BAVICHA, Kamanda Mbowe kuitikisa mikoa sita kwa Chopa!

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,862
Wakati vijana wa chama cha zamani wakiwakosea adabu na kuwapiga waasisi wa taifa hili, vijana wenzao wa Bavicha walioandliwa barabara kuichukua nchi hii na kurudisha heshima ya kijana mtanzania wanaanza ziara ya mikoa sita ya Morogoro, Dodoma, Singida, Kigoma,Tabora na Katavi.

Katika ziara hiyo timu itakayoenda kanda ya magharibi itaongezewa nguvu na Kamanda wa anga mwenyekiti Mbowe. Kamanda alitoa ahadi ya kuishambulia mikoa hiyo ktk kikao cha balaza kuu la chama lakini pia wanapeleka elimu ya katiba inayopendekezwa na kuhimiza watu kuchagua wagombea wetu uchaguzi wa SM.

Timu hiyo yenye makanda 30 inatarajiwa kuondoka makao makuu muda wowote kuanzia leo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la mwenyekiti alilotoa viwanja vya jangwani wakati wa mkutano wa Ukawa.

BARAZA la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), kesho linatarajiwa kuanza operesheni ya kurejesha haki na usawa kwa Watanzania ambao wamenyonywa na kukandamizwa muda mrefu na utawala wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Ziara hiyo ni utekelezaji wa agizo la Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, alilolitoa hivi karibuni wakati wa mkutano wa vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), vilipotiliana saini ya makubaliano mbalimbali ya kisiasa jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa BAVICHA, Paschal Katambi, alisema ziara hiyo itafanyika katika mikoa sita angani na ardhini, na kwamba operesheni hiyo itaitwa ‘M4C BAVICHA Commando', ikiwa imegawanywa katika kanda mbili, Kati na Magharibi.

"Katika kanda ya kati tutapita mikoa ya Morogoro, Singida na Dodoma na ile ya Magharibi itahusisha mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi, ambapo kila timu itakuwa na makamanda 30," alisema Katambi.

Alisema katika operesheni ya angani katika kanda hizo, itamhusisha pia Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, ambako watapita kila mahali kuanzia kitongoji, kijiji, kata, wilaya hadi mkoa na hakuna sehemu itakayoachwa.

Katambi, alisema kikubwa watakachokifanya ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa.

"Pia operesheni hii itawahamasisha wananchi kuhusu uchaguzi huo, ili kila mmoja aweze kutambua umuhimu wa kupiga kura kwa ajili ya kupata viongozi waadilifu watakaolikomboa taifa kutoka katika lindi la umasikini uliosababishwa na CCM," alisema.

Kwa upande wake, Katibu wa BAVICHA, Julius Mwita, alifafanua kuwa kundi hilo la viongozi litagawanywa timu mbili, ya kwanza itahusika na mikutano ya hadhara na ya pili uendeshaji wa semina na mafunzo kwa viongozi wa chini wa chama hicho kuhusu Katiba Pendekezwa.

"Operesheni hii pia inakusudia kutengeneza mazingira ya kukijenga chama kuanzia ngazi ya chini hadi taifa, ili kiwe na mfumo bora wa utendaji," alisema Mwita.
 
Bajeti ya ziara yake ni kiasi gani? Nasikia wafadhili wamempa shilingi bilioni mbili kwa ajili ya ziara hiyo
 
image.jpg
 
Bajeti ya ziara yake ni kiasi gani? Nasikia wafadhili wamempa shilingi bilioni mbili kwa ajili ya ziara hiyo

Vijana watanzania tuache siasa za propaganda zimepitwa na wakati - Salmu Mwalimu.
 
Wakati vijana wa chama ch7a zamani wakiwakosea adabu na kuwapiga waasisi wa taifa hili, vijana wenzao wa Bavicha walioandliwa barabara kuichukua nchi hii na kurudisha heshima ya kijana mtanzania wanaanza ziara ya mikoa sita ya Morogoro, Dodoma, Singida, Kigoma,Tabora na Katavi.

Katika ziara hiyo timu itakayoenda kanda ya magharibi itaongezewa nguvu na Kamanda wa anga mwenyekiti Mbowe. Kamanda alitoa ahadi ya kuishambulia mikoa hiyo ktk kikao cha balaza kuu la chama lakini pia wanapeleka elimu ya katiba inayopendekezwa na kuhimiza watu kuchagua wagombea wetu uchaguzi wa SM.

Timu hiyo yenye makanda 30 inatarajiwa kuondoka makao makuu muda wowote kuanzia leo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la mwenyekiti alilotoa viwanja vya jangwani wakati wa mkutano wa Ukawa.
Kila la kheri kamanda na timu cdm ktk kutafuta ukombozi wa taifa letu kwa kumg'oa mkoloni mweusi ccm...peoplesssssssss!!!
 

Attachments

  • 10669105_658862190879090_1474681969313438198_o.jpg
    10669105_658862190879090_1474681969313438198_o.jpg
    129.5 KB · Views: 272
Unaposema amepewa billion mbili, unadhani hiyo hela itakuwa na thamani kubwa kuliko uelewa atakaowapa wananchi?, mijitu inayohongwa nguo na kuchagua viongozi wa ovyo anayeleta mateso kwa muda wa miaka 5 ndiyo inakuwa na mawazo haya haya. Wawezeshe watu kujitambua na kutambua haki na wajibu wao, utakuwa umewasaidia sana,
 
Kwa Dodoma ni kama mnajisumbua tuu!!! Nawashauri msipoteze nguvu na pesa zenu za mkopo.
 
Back
Top Bottom