Bashe anusurika kutekwa

hii stori mbona ipo kama imechonwa vile. muda wote ufuatiliwe halafu ushindwe kutoa taarifa polisi. ina maana Bashe hana contact za watu ambao wangeweza kujua hiyo noah wakati anaelekea kwake. maanake isije ikawa ni alibi ya kutaka huruma ya watu. lazima hii taarifa tuipokee kwa tahadhari kubwa. la mwisho kwani Bashe yeye mbaya wake si mmoja tuu na anamfahamu na alikwishamtaja kule Dodoma labda angempigia simu na kumuuliza vipi mzee.

Unazungumzia Polisi ipi mkuu ambayo angetoa taarifa? angefanya hivyo ndo kwanza angewarahisishia kazi kwa walichozidhamiria.
 


JUMAMOSI, MACHI 30, 2013 01:07 NA MWANDISHI WETU, DAR

WIMBI la viongozi wakuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, kuendelea kuwindwa na watu wasiofahamika, limeendelea kushika kasi, baada ya usiku wa kumkia jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Hussein Bashe, kunusurika kutekwa.

Tukio hilo, lilitokea juzi usiku wakati Bashe alipokuwa akitoka ofisini kwake Sinza Kijiweni, akielekea nyumbani kwake Mbezi.

Akizungumzia tukio hilo, Bashe alisema wakati anaondoka ofisini kwake kwa gari lake, alianza kufuatiliwa kwa nyuma na magari mawili, likiwamo aina ya NOA ambalo hata hivyo hakufanikiwa kujua lilikuwa na watu wangapi.

“Kama kawaida nilishinda ofisini kwa ajili ya majukumu yangu ya kazi na muda wa kutoka ulipowadia, niliondoka kurudi nyumbani.

“Awali wakati navuka geti la pale ofisini, sikuwa na shaka yoyote, lakini kadri nilivyozidi kuendelea na safari yangu, niliona nyuma nafuatiliwa na magari mawili ambayo yalikuwa yakiendeshwa kwa tahadhari.

“Nilipofika Mwenge ile NOA ilikuwa bado iko nyuma yangu, sasa nikaanza kupatwa na wasiwasi, nikajua hapa kuna jambo.

“Moyoni niliendelea kumuomba Mungu, huku nikijiuliza maswali mengi hawa jamaa ni akina nani, kwa kweli sikupata jibu zuri.

“Nilipofika Mbezi, niliona yale magari yanazidi kunisogelea, kwa hiyo, nikaamua kuongeza kasi na wao wakazidi kuja tu.

“Wakati niko Mbezi jirani na njia panda ya kwenda kwangu, gari moja lilinipita kwa kasi na kuendelea mbele.

“Unajua kuelekea kwangu pale kuna barabara kama tatu ambazo zote unaweza kuzitumia na zikakufikisha hadi nyumbani kwangu,” alisema Bashe na kuongeza:

“Nilichokifanya nilipita barabara ya kwanza na wao wakapita barabara ya pili na ghafla nilikutana nao uso kwa uso, wakati huo naelekea kwangu na kibaya zaidi, gari lao walizima taa kubwa na kuacha ndogo.

“Walivyona gari langu, walinipiga taa kuashiria wanakata kona, lakini cha ajabu walinifuata nyuma na hapo nikaanza kujua sasa nafuatiliwa.

“Nilichokifanya sikwenda nyumbani moja kwa moja, bali niliamua kupaki gari kwenye grosari moja iliyoko jirani na kwangu.

“Baadaye niliamua kuondoka ili niwazunguke kwa nyuma nisome namba za gari lao, lakini sikufanikiwa kwa sababu taa za nyuma zilikuwa zimezimwa,” alisema Bashe.

Kwa mujibu wa Bashe, baadaye aliingia nyumbani kwake na kuwakuta wageni ambao alikaa nao hadi saa sita usiku baada ya kuwasimulia tukio lilivyokuwa.

“Sasa basi, wakati jamaa zangu hao wanaondoka kurudi kwao, walikuta lile gari pale pale njiani, wakanipigia simu, kwamba lile gari nililowasimulia linawafuatilia.

“Nikawaambia wageuze gari lao ili wasome namba, lakini hawakufanikiwa hata kidogo kwa sababu wale jamaa walishtuka na kuamua kutimua.

“Kwa hiyo, nilichokifanya nilikwenda pale Polisi Kawe na kutoa taarifa ambapo nilipewa RB yenye namba KW/RB/2899/2013,” alisema.

Machi 6, mwaka huu, Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, alitekwa na kuteswa na watu wasiofahamika.

Katika tukio hilo, Kibanda alitobolewa jicho la kushoto, alipigwa kichwani na kitu chenye ncha kali na kunyofolewa kucha. Kwa sasa yuko nchini Afrika Kusini ambako anaendelea na matibabu

Kuna mtu wa KUMGUSA Rostam katika nchi hii,SIAMINI SIAMINI SIAMINI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Hawa walikuwa watu wa kumtia hofu tu,majasusi hawarudii mbinu mara mbili katika kipindi kifupi.
Bashe asiwe paranoid!
 
Nimeisoma story yote, kama sikuruka mistari basi njiuliza hivi; Muda wote wakati Bashe "anafukuzwa" na hao jamaa, hivi hakuona umuhimu na ulazima wa KUPIGA SIMU na kutoa taarifa kwa mtu YEYOTE kuhusu alivyokuwa anafuatiliwa? Kwangu mimi hili ni swali kubwa linalonifanya nisiamini anachokisema huyu bwana!!!!!
 
Hapa Bashe atawadanganya baadhi ya manazi wa Chadema na wapenda majungu wa CCM tu.

Huhitaji degree kujua kwamba hii habari ni ya kutunga.
Mimi ni Mnazi wa CHADEMA Damu damu hajanipata.
labda atakuwa kawapata Ma CCM Menzenu yanayoendekeza Upunguani
 
Wahah!! Mkamateni bashe na nape na Ritz kama kuna mtu atang'olewa tena kucha . Hitakaa itokee tena.
Mkuu hapo kwenye RED unamaaanisha huyu Mtani wetu Ritz hapa Jamvini?
 
Last edited by a moderator:
Hapo kwenye blue, labda uniambie kwamba umetoka shimoni leo hii lakini kama wewe unaishi hapa duniani utakuwa unaelewa kwamba hiki kitu kipo dunia nzima. Mimi nadhani badala ya kulalamika ungeutumia muda huu kufikiria namna ya wewe pia kuwa mtu mwenye nguvu kubwa ya kifedha na ushawishi mkubwa serikalini.
Hapo kwenye blue sikubaliani na wewe. Kwenye blue uliyokua unajibu matukio hayo hayako dunia nzima usigeneralize.
 
Watu wanakosea kufikiri kwamba ati kukamatwa kwa Lwakatare wa CDM basi kila litu kitakuwa shwari!Never!
Watanzania hebu jaribuni kuwa na akili zinazofikiri ahead of your time please!

Watu mnatakiwa kujua ya kwamba Lwakatare hahusiki hata chembe na utekwaji nyara wa Absolom Kibanda???kinachoendelea pale ni The Comedy Show tu! Watekaji wa na watesi wa Kibanda they're still at large(hawajakamatwa)!!!Na usidhani hawajakamatwa kwasababu eti hawajulikani.....!!!?? No sir. Hawa jamaa wanajulinaka mpaka Ikulu na kuna mission ambayo iko well organised ili iweze kuwa accomplished! That is CCM government mission to be accomplished before GE2015!!!

Watu jaribuni kufikirisha bingio zenu. Jaribuni kulinganisha kauli na matendo ya viongozi wa CCM na serikali yake: Kauli za kina Mwigulu Nchemba, Nnape Nauye a.k.z Nnepi Nanyea kuhusu Video(mkanda) wa viongozi wa CDM unaoratibu mauaji ya Watanzania na kauli ya juzi tu ya Zee la nyani- Steven Wassira kuwa UWT hawahusiki na utekaji wa Kibanda n.k. kupitia runinga ya ITV.

Try to connect those dots, then you have the whole picture!!!!!Tanzania tuchangamkeni saa ya Ukombozi ni sasa.
Hebu tujaribu kujifunza toka kwa majirani zetu Kenya na kwingineko ambako hakuna ujinga na upuuzi kama huu unaofanyika hapa Tanzania kwa sasa!

Nimalizie kwa Bashe kwamba kama hizi habari ni za kweli basi KUNA UDHAIFU MKUBWA SANA KATIKA UTENDAJI WA KAZI KATIKA KAMPUNI YAO YA NEW HABARI NA YEYE MWENYEWE! Tulichotaka kusikia kutoka kwake ni kwamba tangu siku ile alipotekwa Mhariri Mtendaji wa New Habari Bwana Kibanda kampuni IMEANZISHA ULINZI WA MASAA 24 KWA VIONGOZI WOTE WWANDAMIZI WA NH ILI KUWAHAKIKISHIA USALAMA WAO WANAPOTOKA MAJUMBANI KWAO NA KUINGIA KAZINI!!!
HATA KAMA POLISI HAWATAKI KUNA SECURITY COMPANIES NYINGI ZINAWEZA KUFANYA KAZI HIZO KWA UFANISI KULIKO HATA POLISI!

USHAURI KWA BASHE: KUANZIA SASA WEKA ULINZI WA KWAKO MWENYEWE 24HRS NA WA VIONGOZI WENZAKO KUANZIA OFISINI MPAKA MNAKOLALA NA MUWE NA SILAHA ZENU WENYEWE ZA KUJILINDA! NINA HAKIKA KIBANDA KAMA ANGELIKUWA NA SILAHA YAKE ILE SIKU ALIYOTEKWA ANGELIMLIPUA HATA MMOJA NA KUWA USHAHIDI TOSHA KABISA WA KUMALIZA KESI ZA KIPUMBAVU KAMA HIZI!!!!HAIWEZEKANI WATU WAKUFUATILIE TOKA OFISINI KWAKO MPAKA JUMBANI YAKO HALAFU USICHUKUE HATUA ZA KUELEWEKA KWA AIDHA KUWAFAHAMISHA ASKARI WAKO AU JAMAA ZAKO WA KARIBU.

WEWE ULITAKIWA KUMPIGIA RAFIKI YAKO WA KARIBU NA KUMJULISHA KUHUSU HAYO MAGARI NA YEYE AGELIKUJA NYUMA TARATIBU AKIFUATILIA NYENDO ZA HAO JAMAA NA LAZIMA ANGEWABAINI TU, UJANJA ULIKUWA SIMPLE, ANGELIWEZA KUTISHIA HATA KUWAGONGA ILI MAKUSUDI TU ILI WASIMAME NA HATIMAYE KUJITOKEZA NA KUWATAMBUA. LAKINI HILI LA KUFUATILIWA TU UMEKAA KIMYA KAMA KONDOO NA ILHALI TUKIO LA KIBANDA BADO LIKO BICHI AKILINI MWAKO NA WATU WENGINE INATUPA MASHAKA!

IT'S EITHER NI YALEYALE MAIGIZO YA THE COMEDY YAKIENDELEZWA KUPOTEZA LENGO OR WEWE MWENYEWE YOU KNOW WHAT'S HAPPENING AROUND YOU!!!
 
Operesheni ng'oa kucha, meno na macho bila ganzi inaendelea. Je ni nani yuko nyuma ya matukio haya?
Sidhani kama bwana mdogo Kigwangala ana maujuzi haya.
Uraia wa Bashe nao uko mashakani licha ya kuwa Uhamiaji ilisha tusadikisha kuwa Bashe ni raia halali wa Tz
........Lwakatare na Ludo, teh teh teh teh
 



OFISA Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, Hussein Bashe, amedai kuwindwa na watu wasiojulikana wakati akitoka kazini kurejea nyumbani juzi usiku.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Bashe alisema wakati akitoka kazini kuelekea nyumbani kwake, aliona bajaji, gari ndogo na lingine aina ya Noah yakimfuata.

"Ili kufika kwangu kuna barabara tatu tofauti zilizo karibu, na zote zinaingia barabara kuu, niliamua kutumia njia ya kwanza, lakini ghafla nikaona gari lile likaingia barabara nyingine likaanza kunimulika kwa taa kali, kadiri nilivyokuwa naenda walipunguza mwanga.

"Niliona ni gari aina ya Noah yenye rangi ya fedha ya muundo wa kizamani, nilipotaka kupinda kulia ikanifuata, nikapunguza mwendo na yenyewe ikapunguza mwendo, nikakata kulia hiyo gari ikanifuata pia," alisema.

Bashe aliongeza kuwa alikata kushoto ilipo nyumba yake, na gari lile lilimfuata, hivyo akalazimika kusimama kwa makusudi kwenye grosari jirani na nyumba yake ndipo gari lile likapitiliza kwenda kwenye giza.

Aliongeza kuwa alipoingia nyumbani kwake alikuta wageni wake wakimsubiri na baada ya kumaliza mazungumzo nao waliondoka, lakini walipotoka nje ya lango gari iliyomfuata awali ilijitokeza na kuwafuata wale wageni.

Bashe alisema wageni hao walimpigia simu wakimweleza kuwa wanafuatiliwa na gari alilokuwa amewasimulia.
Alisema kuwa aliwashauri wafuate barabara ndogo ingawa bado lile gari liliendelea kuwafuata, lakini walipoamua kugeuza ili wakutane nalo lilitimua mbio kuelekea Tegeta.

Wakati anazungumza na gazeti hili, Bashe alisema kuwa bado hakuwa ametoa taarifa katika kituo cha polisi Kawe, lakini tayari alikuwa amemwarifu Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi.

Hii si mara ya kwanza kwa Bashe kuwindwa kwani aliwahi kusimulia mkasa kama huo na kuwataja watu aliowahisi siku chache kabla Mhariri Mtendaji wa New Habari na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda kutekwa na kujeruhiwa.

Akizungumza katika kikao cha wadau wa habari kilichoongozwa na Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Bashe alisema wiki tatu kabla ya tukio la kuvamiwa Kibanda, alishuhudia gari la polisi likiwa limebaki nje ya ofisi yao saa 5 usiku na walipotoka liliwafuatilia.

"Kabla ya tukio hilo kumkuta Kibanda wiki tatu kabla, tulitoka ofisini saa 5:00 usiku na kwa muda mrefu nje ya ofisi lilipaki gari la polisi aina ya gofu lililokuwa na namba za usajili PT 180," alisema.

Alisema kwa kuwa yeye na Kibanda wanaishi Mbezi, walipotoka walifuatana lakini cha ajabu gari hilo lililokuwa limepaki nje ya ofisi yao na kuelekea upande wa Shekilango liligeuza na kuwafuata.

"Gari lile liligeuza likatufuata nyuma hadi eneo la Makaburini mbele ya Mwika Bar, likazuia gari yangu na baadaye kupaki nyuma.
"Hawakushuka, lakini baada ya dakika tatu, nne hivi akashuka askari mmoja. Nikawasha taa za gari ndani kwa sababu nilikuwa na mwenzangu nikamuuliza unataka nini? Akasema tunalitilia shaka gari lako, nikamwambia nimewaona ofisini na sasa mnatufuata, mnataka nini? Lile tukio tuliripoti polisi," alisema Bashe.

Alisema wakati hayo yanatendeka, Kibanda alikuwa ameegesha gari lake upande wa kulia wa barabara na kwa kuwa naye aliona tukio zima, alimpigia simu na kumpa tahadhari ya kutoshuka kwenye gari.

Bashe alisema pamoja na mambo mengine alimjulisha Waziri wa Mambo ya Ndani.
Hata hivyo tangu hilo gari la polisi litajwe kuhusika kumfuatilia hakuna hatua zilizochukuliwa hadi alipofuatiliwa tena.

Source: Tanzania Daima Jumamosi.

Mytake:


  • Hivi sasa waandishi wa habari wana hofu juu ya usalama wao!,
  • wanasiasa ndani na nje ya chama tawala wana hofu wana hofu ya kuhujumiana!,
  • waumini wa dini wana hofu ya kuhujumiwa na watu wa dini nyingine
  • na wananchi wengi pia wana hofu na usalama wao..
Ni muhimu sana vyombo hivi sasa vikafanya kazi kwa matendo kuliko maneno!!!..
 
Maadam umeshajua kuwa wanakufuatilia ni vyema uchukue tahadhari wakati wote. Hata Mwakyembe alianza kuriporti polisi juu ya matukio ya kutishiwa kwake lkn walibaki na propaganda mpaka alipopatwa na matatizo. Hivyo hivyo ukiona unariport hakuna linalofanyika na zaidi majambazi ndio yanazidi kukufuata, ujue yanatoka huko huko unakoenda kureport.

HAKUNA IMANI TENA NA POLISI NCHI HII: hii inasikitisha sana watu wanahangaika na usalama wao kama watoto yatima. viongozi wa dini nao ni hivyo hivyo, raia wengine nao ni hivyo hivyo.

Nadhani viongozi husika laana zinawafuata nyuma maana hii hali sio ya kawaida.

nakushauri ya fuatayo;
- muda mwingi usiwe peke yako, ili hata ukipatwa na matatizo basi awepo wa kutoa taarifa haraka
- tumia gari tofauti tofauti mara kwa mara
- weka CCTV camera kwenye gari lako ili tuwatambue hata siku wakifanya tukio
 
Back
Top Bottom