Bashe: Kuna kikundi ndani ya TISS kinahusika na utekaji. Wabunge 11 wapo kwenye orodha ya kutekwa

Hebu ngoja nikuulize swali dogo tu.

Nape aliunda Tume ya kuchunguza tukio la kuvamiwa kwa Clouds Media na matokeo ya Tume hiyo akaahidi kuwa ataikabidhi kwa Rais.

Unajua nini kilimtokea Nape?

Alifukuzwa kazi kabla hata hiyo ripoti haijafika mezani kwa Rais!

Mbunge Nape alitishiwa kwa bastola pale Protea Hotel ili asiongee na waandishi wa habari, tunakumbuka jinsi Waziri wa mambo ya ndani alivyomuagiza IGP Mangu kuwa mtu yule aliyemtishia kwa bastola Nape akamatwe na afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Wote tunajua kuwa hadi leo huyo IGP wetu hajathubitu kumtia mbaroni yule jamaa aliyemtolea bastola Nape!

Sasa wewe unapomshauri Bashe aripoti tukio la kutishiwa kwake Polisi ni kuwa hujajua kuwa 'Bashite Forces' ni UNTOUCHBLES na haliguswi na chombo chochote cha dola hapa nchini!
Sasa kama mnajua hivyo mnapiga kelele za nini sasa tulieni dozi iingie.
 
Bashe anajijua yuko mguu nje ccm ndo maana kila siku ni kumuandama Magufuli, swali la kitoto Mawaziri waliomwambia ndani ya TISS kuna kikundi kinateka watu kwanini walishindwa kumtajia hicho kikundi ili akitaje bungeni?
hujamuelewa? kasema ana ushahidi iundwe tume akawasilishe! za kukusanya madeni?
 
wapendwa wana jf ninamajonzi makubwa sanaa moyoni mwangu kuwa tanzania ninayoipenda sasa nimeichukia.nikimbilie wapi ili moyo wangu upate amani. nilisikia bungeni viongozi wetu wanalalamika juu ya usalama wao. sisi watoto wa makapuku tulalamike wapi. mungu tusaidie maana hatuna pakulilia zaidi ya mbele ya meza yako
 
wabunge wamezoea kuchukua wake za watu pale Dodoma sasa hivi wenye wake zao waliopowa wamechachamaa ndio maana wanahofia maisha yao achana nao wahuni hao!
 
Huyu ana akili kweli ,bunge lijadili upuuzi wake eti kwa kuwa kaambiwa kuna kundi la watekaji TISS yeye ni kiongozi na anajua wapi kwa kupeleka hizo tuhuma za uzushi,halafu bado anaendelea na uongo wake eti kaongea na Askofu mmoja wa katoliki na kaona dalili za kudorora kwa uhusiano ,huu si upumbavu kwa mbunge anayejifanya msomi na muelewa kwa hiyo uhusiano wa wa JPM na kanisa ukidolola ndio nchi itakufa,na hajui kwamba nchi haina dini huu ni jinga na uchonganishi na ni kutaka kupata huruma ya kanisa,sijui ni kwa lengo lipi,wengine wana kwao sisi hatuna kwetu zaidi ya hapa Tanzania,Bashe aache kutumika kwa ajenda zake za kipuuzi pamoja na kundi lake,kutwa ni kulalama tu kwa mambo ya kipuuzi sijui huko ndio kuwaletea maendeleo wana Nzega.Kama watu wamekutumia ujumbe upeleke mahala panapo husika na si bunge liache kujadili mambo ya maana na lianze kujadili habari za kutunga,waoneeni huruma walipa kodi,hamukwenda bungeni kutengeneza majungu.Unatia aibu Bashe.
Mkuu "mfianchi" zamu yako ikifika hutaongea maneno haya labda kama na wewe ndiyo wahusika wenyewe....time will tell kuambiwa utakamatwa na wanadamu wenzio, hujui lini?, saa ngapi?, mahali gani? lazima uwe na mashaka na huwezi kuwa sawa. Bashe kama amepata "temporarly insane" possibly that's why haoni aibu kusema kilichomsibu. Hajui ninani wakumsaidia. Muacheni kijana wa watu aseme ya moyoni.

Kilakitu mnafanya ni siri. Umetishiwa watu wanataka kuchukua uhai wako pia ufanye siri na una primary evidence kwenye simu yako.. matokeo ya kufanya siri kwa mambo ya hatari kama hayo ndiyo unakuja kuitwa tukutane mahali, unafanya siri, humwambii jirani yako, wala mke wako, wala kutoa taarifa kwa wananchi ama vyombo vya dola. Unakwenda unapotea mazima hujulikani ulipo hata maiti yako haiwezi kuonekana. Maana anayejua ninani aliyekuita ni wewe mwenyewe, umeitiwa wapi ni wewe mwenyewe unajua, umepelekwa wapi ni wewe na sasa victim pia ni wewe mwenyewe na umekufa. Sasa ninani atatoa taarifa umefia wapi? Wakati unayejua umefia wapi ni wewe mwenyewe? na roho imeshatengana na mwili huna kauli? Jamani tuache uvyama tumuonee huruma Mhe.Bashe.

MAOMBI YA MTANZANIA MASIKINI NA MVUJA JASHO, KARIBUNI TUOMBE JUU YA NCH YETU JF:
"EEH MUNGU WANGU NI WAKATI WA KUSEMA KWA SAUTI YA ISHARA NA VIONGOZI WA NCHI YA TANZANIA, MOYO WANGU UMEJAA HOFU NA MAJONZI JUU YA NCHI YANGU BWANA WA MAJESHI TUONDOLEE HIZI CONFUSION, PERSONAL & INTERPERSONAL CONFLICTS, ZINAZOZAA MGOGORO WA KIVYAMA NA BAADAE KITAIFA. MUNGU WANGU SEMA NENO KWA LUGHA YA ISHARA JUU YA TANZANIA ILI TUKWEPE HASIRA YAKO JUU YA YANAYOTOKEA NA YANAYOFANYIKA KWA MAPENZI YA WANADAMU NA WALA SI KWA MAPENZI YAKO MUNGU. TUEPUSHE NA HARUFU YA DAMU KATIKA NCHI YETU, TUEPUSHE NA MIGOGORO YA KIVYAMA, KIDINI, NA KIUONGOZI, TUEPUSHE NA ADHABU KALI AMBAYO UNAWEZA KUIACHILIA ENDAPO SISI NA VIONGOZI WETU TUTAENDELEA KUNGANGANIA KUFANYA MAMBO KWA MAPENZ NA UTASHI WETU. HUKU TUKIJUA KUWA "SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU"

BABA, WENGI TUMELILIA BUNGE LIVE TUMEKOSA, KATIBA MPYA TUMEKOSA, UNQUALIFIED LEADER WAONDOLEWE NAFASI ZAO NAKUPEWA ADHABU STAHIKI NA NAFASI ZAO WAPEWE QUALIFIED TUMEKOSA: NA SASA WIMBI LA KUTEKWA NA KUPOTEA BABA TUMEANZA KUKABILIANA NALO, NA PIA WENGINE WAMESHAPOKEA MESEJI ZA VITISHO NA TAARIFA JUU YA KUTEKWA KWAO BABA. MUNGU ULISEMA SAUTI YA WENGI NI SAUTI YAKO BABA, FANYA KITU KUONYESHA UWEZO NA MAMLAKA YAKO EEE MUNGU WA ISRAEL. ILI KAISARI NA MAFARISAYO WATAMBUE KUWA WEWE NI MUNGU WA ISRAEL, IN THE NAME OF JESUS CHRIST OF NAZZARETH. Amen
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom