BASATA yatangaza kumfungia Ney wa Mitego kujihusisha na sanaa kwa muda usiojulikana

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
BASATA yatangaza kumfungia Mwanamuziki Ney wa Mitego kutojihusisha kabisa na kazi za sanaa kwa muda usiojulikana.

Hatua hiyo imetangazwa na Katibu Mtendaji wa BASATA leo JIjini Dar.
 
Baraza la Sanaa Tanzania BASATA limemfungia Mwanamziki Ney wa Mitego kutokana na nyimbo yale pale kati ambayo inakiuka Maadili.

Kifungo hiko ni cha muda usio julikana.

source: EATV
 
Mimi ninachojiuliza ni hivi mtu yeyote huko duniani akitunga wimbo wenye 'maudhui' yaliyo tofauti na Tanzania hairuhusiwi kuusikiliza hapa!? Tuchukulie uko katika lugha tofauti na kama tunavyojua wanamuziki ni wengi duniani na kila mmoja anatoa wimbo wake. Sasa Ney wa Mitego sijui akienda akarekodi wimbo tuseme Amerika, Ulaya, Asia nk wakaupenda alafu TZ na basata yetu tukaupinga, hao basata wataenda huko duniani kuwaambia wamiliki wa tv, maredio na mitandao kuwa "huo wimbo mnaupenda lakini sisi TZ tumeupiga marufuku na nyie hamruhusiwi kuusikiliza"!
Mbali na hapo ni kuendelea kushikilia mitizamo finyu ya kuamini kuwa ukimhoji shoga unapelekea ushoga kushamiri wakati ulikuwepo kabla hata redio hazijakuwepo.
 
Mimi ninachojiuliza ni hivi mtu yeyote huko duniani akitunga wimbo wenye 'maudhui' yaliyo tofauti na Tanzania hairuhusiwi kuusikiliza hapa!? Tuchukulie uko katika lugha tofauti na kama tunavyojua wanamuziki ni wengi duniani na kila mmoja anatoa wimbo wake. Sasa Ney wa Mitego sijui akienda akarekodi wimbo tuseme Amerika, Ulaya, Asia nk wakaupenda alafu TZ na basata yetu tukaupinga, hao basata wataenda huko duniani kuwaambia wamiliki wa tv, maredio na mitandao kuwa "huo wimbo mnaupenda lakini sisi TZ tumeupiga marufuku na nyie hamruhusiwi kuusikiliza"!

Tatizo hapo ni siasa......Ney wa Mitego alizunguka nchi nzima kumnadi Lowassa naona sasa ndio anapata konsekwensezi. Kwani nyimbo ngapi ziko ovyo tu hazifungiwi.
 
Vipi kama Ney akibadilisha Jina.....Na Je wamemwambia kujihusisha na maswala ya sanaaa....vipi yaani hata kwenda kwenye matamasha, au kuangalia kwenye tv? Vipi kama atafanya ila atalenga soko la burundi au kenya
 
Nyimbo nyingi za wasanii zinamatusi yaliyojificha. Wimbo wa Koffi Olomide ekotite nao ni ishara ya matusi kwamba haijaingia/haijazama kwa hiyo twanga foto mzigo ukiwa nje.

Kwao hawaupendi lakini huku bongo watu meno nje. Tukiamua kupitia mashairi ya nyimbo basi tutafungia nyimbo nyingi.

Kuhusu Ney wa Mitego, hapo kati patamu sijajua ni kati ipi lakini kama watu wametafisi ni kati ya kichwa na nyayo basi ni tatizo.

Yupo Man Fongo anasema hainaga ushemeji tunakulaga. Huu wimbo unahamasisha kukosa uaminifu kwa mke wa kaka yako au jamaa yako. Nao haufai.
 
Duhhhhhhhhh, naanza kukuelewa. Hope hapo kuna zaidi ya wimbo. Sijui kama Ma-imvi hauswi hapo?
 
Smokey D
S.L.P Unknown
Africa,
Ney Wa Mitego
S.L.P Dar
Tanzania

Ndg Mr Ney

YAH:Kutoa Track Nyingine Mpya na Kali Zaidi Ya Pale Kati Patamu iitwayo "Pale
Nyuma Patamu"

Rejea kichwa cha somo hapo juu..
Ni mimi shabiki wako nguvu nakubali mziki wako hata kama kuna haters wanauchukia.Nimesikitika sana kusikia eti ulewimbo wa Pale kati patamu umefungiwa na Basata na isitoshe eti na wanakufungia kutojihusisha na mziki kwa mda usiojulikana Duh!!
Nasikitika sana hautotoa video yake ya Pale kati patamu..Ukimaliza hicho kifungo naomba utoe Track nyingine kali ya "Pale Nyuma Patamu" au "Fumua Marinda"

Wako Shabiki Wa Damu

Smokey D
 
Hilo jamaa nalo limenichosha lifungiwe tu, kila siku kuimba upumbav tu
 
nimesikia pia kipindi cha XXL cha Clouds FM wakisema. siungi mkono hii kitu sababu Nay atakuwa na watu wengi wanamtegemea kwenye sanaa yake, ningemshauri Nay awaombe radhi basata au aende kwenye vyombo vya sheria,
basata pia watumie busara, inakuwaje nyimbo tu zinafanya msanii anafungiwa daima!
 
Hawana uwezo wa kumzuiya Ney asifanye anachotaka kufanya, labda tu kama Nay atakuwa ni goigoi wa sheria.

Hao Basata walimfungia Shilole CCM wakamtumia kwenye majukwaa ya kampeni kama kawa hawakubinuwa mdomo wao.

Nay aendelee na kazi zake kama kawaida zile ambazo hazina maadili ndio zizuiwe kwenye redio na tv ila huku online Basata hawana mamlaka hata chembe.

Hii ndio shida ya taasisi za kale kuongozwa na watu waliopitwa na muda

Hivi ni nani asiyependa pale kati? Kuna shida gani kupasifia pale kati? Hawa Basata wana akili timamu kweli?
 
Kamanda ney usikate tamaaa yote ni kwa sababu uliunga mkono ukawa
 
Wakuu kuna stori zinaenea chini kwa chini kwamba rapa nay wa mitego amefungiwa na BASATA kutokufanya mziki kwa mda usiojulikana. Mwenye taarifa atujuze jamani kama ni kweli jamaa kapingwa shoka na basata
 
Back
Top Bottom