Be aware na tamthiliya ya Be Careful With My Heart

MamaBeata

JF-Expert Member
Apr 15, 2013
325
112
Habari zenu, nadhani kuna baadhi yetu wanafatilia ile tamthiliya ya Be Careful with My Heart inayoonyeshwa katika luninga ya Star TV. Sasa mimi pia ni mdau huwa nakaa naangalia na familia akiwemo msichana anaenisaidia kazi za nyumbani.

Sielewi yeye alikua anaichukuliaje ila nadhani anajifananisha na Maya yule. Nina mtoto mdogo wa kike. Nikawa naona anazidisha mapenzi kwa yule mtoto nikaona sio mbaya.

Pili kuna wakati mume wangu hupendelea chai mida ya jioni sasa pale akiagiza chai inakuwa kama tunagombania kwenda kuandaa na yeye. Mimi huwa nanyanyuka nikijua ni wajibu nakuta mwenzangu yuko jikoni tayari.

Mwanzoni hakua kiherehere hivi nikakumbuka mambo ya chief kuipenda kahawa ya Maya nikajipa moyo niache mawazo machafu. Sasa leo ndio nikaona too much yani alipotoka kuoga kajipulizia perfume nyumba nzima inanukia.

Nikakumbuka jinsi Maya alivyojipulizia perfume nyingi ile episode ya jana. Nikamfata chumbani nikamwambia kulikoni mperfume wote huo? Akasema hamna kitu.

Nikamwambia unajipulizia umvutie nani? Akasema sina hayo mawazo. Nikamwambia hayo unayoyaona kwenye tamthiliya ni maigizo. Na hata yangekua kweli yule Sir chief mkewe amekufa.

Sasa usikae busy kutaka kumfurahisha mume wangu mi bado niko hai. Hakujibu kitu nikawaza tu huyu sir chief kazua jambo. Haa!
 
Mhh!!!!!sema tu kwa sababu mke wa sir chief amekufa,ila kama angekuwa hai,na ww ungeplay part yako.au vp
 
Tofauti ni kubwa sana,

Kwenye tamthilia hiyo, Mama Mwenye Nyumba alishakufa kitambo tu wakati kwenye familia yako Mama Mwenye Nyumba ni wewe na uko hai.

Pili usimuendekeze beki tatu wako kuangalia angalia video na wewe pamoja

Tatu kama beki 3 ni mzuri basi Fanya substitute haraka!!
 
Hu ile tamthilia si mchezo mambo ya sir chief na mdada wako.ana copy na ku apply kwa husband kweli.be.carefuly with ua dada
 
Back
Top Bottom