Kana-Ka-Nsungu
JF-Expert Member
- Oct 4, 2007
- 2,257
- 354
, mind you UK, wamebadili speed limits zao ku accomodate maendeleo, kwa sasa lori ni 95km/h na basi ni115 km/ h kama sikosei
Very wrong sir, niko UK na ni dereva wa miaka mingi, as far as I know speed limit haijabadilishwa. Maximum kwenye motorway kwa mabasi na malori ya chini ya tani 7.5 ni 70km/ph kama ilivyo kwa magari ya kawaida, lori likiwa kubwa zaidi ya hiyo 7.5 max yake ni 60km/ph. Hapa tunazungumzia nchi ambayo ina miundo mbinu mizuri, sehemu nyingi ni tambarare, hakuna kona za ajabu ajabu wala milima, most of their road hasa kwenye motorways zimenyooka, lanes 4 hadi 5 upande mmoja tu, kuna taa barabarani usiku, etc na kupata leseni hapa ni mbinde, watu wanafanya mitihani hata mara 10, hadi ufaulu practical na theory ndo unapata leseni, hakuna longo longo. Pamoja na haya yote, bado wameona hivyo ndio viwango safe vya speed.
Ukija nyumbani, kuruhusu basi litembee hata kwa mwendo wa 100 km/ph tu ni kuruhusu majanga. Una madereva kibao wanaotumia leseni za kufoji au za kununua kwa hongo na hawajasomea kabisa udereva, wamejifunza kiujanja ujanja tu, madereva wengine wakiwa njiani wanawaachia makonda wawasaidie kuendesha, dereva mmoja anaendesha gari mwenyewe for more than 10 hours, hapa mtu anapiga masaa yake 4-5 anashuka, anaingia mwingine. Matumizi ya vilevi hasa pombe, bangi na miraa ni vitu vya kawaida sana kwa madereva na polisi wetu ni mara chache sana kuwashtukia, not sure hata kama wana vifaa vya kutest hizi mambo. Na konakona zetu na mamilima, think of msambiazi (korogwe-mombo) au kitonga (iringa-mbeya), kama huna uzoefu na unakanyaga mafuta tu- lazima utaua watu. Pia kuna head on collisions nyingi kutokana na wembamba wa barabara zetu.
Kwa maoni yangu binafsi hata hii 100 inayotumika sasa ingepunguzwa tu, tumeshapoteza watu wengi sana kwa haya maajali jamani, utashabikia speed tu kama hujawahi kupoteza rafiki au ndugu kwa mambo haya.