majani anahojiwa kwenye mkasi alisema kwa kawaida beat huwa ni mali ya Producer
 
Mkuu Hivi Ngwair na Fid Q walishawahi kuwa na beef!!! au ilikuwa ya kimya kimya sana??? hebu dadavua kidogo

Walikuwa na beef nzito ila haikuwahi kwenda media...chanzo ni kudiss-ana fid alimdiss cowboy kuwa halikuwa hajulikani na Mox then wakagombea mikasi..Ila beef ilikuwa kubwa zaidi baada ya Fid kuwa anaongea maneno mabaya kuhusu life binafsi la Ngwea,Ngwea alimaind hadi aliandika ngoma anamtukana sana Fid Q aliirekodi Majani, sema huo wimbo haukufika media..Ila waliwekana sawa maisha yakaendelea.
 
Hii ya Nikki wa pili na Nikki Mbishi Inawezekana ikawa ilisababishwa na jina la Nikki?? maana kuna nyimbo ya Nikki Mbishi anauliza iweje kuna Nikki wa Pili wakati Nikki wa kwanza hajulikani??

Hii mara nyingi huanzishwa na Niki mbishi kwa ubishi wake na kupenda sifa bahati mbaya mwenzie hairespond kihivyo.

Ila ya Tamaduni na Weusi naona Moko wa miujiza bado kaikomalia juzijuzi tu kawapa madongo tena weusi.
 
Kuna Bifu nyingine ilikuwa kati ya P-funk Majani na Chid Benz ingawa haikuvuma sana kwenye media ila ilikuwa kubwa
 
Jay Moe kwenye nyimbo ya Jipange kuna line anasema "amani kaka voda milionea, mwambie mdogo wako aache poda ale mmea" akimchana Langa. Langa nae kwenye nyimbo yake ya Gangster kuna line anasema " amani kwa kaka voda milionea mwambie mo aache ushoga na umbea" kwenye nyimbo ambayo langa alitangaza kuacha poda sina uhakika na jina jina kifo, jela. Langa ananmstari "amani kwa kaka voda milionea, mwambie mo nishaacha poda na pia sili mmea"

Hahahaaahaaa....hiyo michano yao ipo juuu... nimeipenda balaaaaaa
 
Back
Top Bottom