William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,588
- 10,376
URAIA WA BASHE:
Nimesema mara Nyingi na leo nasema Tena URAIA WANGU HAUNA MASHAKA hata kidogo, labda nitoe maelezo mafupi hapa, Kutokana na sheria yetu ya UHAMIAJI KUNA AINA MBILI WATU kuna watanzania ambao wanaomba uraia kwakuwa hawajazaliwa TANZANIA inabidi baada ya muda wakaiishi kwa kutumia HATI MAALUM (PARMIT) Ambayo inakuwa re newable wataomba na watatangazwa katika magazeti na hawa wanatakiwa waishi si chini ya miaka 10.
Kundi la pili ni Mtanzania ambae anazaliwa Tanzania na ambae mzazi wake hasa wa kiume wakati mtoto huyo anazaliwa HAKUWA RAIA wa Tanzania,now Commenting on my setuation, BABU MZAA BABA alihamia Tanzania 1949, akiwa na baba yangu waliishi mkoa wa Tabora wilaya ya Tabora mjini,BABU MZAA MAMA aliahamia Tanzania 1902 akiwa na BABA yake aliishi maeneo ya SUMBAWANGA NA BAADAE ENEO LINALOITWA LAHELA NA ALIKUWA AKIJULIKANA KAMA MZEE ABDI ALI WAJINGA, BIBI MZAA MAMA ALIZALIWA BOMA NG"OMBE MOSHI Mwaka 1920, mama yangu mzazi alizaliwa Tabora mjini mtaa wa Mwanza Road.
Ukitazama that background utaona mzazi ambae alihamia Tanzania ni BABA yangu, kwa wanaofahamu historia ya Nchii hii watakumbuka 1957 wakati waingereza wanaandaa mazingira ya kukabidhi uhuru wa TANGANYIKA waliita all MINIORITY SOCIETY ambao walikuwa chini ya British Ambrella, na kuwaambia wana uhuru wakuchagua kubaki na URAIA wanchi walizotoka.
Na wakati huo babu zangu wote walikua na BRITISH PASPORT KWA SABABU WALIKUA WAMETOKA ENEO LA KASKAZINI LA SOMALIA LILIKUA CHINI YA BRITSH COLONY LILIKUA LINAITWA SOMALILAND, ama wachukue UHURU WA TANGANYIKA.
Babu zangu waliamua kuacha URAIA wanchi walizotoka na kuchukua uraia wa TANGANYIKA.
Waliasiliwa na kuandikishwa kama RAIA wa Tanganyika na kukabidhi HATI za uingereza na wao kutambulika kama WATANGANYIKA hiyo ilikua 1957.Hi unaweza kwenda RITA katika Registry za 1957 utakuta ukoo wa babu mzaa mama na babu mzaa baba .kwa mantiki hii wazazi wangu wote ni RAIA wa Tanganyika toka 1957 mpaka 1964 wakawa Raia wa Tanzania. Kwahiyo hoja ya urai wangu haina la kujadili
Ukiangalia 1959 TANU branch office ya Nzega ambayo kwa sasa ni ofisi ya CCM kata, alieitoa na kumkabidhi ofisi ile MAMA AMINA MAUFI wakati huo akiwa ni Mwenyekiti wa Tanu Branch na katibu wake ni Mwl shija ambae sasa ni mkiti wa CCM wilaya ya Nzega alikuwa Marehemu Babu yangu.
Chumba kile lilikuwa DUKA lake nay eye aliwapa ili ofisi ya Tanu ifunguliwe pale,hii ni memory iliyonifanya 2008 nilikarabati Jengo lile liweze kutumika mpaka leo.
NINI KILITOKEA BAADA YA HAPO:
Wazazi wangu walioana baadae na kuzaa watoto sita mm nikiwa mmoja wao,kilichotokea ni kwamba 1986 /7 mzee anaeitwa MZEE RASHID NYEMBO( marehemu) ambae alikuwa Rafiki mkubwa wa Mzee wangu walikuwa na Safari ya Maswala ya kidini mzee wangu hakuwa na Hati ya Kusafiria wakati huo na u can imagine wakati huo hakuona umuhimu wa swala hilo.
Alitakiwa kupata hati alifata utaratibu lakini AFISA uhamiaji wilaya ya Nzega alikuwa anaitwa MR MALONGO na wakati huo kulikuwa na opartion za kukamata wahamiaji na kila wakija watu kutoka makao makuu ama mkoani walikuwa wanamsumbua na kumtaka atoe maelezo ya WHO IS HE.
Alishauriwa ni vizuri aombe UARAI KWA UTARATIBU WA MTU ALIEHAMIA TANZANIA, mzee wangu alifata utaratibu na kupewa HATI YA URAIA CERTIFICATE OF NATURALISATION 1987 na alipata hati na mambo mengine.
Tukumbuke Sheria yetu inatambua MZAZI WA KIUME,kwakuwa niliamua kuingia katika SIASA na ninafahamu hata leo ukipata msichana unaempenda PROTECTION ni MUHIMU basi 2008. Niliamua kwenda mahakamani kukana UARAI WA BABA (si kwasababu sina sifa bali kujilinda kama mtu anapoamua kutumia kondom ni katika kujilinda na un forseen events) lakini bcs kutokana na DOCUMENTATION mzazi wangu wa kiume alipewa HATI ya URAIA 1987.
Na mimi kwa kuwa najua in politics anything can HAPPEN hasa pale linapotakiwa jambo flani kufanyika basi wakati nagombea UENYEKITI WA UVCCM TAIFA NILIAMUA KUWA NA HATI YA KIAPO INCASE OF ANYTHING na hilo likaja kujitokeza likakosa nguvu nikatoa kiapo hoja ikafa, pamoja na kuwaeleza URAIA wangu haukuwa na shaka yoyote lakini pia nilisema nimeisha timiza sharti la kwenda mahakamani nikaitumia.
Na 2009 niliamua kutaka IDARA YA UHAMIAJI INIPATIE CERTIFICATE OF CITIZENSHIP ambayo utaratibu wake nitofauti na ule wa mtu anepewa CERTIFICATE OF NATURALIZATION, 2009 nilipatiwa hati hiyo ambayo mpaka leo ninayo .
Kwahiyo MH MASHA hakupotosha ,mkurugenzi wa UHAMIAJI HAKUPOTOSHA, wala mkurugenzi mkuu wa RITA hakupotosha pale alipotoa ushuhuda wa kimaandishi juu ya uhalali wa wazazi wangu kuwa katika registry ya mkoloni ya 1957 na wote hawa walikiandikia chama BARUA kuthibitisha tena baada ya mimi kutoteuliwa na mimi kuwaandikia Barua ni kitaka kauli yao juu ya upotoshaji uliofanyika,nakala ya Barua hizo ninazo mpaka leo, NIMSHAURI mbunge wangu usiongelee usilolifahamu usiwe mmoja wa wale wanaofumbia macho ukweli kujipa maliwazo ya MOYO.
- Wakuu naomba kusema tena kwamba swali langu kwa Bashe, limetokana na hiiki kipengele, na bado ninamsubiri Bashe atakapoweza aje anijibu kama Rais alisema uongo kuhusu utata wa uraia wake, again swali langu nimelielekeza kwa Bashe sio anybody else!
William @ NYC, USA.