BAVICHA waishughulikia CCM; Katiba, kutukana waasisi, Interahamwe, wamkamata Makonda

Chief Isike

JF-Expert Member
Jan 17, 2010
445
462
TAARIFA KWA UMMA
Kama ambavyo tulitoa taarifa yetu kwa umma wa Watanzania Aprili 20 mwaka huu, kuunga mkono hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) katika kupigania maoni yanayowakilisha matakwa na maslahi ya Watanzania kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya, ambapo tuliwataka wananchi;

1. Kuungana na makundi mbalimbali katika jamii, taasisi, asasi za kiraia na watu wengine mashuhuri ambao wameamua kujitoa hadharani kusimamia maoni ya wananchi kama yalivyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya kwenye Rasimu ya Pili, kama inavyoelezwa katika katiba ya sasa, ibara ya 8 inayosema mamlaka ya kuongoza nchi yote yatatoka kwa umma/wananchi.

2. Kutumia nguvu zote zilizojaa ushawishi wa hoja na mbinu halali dhidi ya njama za aina yoyote zinazofanywa kupindua na kuchakachua maoni.

Leo pia tunaendelea kusisitiza kuwa;

1. Hakuna kikundi chochote kinaweza kujitwalia mamlaka ya kwenda kinyume au kupindua maoni ya wananchi kwenye Rasimu ya Katiba Mpya, ambao ndiyo wenye hati miliki na nchi yao.

2. Wananchi wa Tanzania ambao waliona mchakato wa kuandika Katiba Mpya ni fursa ya kipekee ‘kujizaa’ upya kama taifa, kwa kurekebisha na kuboresha utaifa wao kupitia mkataba halali wa ‘katiba’, wanafuatilia kwa makini mno namna ambavyo watawala wanataka kupoka na kubaka demokrasia kwenye jambo nyeti kama hili kwa manufaa ya CCM.

3. BAVICHA kwa kushirikiana na vijana wengine wenye machungu na TANZANIA, tutashawishi, kuratibu na kusimamia hoja za msingi katika kuhakikisha kizazi cha sasa na vingine vijavyo, vinanufaika na matunda yatakayo andaliwa leo.

4. Hatutakubali kuona Katiba Mpya inapatikana kwa ghiliba, hila na vitisho vya watawala badala ya makubaliano na maridhiano yenye nia na dhamira safi, yakiweka mbele maslahi na matakwa ya Watanzania bila kujali tofauti yoyote ile kama dini, kabila wala rangi.

Tunapenda kusema hivyo kwa sababu zimeanza kuonekana dalili za njama za wazi kabisa zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia njia mbalimbali kutaka kutengeneza hali ya taharuki na kuwatisha wananchi wasijenge hoja za kudai maoni yao yaheshimiwe kwenye kuandika Katiba Mpya ya Tanzania.

Njama hizo za kujenga hali ya hofu na kuibua sintofahamu ambazo zimekuwa zikizungumzwa na viongozi waandamizi wa chama hicho, zimeendelea kudhihirika tena baada ya chama hicho, kupitia kwa kada wake. Paul Makonda, kutoa tamko la kuhamasisha vurugu na ‘kuanzisha’ vita, kwa nia ya kuwatisha wananchi washindwe kudai katiba yao inayotaka kupokwa na CCM.

Kada huyo ambaye anajulikana ndani na nje ya chama chake kwa namna alivyo mahiri wa kutumika kwa ajili ya maslahi binafsi ya watu au wakati mwingine hata dhidi ya chama chake, kwa ajili tu ya kutetea tumbo lake, amenukuliwa leo kwenye vyombo mbalimbali vya habari, akitoa maneno ambayo kwa hakika yamezidi kuwachochea wananchi kujua kuwa CCM si chama cha siasa tena, bali genge la wabaka demokrasia.

Kupitia vyombo mbalimbali vya habari, Makonda amenukuliwa akitoa maagizo kwa vyombo vya dola na vijana wanaounda jeshi haramu la CCM (Intarahamwe), linalojulikana kwa jina la Green Guard kuanza kufanya mashambulizi dhidi ya viongozi wa UKAWA kwa sababu tu wameipiku CCM na mawakala wake, katika kujenga ushawishi kwa wananchi unaotokana na hoja zenye ushahidi wa takwimu za kitafiti na mtiririko wa mantiki katika kutetea maoni ya wananchi kwenye rasimu ya katiba.

Kauli hiyo ya Makonda ya kuwaagiza vijana wa Green Guard wajipange kufanya mashambulizi bila shaka kwa nia ya kuteka, kujeruhi, kutesa na hata kuua, ambayo imepata baraka za viongozi wakuu wa chama chake (ref. Gazeti la Mwananchi, Jumanne, Aprili 22, 2016, Toleo Na. 5022, uk. 3, aya ya 9), imedhihirisha mambo mengi ambayo BAVICHA tumekuwa tukisema kuwa CCM kinahusika;

Uhalali wa kuwasemea waasisi

CCM ilishapoteza uhalali wa kuwatetea au kuwasemea waasisi wa taifa hili na hata waasisi wa chama hicho. Hakina ushawishi wa kisiasa tena wa kuweza kutetea uadilifu na uaminifu wa viongozi wetu walioweka misingi ya taifa hili.

Makonda kama anataka kujipambanua na walafi wenzake wa CCM, alipaswa kuliona suala hilo mapema. Alipaswa kuwa mtu wa kwanza kujiondoa kwenye chama chake mara tu kilipoanza kukodi na kutumia vijana vibaya kuwasema vibaya viongozi wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, wakiongozwa na Jaji Joseph Sinde Warioba.

Lakini kwa sababu anazo sifa zote za unafiki kama zinazoelezewa kwenye vitabu vya dini, Makonda akishirikiana na wana CCM wenzake wanaomtumia, walinyamazia vitendo vya kihuni vilivyofanywa na chama hicho kukodi vijana kwenye makongamano na vipindi vya tv na redio kumtukana matusi na kumtakia kifo Jaji Warioba na wenzake.

Itakumbukwa kuwa kitendo cha kulaani na kuwatakia kifo viongozi waandamizi wa nchi hii ‘mwasisi’ wake ni Nape Nnauye ambaye aliwahi kunukuliwa akiwatakia kifo cha haraka wajumbe wa Tume ya Warioba, akisema kuwa watakufa haraka, kwa sababu tu wamesimamia maoni ya Watanzania kuhusu muundo wa Shirikisho la Serikali Tatu.

Upo msemo wa kiingereza usemao ‘You cannot eat your cake and still have it’, ukiwa na maana kwamba huwezi kutumia ulichonacho kisha ukaendelea kuwa nacho kama kilivyokuwa, haiwezekani. Ndicho wanachofanya CCM kwa sasa, hasa linapokuja suala la kulazimisha kuwa wasemaji na watetezi wa waasisi wa taifa hili. Ni unafiki na kutaka kuendelea kuwa na keki ambayo wameshaila.

CCM walipoteza uhalali wa kuwasemea waasisi mara tu walipoanza kuacha misingi ya chama chao na kukumbatia uchumi wa soko ‘holela’ badala ya huria, wakaanza kuwauzia rasilimali za nchi hii wageni kwa bei za kutupwa. Wakauziana hadi nyumba za umma, zingine zikiwa kwenye maeneo nyeti kwa bei za kutupa.

Kama Makonda anahamasisha vijana wa CCM kufanya vurugu kwa sababu waasisi wamesahihishwa au kukosolewa (kama ambavyo waliwahi kukiri wenyewe kuwa kuna mahali walifanya makosa), tunaomba kuwauliza CCM, je wanataka vijana wengine ambao ni wengi zaidi kuliko Green Guard, wenye uchungu na taifa hili, waanze kuwasemea na kuwapigania waasisi kwa nguvu kama wanavyotaka kufanya wao CCM?

Maana vijana wenye uchungu na Tanzania, ambao ni wengi kuliko CCM wanayo machungu makubwa baada ya waasisi wa taifa hili kutukanwa hadharani na viongozi waandamizi wa CCM na serikali ya chama hicho.

Tena vijana wenye uchungu wa kutukanwa kwa waasisi, hadi leo hawajakaukwa na machozi baada ya viongozi wakuu wa CCM kumtukana na kumtusi Mwalimu Nyerere hadharani kwa kuuza kwa bei ya sawa na kutupa iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara. Je wanataka vijana waanze kumdai hiyo benki Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa?

Vijana wenye uchungu na nchi hii hawajasahau namna ambavyo CCM walimtusi na kumtukana kwa vitendo na maneno Mwalimu Nyerere kwa kukumbatia soko holela na uuzaji wa nchi kwa jina la ubinafsishaji hadi Baba wa Taifa akasema watauza hadi Magereza!

Hawajasahau pia jinsi ambavyo CCM walimtusi na kumtukana Mwalimu Nyerere kwa kuufanya ufisadi kuwa mojawapo ya sera za siri zinazosimamia utendaji wa chama hicho na serikali yake, kiasi kwamba walifikia mahali wakaiba hadi Benkii Kuu ya Tanzania.

Je CCM wanataka vijana wenye uchungu na kuharibiwa kwa taifa lao, walioeneea nchi nzima, wasimame pale walipo tayari kwa kuhesabiwa, kuwapigania na kuwasemea waasisi wa Tanzania dhidi ya rushwa inayofanywa na kuatamiwa na CCM kwenye siasa za nchi hii, jambo ambalo lilipingwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa nguvu zote?

Akina Makonda na wenzake wanaomtumia ndani ya CCM, kama wanataka walau kurudisha uhalali walioupoteza siku nyingi, walipaswa kuagiza vijana wao wa Green Guard kuanza kushambulia viongozi wa CCM ambao wamegeuza ikulu kuwa pango la walanguzi badala ya kuwa mahali patakatifu kwa ajili ya kuwapatia Watanzania haki na matumaini, kama alivyosema Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.

Kama CCM wanafikiri wanayo mamlaka ya kushambulia mtu kwa sababu eti ya kuwalinda waasisi wa taifa hili, walipaswa kuwa wameshawashambulia na kuwafutilia mbali viongozi wa CCM ambao leo wamesababisha TEMBO kuwa kwenye hatari ya kufutika kutokana na ujangiri wanaoufanya.

Kama akina Makonda na hiyo CCM wanafikiri wanaweza kushambulia watu na kuua kama ambavyo wamekuwa wakifanya na wanavyopanga kufanya kwenye huu mchakato wa Katiba Mpya na kuelekea uchaguzi mkuu ujao, basi wangeanza kwa viongozi wa CCM na serikali yake ambao wameamua kuitangaza Tanzania duniani kwa ubingwa wa kuuza na kununua dawa za kulevya.

Kama kuna tusi, kashfa, kejeli, tukano na bezo ambalo CCM wamewafanyia waasisi wa Tanzania basi ni UFISADI, UBADHIRIFU, UJANGIRI na DAWA ZA KULEVYA.

Aibu hii ya dawa za kulevya ambayo viongozi wa CCM na serikali yake wameamua kulibebesha taifa hili ili wao wapate fedha huku wakiwageuza vijana wenzetu kuwa punda wao wa kubebea bidhaa hizo haramu, ni moja ya tusi kubwa mno ambalo waasisi wetu wametukanwa, wanatukanwa na bila shaka wataendelea kutukanwa na CCM.

Iko siku vijana wenye uchungu na nchi hii watasimama na wote watakuwa tayari kuhesabiwa, kuwapigania waasisi wa Tanzania dhidi ya ujangiri unaendelea kukubuhu huku ukiachiwa kutamalaki kufutilia mbali utalii wetu, kwa sababu tu unafanywa na viongozi wa CCM.

Watasimama pia kupinga vijana wenzao kuendelea kufanywa mazezeta kutokana na kuuziwa dawa za kulevya, biashara ambayo CCM na walishasema wanaoifanya wanawajua, lakini hawawezi kuwakamata kwa sababu ‘ni wao hao hao’…ni wao wenyewe’.

Vijana hao wenye uchungu na nchi yao ambao sisi tuna uhalali wa kuwa sauti yao, iko siku watasimama na watakuwa tayari kuhesabiwa, na hizo siku zinakuja, pale watakapoamua kuwasemea na kuwatetea waasisi wa Tanzania kwa kupinga vitendo vinavyofanywa na CCM vya kuwatoa uhai vijana wenzao, wazee wao, baba zao,mama zao, kaka zao, dada zao, wadogo zao, kwenye mauaji yanayofanywa kwenye shughuli za kisiasa.

Kumwaga damu isiyokuwa na hatia kwa sababu tu za kisiasa, ni moja ya matusi makubwa ambayo waasisi wetu wanatukanwa kila siku na viongozi wa CCM na serikali yake, hususan kwenye mikutano na operesheni za CHADEMA na chaguzi ndogo.

Siku zinakuja pia, ambapo vijana wenye machungu na nchi yao, watasimama na kuwa tayari kuhesabiwa, wakipigania hadhi ya waasisi wa Tanzania kwa namna walivyotukanwa na viongozi wa CCM na serikali yake, walipowasamehe na kuwapigia magoti mafisadi na wala rushwa wakubwa ndani ya nchi hii, walioliibia taifa hili mabilioni, huku wakiwapeleka jela na kuwafunga vijana wanaoiba bata au kuku.

Vijana hao wenye uchungu na nchi yao, watapambana kupigania hadhi ya waasisi wao kwa kuwatetea vijana wanaobambikiwa kesi na kuozea gerezani huku mafisadi wanaosababisha ukosefu wa elimu bora shuleni na afya bora hospitalini, wakitembea vifua mbele wakiwa kwenye magari yenye viyoyozi yanayopatikana kwa kodi ya mnyonge wa Tanzania.

Uchungu huo wa vijana ukifikia kilele cha juu, wataamua kwenda kubisha hodi kwenye magereza ambayo yametumika kuwaumiza vijana wasiokuwa na hatia kwa sababu tu wamezaliwa familia maskini, huku vijana wanaotumika na watawala kama akina Makonda wakiachwa kutembea barabarani pamoja na kutoa kauli zinazoweza kusababisha mauaji kama alivyofanya juzi.

Wamedhihirisha tuliyoyasema- Interahamwe;

Interahamwe ni kikundi cha kijeshi kilichokuwa kinatumiwa na watawala kupambana kwa nguvu na kukandamiza demokrasia na wapinzani wa kisiasa wa serikali nchini Rwanda hadi kusababisha mauaji ya kimbari nchini humo. CCM nao wanapitia katika hali hiyo hiyo ya kulazimika kutumia vikundi haramu vya kijeshi ambavyo vinalindwa na dola, kushambulia watu wanaosimamia maslahi na matakwa ya wananchi.

Kauli ya Makonda ambayo Jeshi la Polisi nchini kupitia kwa msemaji wake, Advera Senzo limesema eti halina taarifa nayo, imedhihirisha kwa ushahidi kuwa kikundi cha ulinzi cha Green Guard huwa kinatumika kushambulia, kupiga watu, kuteka, kutesa na hata kuua kama ambavyo kimefanya mara kadhaa hususan wakati wa chaguzi ndogo.

Pia kauli hiyo imedhihirisha kile ambacho wananchi wamekuwa wakihoji kulikoni ukimya wa serikali na vyombo vyake katika matukio mbalimbali ya utesaji, utekaji nyara kwa nia ya kuua, ambavyo watu mbalimbali ndani ya jamii wamekuwa wakifanyiwa hususan wanapokuwa na mtizamo au maoni tofauti na watawala.

Upo ushahidi wa wazi, ukiwemo wa viapo, kuwa Green Guard ambao CCM wamewaagiza kushambulia viongozi wa UKAWA wamekuwa wakihusika katika matukio ya njama za kutesa, kuteka na kuua watu, kwa kutumia njia mbalimbali, ikiwemo silaha na sumu, suala ambalo mara kadhaa chama hicho kimekuwa kikikanusha, lakini hatimaye kimedhihirisha.

Na kauli hiyo ya CCM ya kuagiza Green Guard kushambulia watu, ikithibitishwa zaidi na matendo ya kikundi hicho, imesaidia kufafanua kauli iliyotolewa bungeni na mjumbe wa UKAWA, Prof. Ibrahim Lipumba, kuwa chama hicho kimegeuka kuwa Intarahamwe.

Kauli yake ya jana bungeni ya kutukana viongozi wenye heshima kubwa ndani ya jamii ya Watanzania, akiwa ametumwa na watu wanaomtumia kusema maneno ya hovyo kila siku, imedhihirisha namna ambavyo CCM wamepigwa ‘upofu’ wa hekima na busara.

Kauli hiyo ya jana bungeni imedhihirisha pia kuwa CCM wamefilisika kabisa katika ujenzi wa hoja zinazoweza kushawishi wananchi wakubaliane nao, kwa upuuzi wanaouonesha ndani ya bungeni, ambapo wamekuwa wakitukana na kubeza maoni ya wananchi yaliyomo ndani ya Rasimu ya Katiba Mpya.

Makonda ni mtu wa aina gani

Kama kauli ya Makonda isingekuwa na baraka za CCM na watawala walioshindwa kusimama kwa hoja na uhalali wa kisiasa, tungewaomba Watanzania wampuuze kwa upuuzi wake ambao amekuwa akiuufanya na kuusema unaomthibitisha kuwa yeye ni mpuuzi.

Anajulikana kwa umahiri wake wa kutanguliza tumbo lake na kulinda maslahi ya wakubwa wanaomtumia kwenye makundi ya ndani ya CCM.

Akiwa Moshi alikokuwa akiwalaghai (na kuwatapeli fedha akisingizia analipa ada) baadhi ya watu ambao huwa wanamtumia kuwa yuko chuoni anasoma, wakati hasomi, alikuwa akijulikana mji mzima kwa jinsi ambavyo mtu yeyote mwenye fedha angeweza kumtumia kwa namna mbalimbali ikiwemo kutoa matamko. Mara kadhaa ametumika na watu wa nje na ndani ya CCM kukihujumu chama hicho anachosema yeye ni mwanachama.

Itakumbukwa pia kwamba wakati wa uchaguzi mkuu wa chama hicho mwaka jana, baada ya kushindwa nafasi aliyokuwa akigombea, ni Makonda huyu huyu ambaye aliandika mambo mengi akionesha namna ambavyo CCM kinanuka rushwa na kimekubuhu kwa ubakaji wa demokrasia.

Lakini kwa sababu siku zote amekuwa akifikiria kwa kutumia tumbo huku akilitanguliza mbele kabla ya kitu kingine na wenzake wanamjua, hao hao aliowaita wala rushwa na wabaka demokrasia, wakampachika cheo hicho alichonacho sasa ndani ya UVCCM ambacho kimemfanya ale matapishi yake, sasa eti anawaita ni wazalendo, badala ya genge la wahuni kama alivyowasema yeye mwenyewe.

Pamoja na makelele yake, basi walau angelikuwa mwadilifu, hana hata chembe ya sifa hiyo. Badala yake kama ilivyo kwa mwanaCCM, Makonda anatembea na lundo la tuhuma za ufisadi na ubadhirifu, huku mfano mzuri wa hivi karibuni, ni kitendo chake cha kula fedha na kukwamisha uchaguzi wa Vijana wa Chipukizi wa CCM uliokuwa ufanyike mjini Morogoro.

CCM wanajua kwamba uchaguzi huo umeshindwa kufanyika kwa sababu Makonda ambaye ni anahusika na kitengo hicho alikula fedha zote, kiasi kwamba watoto wale walikosa hata mahali pa kulala. Kwa sababu ndani ya chama hicho wanazidiana kiwango cha ulafi, hadi sasa hajachukuliwa hatua yoyote.

Itakumbukwa pia, kwamba ni kijana huyu huyu akiwa pamoja na viongozi wengine waandamizi wa CCM, akiwemo Samuel Sitta, Harrison Mwakyembe, Nape Nnauye na wengine, waliwahi kuunda chama cha CCJ, wakisema CCM ni chama kinachokufa na hawawezi tena kuwa wanachama wa chama kisichosimamia misingi yake.

Tunaweza kusema mambo mengi kwa namna tunavyomjua kijana huyu. Yeye anajua kuwa hata jina analotumia SI JINA LAKE HALISI, lakini itoshe kusema kuwa tangu tulipomtangaza Nape Nnauye kuwa ni Vuvuzela namba moja ndani ya CCM na hadi leo anajulikana hivyo, hatukuwahi kujua kuwa mwingine anayemfuatia kwa ukaribu kwa uvuvuzela ni Paul Makonda. Ndiyo maana haishangazi kuwa katika makundi ya CCM, watu hawa wako kundi moja. Ama kweli ndege wenye manyoya yanayofanana, huruka pamoja.

Hitimisho

Tunahitimisha kwa kutoa angalizo na onyo kwa vijana wa CCM ambao tunajua wako kwenye maandalizi ya kuanza kufanya fujo zinazoratibiwa kimkakati kuharibu mchakato wa Katiba Mpya, ili kuwapatia ‘fursa’ watawala kuweka visingizio vya kuzuia harakati za UKAWA kuuelimisha umma.

Wasijaribu wala kudiriki kutekeleza hayo maagizo ya kuwashambulia wananchi kwenye shughuli zao mbalimbali na viongozi wa UKAWA. Katika hili tunaomba kuwa wazi, tuko tayari kusimama na kuwalinda viongozi wetu.

Imetolewa leo Aprili 22, 2014, Dar es salaam na

Daniel Naftal
Afisa Utawala na Fedha
Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA)
 
Attachments

  • TAMKO LA BAVICHA.docx
    22.9 KB · Views: 124
Bavicha!!!!!!!!!!!!
We will miss JOHN MNYIKA. naona mlolongo wa malalamishi na kutojiamini.
Lingine ni kwamba, bado mnaendesha siasa za kitoto. Na safari hii hatutawachukulia kama WATOTO. Tutawachukulia kama WAASI na tutawasambaratisha vibaya.
The stage is set ....we are waiting for the actors to show up on the stage.
KAMA HUTAKI SERIKALI MBILI..... START PARKING YOUR BAGS
 
Tamko limejaa hekima na uzalendo zaidi! Watanzania wasipokuwa makini maoni yao yatachakachuliwa zaidi! Mainterahamwe wako bungeni ili kuhujumu mchakato wa katiba mpya!
 
Hahaaa UKAWA wazee wa michepuko, njia kuu imewashinda mnatafuta michepuko.
 
Huyu Makonda ameshindikana anatukana wakubwa, aliwahi kumtukana Mzee Lowassa kwa kujiamini kabisa kama inchi hii ni ya mamake. alimtukana Lowassa eti
1. Fisadi
2.Mla rushwa
3.Mtoa hongo mubwa
4. Hawezi kuwa amiri jeshi mkuu
Je kwani yeye Makonda ni nani?
 
Wadau.
Hili tamko limejaa ukweli, mantiki, falsafa na linatoboa Yale yote muhimu ambayo kila kijana mwenye fikra, uchungu na uthabiti kwa Tanganyika na zbar atakubali kuusimamia ukweli huo.

Tamko hili lilivyotulia yafaa kabisa uongozi wa CDM wafanye jambo Moja rahisi lakini litakalotikisa na kuimarisha ukweli huu na kuanika zaidi uozo wa ccm ili vijana wote na umma wapate kusimama kwa uthabiti dhidi ya ufidhuli wa ccm uliotawala zaidi ya nusu karne sasa! Haifai hata kidogo kwa uongozi wa CDM na wapenda nchi wote kukaa kimya! Yafaa kufanya jambo moja rahisi lakini litakalojenga uthabiti kwa taifa na kudumisha ari ya kulikomboa taifa. CDM taifa waunge mkono BAVICHA kwa kulifanyia Editting, kulingariaha zaidi na kuichapisha hii kama kitabu mapema. Tunakihitaji sana tuwaelimishe wengi mitaani, vyuoni, na kila kona ya taifa ili waepukane na hii kansa inayofanana kabisa na ya interahamwe. CDM Wafanye kuongezea nyama za nguvu, hoja na list ya ufisadi toka enzi za uuzaji Mali za umma au ubinafsishaji hadi EPA na karibuni kabisa ufidhuli ktk BOT na IPTL, KADHALIKA ccm imeoza kwa mambo mengi, ujangili, uuzaji sembe, sera mbovu za elimu, afya na umaskini na uharamia ambao umefanyika chini ya au kupitia kwa wakala wa watawala wa ccm na jinsi wanavyohaha kuvuriga rasimu ya pili ya katiba il I kujilinda.

Hiki kitabu kama kitachapishwa kitakuwa 'asali' kwa taifa na vijana kwa wakubwa watakinunua kuliko kitabu chochote...tunakihitaji tukisambaze...hiki kitaweka msingi usiofutika kuhusu ukweli na udhalimu wa ccm. Hili tamko thabiti halifai kupotelea mbali...ni hazina kwa vijana wote wanasimamia Tanganyika na bar huru.

Naomba kuungwa mkono.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom