Barua ya wazi kwa mkurugenzi wa usalama wa taifa

Status
Not open for further replies.
Just,
asante kwa wazo lako la kiungwana na kuipenda nchi yako kama TISS wanatembea JF watakuwa wametusikia na kupata changamoto.
 
wote hao wanafanyiwa vetting lakini kwa sheria za nchi yetu na mfumo wetu TISS wakibaini tatizo ni nini wanatakiwa kufanya kisheria si kimtazamo wetu. Je, wanamwambia TENDWA, Mahakama, RAIS au nani? Rais ni wa CCM je akiondolewa mgombea wa upinzani!!!!

Ama kuna mapungufu kwenye sheria zetu au mfumo wetu wa kuwajibishana. sheria mbovu zinatakiwa kuondolewa na TISS au Bunge????

mama porojo una hoja zenye mashiko ni kweli mwenye malaka ya kuondoa hizo sheria mbovu ni bunge lakini kwa professional tactics naamini TISS wanaweza kuzisukuma maana wanasiasa wa kuzisukuma ndio wa kwanza kuhakikisha hazifiki bungeni (no political will)
 
Just,
asante kwa wazo lako la kiungwana na kuipenda nchi yako kama TISS wanatembea JF watakuwa wametusikia na kupata changamoto.

nashukuru si unajua yule raisi wa marekani alewaambia vijana wasiulize marekani imewafanyia nini bali wajiulize wao wameifanyia ni amerika. kwa hii barua yangu ya wazi naweza nikawa nimechangia kitu kwa taifa langu
 
Mama Porojo ulichosahau ni kwamba Tanzania ya sasa haina Idara ya usalama wa Taifa,nasema haina kwasababu haifanyi kazi kabisa ya kuwatetea wananchi,nakumbuka vizuri sana enzi za utawala wa Baba wa Taifa mwalimu Nyerere alikua akipata habari zote za nchi kupitia kwa idara hii na ilikua ikifanya kazi vizuri sana ndani na nje ya nchi,wakati ule ili uajirie Usalama wa taifa Taarifa zako zilikua zinakusanywa toka ulipozaliwa hadi hapo ulipo,siku hizi hawaajiriwi kwa kuchunguzwa kama zamani,sasa hivi ni "unamfahamu mkubwa gani"basi unaajiriwa.
Leo hii Nchi yetu inakaribia kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe hakuna hatua yoyote inayochukuliwa,huu uchomaji wa makanisa kianchofuata ni Hatari sana kwa Taifa letu na usalama wataifa wapo na wala hawajui wafanye nini.
 
Mkuu hongera sana, tunataka moyo wa kizalendo namna hii, ni kweli pengine Mkuu wa Usalama wa Taifa hakufikiria kuwa ana nafasi kubwa sana katika nchi hata kumzidi rais maana hata rais kiusalama anamtegemea Mkuu wa Usalama wa Taifa na Taasisi yake. Na kweli kabisa, rushwa nayo ni tishio kubwa sala na usalama wa taifa, tatizo wao wanafikiria zaidi vitendo vya kigaidi bila kuingiza rushwa kama kimojawapo wa vitendo hivyo vya kigaidi.

Zaamani Tasisi hii ilikuwa inafuatilia kwa karibu sana teuzi za viongozi, maadili ya viongozi, na nachelea kusema, miaka ya nyuma huwezi chaguliwa hata ukuu wa Wilaya bila Taasisi hii kukufanyia kazi na kujiridhisha, je haya hayapo tena siku hizi? ama tuseme wameshastaafu wote waliokuwa wanafanya kazi huko na sasa wameingizwa wapya ambao hawajui kilicchokuwa kinafanyika siku za nyuma?

Siku za nyuma, hata ungizwaji wa fedha ungefuatiwa, lakini sasa hivi watu wanatoa arushwa kwa mifedha mingi, je wanazipata wapi fedha hizo? Ama tuseme kuundwa kwa TAKUKURU kumepunguza kazi kwa Taasisi hii? Ukweli inatisha kuona sasa mambo hayapo kama inavyotakiwa hata katika teuzi, chaguzi usalama haupo.

Sasa inmefikia wakati kwa wachache katika TAASISI hii nyeti kufanya kazi kama ilivyokuwa nyakati zile ambapo mtandao wa Taasisi hii ulifanya kazi nzuri na hivyo kuilinda nchi dhidi ya maadui wake na kusimamia teuzi mbalimbali za viongozi hali iliyotufanya tuwe na viongozi bora na wazalendo.
 
Tatizo kubwa la nchi yetu kimfumo liko kwenye sheria na siasa huko kukikaa sawa vyombo vingine vyote vitakuwa vimejipanga mstari mmoja.

Acha kutuzuga hapo hata kama sifanyi kazi kwenye hiyo taasisi logic inatosha kuniambia ni failures...Unawezaje kusema mfumo ukikaa sawa wote watanyooka huyo wakuifanya ikae sawa ni kina nani? Ama hata neno lenye inteligence katika direct meaning halisaidii kukuonyesha what is wrong?

These people are supposed to be super brains, of high integrity na wenye uwezo wa kuleta positive change wakati mwingine hata dhidi ya mfumo if they know what is prime objective kulinda usalama na integrity ya nchi....

Kama nako huko kwenye hicho chombo kinachoitwa intelligence thinking ya hao waliopo ni hii kama yako basi Mungu saidia acha wenye imani tusaidie nchi yetu maana huwezi kutegemea success from failures!

Its pity by all standards kutetea TISS katika huu uozo uliopo...If they cant use sheria basi watumie integrity na brain zao!..Mbona kwenye kulinda uovu wanafanikiwa kama ilivyo bainishwa na kina kubenea? Lakini hata huko pia kwasababu ya incompetence wameshindwa kufuta traces zao.....

Nchi imekuwa ikiabishwa before our eyes bado mtu anakuja kutetea hiyo incompetence ya hao watu....God forbid nashukuru am not part of that ugly thing and I hate it with all my heart!

Sina ujasiri wa kujiita mtanzania kwakua tu mbele ya macho ya mataifa wote tunaonekana waongo mafisadi people who can never be trusted wengine tunalipa hiyo image kwakushindwa kuwa convince not everybody from that country is the way things happen in general! Unahangaika ku-prove integrity yako mpaka saa nyingine unajuta kuzaliwa Tanzania!
 
Rushwa si kosa la TISS
wakati TAKUKURU ipo kwa mujibu wa sheria na chombo kinatumia kodi zetu
kujiendesha.

Kama tunataka kazi ya TAKUKURU kuwa ya TISS fungu la kupambana na rushwa
kutoka hazina lipelekwe TISS na TAKUKURU ivunjwe
tatizo si kuiondoa taasisi ya kupambana na rushwa la msingi ni TISS na TAKUKURU to work as a tim, ilikupunguza gep la rushwa TZ.
 
tatizo si kuiondoa taasisi ya kupambana na rushwa la msingi ni TISS na TAKUKURU to work as a tim, ilikupunguza gep la rushwa TZ.


sawa kabisa ndugu malofyo kinachohitajika kwa sasa ni hatua madhubuti maana muda si mrefu tunaweza kuwa na genge la wahuni watakao kuwa wanasumbua serikali na wananchi wake
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom