Mkuu wangu usitake kunichehesha miye weee. sasa swala la kitimoto linahusiana vipi na Ukristu. Ni wapi imehalalishwa au unachukua mfano huu kwa maana kwamba kula kitimoto ni tusi kwa Mkristu?.. mbona sikuelewi? kitimoto chakula iweje liwe swala la Ukristu!..yaani leo hii miye nikimwambia mkristu kwamba anakula kitimoto itakuwa namtukana hata kama miye ndio namuuzia kitimoto chenyewe.. aaah mkuu wangu tafadhali, Mphililino ana kula mbwa na huwezi kusema ni tusi kwake bali sifa ya chakula chake ukitaka nawe onja!.Mkuu Mkandara, Hoja zinapokuja kijumlajumla hujibiwa kijumlajumla vile vile! Kwa mfano Wakristo wanapoambiwa kuwa wanakula kitimoto ili hali baadhi yao hawali (eg Wasabato), Waislamu nao huambiwa hawajasoma na ni watu wa kulalamika tu! Ukweli nionavyo mimi sio Waislamu wote ambao hawajasoma! Wapo maprofesa waliobobea kama akina Issa Shivji, Safari, nk. Kwa hiyo kama pande zote mbili zingekuwa zinajadili mambo kwa kutumia isolated incidences tusingefika huko! Kwa hiyo ukileta hoja za jumla dhidi ya Dini nyingine utegemee majibu ya jumla! Pia umenishangaza sana unapokuwa na makengeza kiasi kwamba huoni matusi tunayoporomoshewa sisi Wakristo! Kwa hiyo Mkristo yeyote akisoma hoja zako zilizokuwa biased naye atatoa hoja zilizokuwa biased, mwisho wa siku utadai kuwa HATUKO PAMOJA! Wewe unachangia kwenye juhudi za kutaka TUSIWE PAMOJA kisha mwisho wa siku unadai tuko pamoja kivipi! Pamoja na hayo Wakristo wamekewa wanawa-criticise akina Mkapa, Lowassa, nk hapa JF, hatujaona wakikingiwa kifua kwa sababu ya Ukristo wao! Mtikila pamoja na wachungaji waliojihusisha na DECI wamefikishwa mahakamani, Wakristo wameacha Sheria ichukue mkondo wake. Kwa upande wa baadhi ya Waislamu hali ni tofauti! Kwanza waliochoma makanisa tuliambiwa kuwa ni "wahuni!" Kisha "wahuni" hao walikamatwa tuliona CUF ilivyofanya juhudi kubwa ya kuwatetea "wahuni!" Mpaka sasa hatuelewi kwa nini baadhi ya Waislamu hao wametuchomea Makanisa yetu moto na mbaya sana kutuibia vifaa vya Kanisa! Utani wa watoto ulichukuliwa kama ugomvi wa Wakristo na Waislamu! Suala la Muungano kule Zanzibar limechukuliwa kuwa ni la "kikanisa" zaidi! Hatujui baadaye litaibuka lipi! Kuhusu Zitto, akiona CDM hawamkubali dawa si kuibua hoja ya kidini, aende Chama ambacho anaona kinamfaa! It is strange kuwatuhumu watu hawakupendi ili wakupende! Just like Mwakyembe alipodai Serikali inataka kumuua huku akiendelea kuwa kwenye Serikali hiyo hiyo! Tena anapoweka hoja hizi dhaifu anazidi kujimaliza kisiasa zaidi! Wewe endelea tu kumchimbia shimo! Nawasilisha!
Haya mambie hoja yangu ilokuwa Biased? maana tunapozungumzia chombo kilichoundwa na watu tena Watanzania walokaa na kuuziana mali ya Taifa inakuwaje iwe swala la Ukristu?. Nielewe vizuri nachosema miye, zile shule na Hospital zilikuwa za Mjarumani au kanisa sio mali ya wakristu na wala watanzania hawakumiliki mali zile. That is the fact na ndio maana Nyerere alizitaifisha. Na hata ukirudi ktk swala la shule na Hospital za Aghakhan hazikuwa za waislaam bali za Aghakhan ambaye alitoa huduma za elimu na Afya nchini na zilipotaifishwa zilitaifishwa toka kwa AghaKhan sio kwa waislaam..That is the Fact, achana na habari za kina Mohammed Said..
Hivyo kama kesho Aghakhan akirudishiwa shule mimi hapa siwezi kusimama na kudai ati waislaam wamerudishiwa shule zao. Huu utakuwa ujinga kwangu maana huyo Aghakhan ataendesha biashara yake ya kutoa ELIMU na AFYA na hatakuwa anatufanyia hisani Waislaam hata kidogo, bali ni biashara kwake na katarget market ya biashara zake kwa waislaam ama kutumia Uislaam. Huyu hana tofauti na Wachina au wakorea huku majuu hawa ndio utawakuta wakifungua maduka na kuuza vitu vya watu weusi na kutuita - BROTHER! we are same same brothers.. Think large, lini Mimi Mtanzania mweusi nikawa na Ukaka na Mchina au Mkorea?...