Hekima haijawahi anguka wala pata ajali toka ianze.sasa imeanza kuharibu.
Mungu wangu!
Ajali kwa mara nyingine!!
mabasi ya Hekima nayafahamu na ni maarufu sana kwa kuwa na mwendo kasi mkali sana.
Imezoeleka ukitaka kufika mbeya mapema, panda Hekima, Mbeya express au happy Nation.
mdau mmoja amesema Hekima tangu waanze hakuna gari yao imewai kupata ajali.
Hata mimi napata kigugumizi, sijui tumeasi? I dont know kwakweli. MUNGU atusamehe tulipokosea jamani vinginevyo tutakwisha kabla ya wakati wetu!!! It pains once you think twice and deeply. Fikiria umekaa stendi unamsubiri mdogo wako anatoka safari halafu unasikia basi alilopanda limepata ajaliTerrible. Lakini why Tz things like these are daily on the increase?
Kwanini hamuwashushii kichapo hao madereva?niliwahi panda hili basi toka mbeya mpaka dar,kwakweli ilikua ni hatari sishangai likipinduka na kuua wengi,spidi jamaa alikua anaenda nayo ni hatari,nasikia alitoka lusaka zambia saa 12 asubuhi,tumefika dar saa tisa na nusu likiwa ni basi la kwanza kuingia,nilishikilia roho toka mbeya hadi dar,maana hiyo spidi mmh,poleni majeruhi na marehemu.
Inasikitisha sana... lakini ndani ya miezi mitatu tu, tumepata taarifa za ajali hizi nyingi, what's wrong?
nilisafiri hivi karibuni kwa njia ya barabara kwenda mbeya. Kwa kweli hali niliyoiona inatisha. Madereva wengi wa ma-bus wanakwenda mwendo kasi na hu-overtake hata sehemu zisizopaswa ku-overtake. Nilijisemea moyoni "ndio maana ajali nyingi hutokea'. Ajali nyingi zinasababishwa na uzembe wa madereva na sio 'mapenzi ya mungu' kama tunavyokimbilia kusema mara nyingi.
Mbona inasemekana hakuna aliyekufa mpaka sasa, rafiki yangu kapita eneo hilo mda mfupi, anasema imetokea tanangozi mita chache baada ya ile minara mingi ya simu, likiwa linatoka tunduma kwenda dar. Mungu awape faraja yake waliokutwa na tatizo hilo.
Mbona inasemekana hakuna aliyekufa mpaka sasa, rafiki yangu kapita eneo hilo mda mfupi, anasema imetokea tanangozi mita chache baada ya ile minara mingi ya simu, likiwa linatoka tunduma kwenda dar. Mungu awape faraja yake waliokutwa na tatizo hilo.