Jamiitrailer
Member
- Oct 20, 2019
- 25
- 80
Kilichoelezwa na BBC kuhusu tuhuma dhidi ya TB Joshua zinaweza kuwa zina ukweli kwa vile wapo binadamu waliowahi kufanya mambo kama hayo na wengine watafanya.
Lakini tuhuma hizo pia zinaweza kuwa ni za uzushi kwa vile watu wanajua kuzua mambo kwa faida zao....lakini wanaotoa tuhuma wana haki ya kusikilizwa.
Lakini tuhuma zao pia zinatakiwa kuingizwa katika mizani ya kupima dalili za ukweli na uwongo.
Mathalan,BBC wamemuelezea huyo binti wa TB Joshua,anayetoa tuhuma kuhusu baba yake kwamba anasifiwa na waliokuwa wanga wenzie kwamba ni yeye pekee huyo binti ndiye aliyekuwa na ujasiri wa kumkabili baba yake na kumuuliza kwa nini anawanyanyasa. Lakini ni BBC hao hao wanaosema imebidi wafiche utambulisho wa jina halisi la huyo binti na makazi yake kwa vile ana hofia maisha yake.
Hapo ndipo pana walakini,...ina maana BBC hawajiulizi imekuwaje huyo binti aliyekuwa jasiri wa kuweza kumkabili baba yake wakati huo akiwa hai..na asihofie chochote wakati akiendesha maisha yake katika jiji la Lagos kama walivyodai,....eti aje kuwa no hofu leo wakati baba yake keshafariki?
Huo ujasiri wake umetoweka mara baada ya baba yake kufa? Tulitarajia angekuwa na uhuru na kutohofia chochote wakati huu.
Na jambo jingine,kwa nini BBC iwachukue muda mrefu kiasi hicho kama huyo wanayedai ni binti yake alitoa tuhuma hizo mwaka 2019?
BBC wanasema walisubiri watu wengine wajitokeze ili waweke bayana habari kamili.
Hiyo hoja haina mashiko...,kwa vile inakufanya mtu kutamani kujiuliza kwa nini BBC wasimkabili TB Joshua na tuhuma wanazosema ni za binti yake kwanza,..?
Ina maana kama huyo binti angekuwa ni mhanga pekee,BBC wasingejihangaisha kuelezea kadhia yake....yaani kama akinyanyaswa mtu mmoja hakuhesabiwi kuwa kosa hadi wanyanyaswe watu wengi ndipo liwe kosa?
Ina maana kwa mujibu wa BBC..mtu mmoja mwenye ushahidi wa kubakwa au kutotendewa haki na mtu mwenye nguvu au uashawishi hasaidiwi kusikika au kutafutiwa haki hadi wabakwe wengine wawili au zaidi?
Binti mmoja wa TB Joshua anayeitwa Serah Joshua ameolewa na kijana wa Kitanzania . Waandishi wa habari wa kibongo wammuhoji huyu binti awape picha ya upande wa pili wa maisha yalivyokuwa nyumbani kwao.