Barua ya Waislamu kwa Katibu Mkuu wa CCM Kupinga Mahakama ya Kadhi...

Status
Not open for further replies.
tupimane kwa kupigana tutajua wapi wengi hivi tunapiga kelele za bure

Si mlipiga majengo (makanisa) mkaishia mahabusu mkuu? Mlidhani mkileta chokochoko yangetokea mapigano? Hiyo ndio "haki sawa kwa wote!"
 
unamtisha nani wewe!amini unachotaka na unafiki wako..we nani kwani mpaka uanze kutishia watu,ukitaka pia hamua unavyoamua mdini mkubwa wewe..eti zitto anachukiwa sababu ya imani yake!!basi amua unachotaka kuamua acha unafiki wako watu tunakuchora tu kisha tumekudharau siku nyingi.

Mzee mzima umekuwa mnafiki kiasi hicho,vijana watajifunza nini kwako??!!..yani wewe kila mjadala wa udini hukosekani alafu haujiulizi mbona wazee wenzako wapo sobber na mambo ya udini au hawaoni izi thread!!

Badilika we mzee unafiki sio mzuri..
Napenda sana pale mtu anaponiita mnafiki wakati hana mfano zaidi ya kwamba nimpendeze yeye...na sidhani kama unaelewa maana ya Mnafiki isipokuwa unalitumia tu neno hili kama mnavyotumia Pepo....

Mkuu wangu simtishi mtu wala hakuna anayetishika hapa JF.. bali nawaambia ukweli usoupenda kuusikia. Mnafiki yeyote angesema uongo, akaahidi asitimize na hata akiaminiwa haaminiki, hivyo sijasema uongo bali ukweli unaojieleza wazi kabisa hapa hapa JF kutoka vivyanu mwenu. Itakuwaje nyie mseme hamna Udini lakini kila siku hamkosi kuandika mada zisizopungua mbili kuhusu Waislaam tena kwa ubaya na dharau - watu ambao mnadai ni ndugu zenu, majirani zenu (Uongo mkubwa) kuwasema hawakusoma, wajinga tena mnamtukana hadi mtume wao halafu mnataka sisi tuwaamini kwa lipi.

Nimesema mnamchukia Zitto kutokana na imani yake maana mnazo agenda zenu na sasa zinajitokeza wazi kabisa na narudia kusema itakula kwenu. Zitto ana matatizo yake lakini sii wa kumchukia kiasi hicho - hapana kuna siri nyuma yake maana huyu huyu Zitto akifanya vizuri bungeni, Oooh! Zitto wetu wa Chadema... akiharibu anaitwa kibaraka kwa nini asiwe kibaraka hata anapowakilisha hoja mnazopenda kuzisikia!..Hivyo wala usinishtukie miye bali jishukieni wewe mwenyewe maana tumeshawagundua janja yenu na haitafika mahala...Kila siku tuko pamoja - Pamoja wapi?..
 
Umejitahidi sana kuandika maelezo marefu ukidai ni barua toka huko ulikoeleza. Ila jambo la msingi ni kwamba huna haja ya kutunga barua au kutoa maneno yeyote ambayo yanaonyesha upogo wa ufahamu. Jua kuwa hata kama barua hiyo ni ya kweli imeandikwa na huyo aliyesaini hapo chini, bado ukweli wa mambo utabaki palepale. Angalia makundi haya: WAUMINI, WANAFIKI NA MAKAFIRI. Kafiri muda wote humtumia MNAFIKI ili kuvuruga mipango ya ndugu zake kwa maslahi yake binafsi ili MAKAFIRI wapate kupitisha mipango yao. Ndio maana M/Mungu ameahidi adhabu kali sana kwa wanafiki.
Dai la waislam kutaka Mahakama ya kadhi lipo palepale na wala halina mgawanyiko kama barua yako inavyoeleza. Jambo la msingi hapa ni kuvumiliana kwa yale ambayo kundi moja la dini linapohitaji serikali yao kuwatimizia matakwa yao. Niwapongeze sana waislam wa TZ kwa uvumilivu wao wa muda mrefu juu ya serikali zao na hata watu wa kundi jingine la dini. Waislam ni miongoni mwa walipa kodi wakubwa kabisa katika nchi hii, wanapokuwa na mambo ambayo wanahitaji serikali yao iwatimizie, si busara kundi moja la dini nyingine likasimama kati na kuishawishi serikali isitekeleze matakwa ya waislam. Ila busara ni kwamba kundi hilo jingine (wakristo) nao wajenge hoja zao kwa serikali yao kuomba mahitajio yao nao watekelezewe. Siku zote huwa nasema, MTOTO mwenye roho mbaya na UCHOYO hupenda kila kitu apate yeye.

Nilipo BLUE.

Nimelipenda sana neno hilo kwani lina kila sababu ya kuitwa kuwa UMENENA KWELI.

Mash'kuura

Mkuu Mkandara,
Hoja kuhusu "Zitto kuchukiwa kuhusu Uislamu wake," napenda kuizungumzia kama ifuatavyo:
1. Imeonekana kama Zitto ni mwislamu pekee aliyepo CDM kwa vile kila anapokuwa critisized hukingiwa kifua cha udini! Kwa namna hiyo mtamwangamiza kisiasa badala ya kumsaidia kama kweli anataka kuwa Rais wa nchi! Hoja ya udini wake inafaa sana kama anataka kuwa kiongozi ndani ya chama kingine, km CUF, CCM, nk
2. Maneno na Matendo ya Zitto yanaonesha anatumiwa na CCM kwa ajili ya kuangamiza upinzani, hili liliwahi kusemwa hata na mama yake Zitto! Lisemwalo lipo, kama halipo liko njiani linakuja!
3. Zitto amebadilika sana tangu alipoteuliwa kwenye Tume ya Mikataba ya Madini, sio Zitto yule ambaye gari lake liliwahi kusukumwa alipofukuzwa Bungeni! Zitto wa sasa ni "Shibuda type" anayetaka kuwa Rais huku akijua umri wake hauruhusu! Ni mtu ambaye amekuwa mtetezi kiaina wa mafisadi:
(a) Hakutaja orodha ya walioficha fedha nje ya nchi. Zitto wa zamani hilo lisingempa tabu,
(b) Alitetea ununuzi wa mitambo chakavu ya Dowans huku akijua kuwa Sheria ya Manunuzi ya wakati huo hairuhusu. After all kampuni yenyewe ni ya kifisadi! Zitto wa zamani asingefanya upuuzi huo.
4. Zitto mpya atafanya fyongo kisha mkimsema atakimbilia mwavuli wa udini! Kama hajui Zitto anajiangamiza zaidi kisiasa kwa karata hii!
5. Zitto angejifunza kwa akina Abdallah Safari, Arfi na wengineo ambao hatujaona wakieneza "kuonewa" kwa sababu ya Uislamu wao, otherwise Ikulu ataiona tu akialikwa na Rais atakayekuwepo!
 
Last edited by a moderator:
Wapi nimemhiusisha Slaa na Ukristu. Hivi ipo connection kati ya Slaa na kanisa?...Nilichosema mimi ni kuhusu Lipumba kuzungumzia swala la serikali kuzungumza na maimamu, sikuona kosa lolote na nikasema wazi kwamba nilitegemea wewe ungemwambia Slaa awambie serikali maana swala hili sii dogo kama mnavyolifikiria.

Na kwa ujinga kama huu litawagharimu sana, nyie jiingizeni mkenge wenyewe. Na sasa naamini kabisa kumbe sababu za kutomkubali Zitto zinahusu pia imani yake ya dini maana kama mnaweza kuwatukana hivi waislaam halafu mnadanganya watu kwamba Chadema haina Udini, inao wanachama wakati maneno yenu wenyewe yanakinzana - tuamini lipi?..hivi mnafikiri sisi wajinga kiasi gani?...

Viongozi wa Chadema kuweni macho sana na watu, na wala msifanye mzaha hata kidogo maana inatisha. Nanyi ikina Sweke maana kikwetu sisi Sweke ni kumfukuza mbwa, hivyo nawaomba sana msiendelee kuwafuga watu kama hawa. Bora mara kumi mkuu wangu bishaa na hao kina Ritz kuliko kuniweka mimi ktk mtihani huu maana unaniaminisha nisotaka kuamini...
Kwani mimi nimekuambia unamuhusisha Slaaa na Ukristu?
Nilichokuambia ni hiki
quote_icon.png
By sweke34

Wewe mpaka ukitokea ujinga/udaku unaokihusisha chadema na kanisa ndiyo utaanza kulialia kwamba Slaa ajitokeze kukanusha habari hizo.
J
icho lako linaona upande mmoja tu kwa sababu umevimbiwa sana na udini...!

Nikikumbuka posts zako za kwenye ile thread ya Zomba/na threads nyingine.
Post ya 183 page ya 10 kwenye uzi wa Zomba(Kashfa ya Chadema na Kanisa Katoliki)

quote_icon.png
By Mkandara

zomba,
kwanza siwezi kubishana na wewe ikiwa habari hii imetolewa gazetini. Na nawashangaa sana watu wanaokuja hapa kupinga habari hii lakini sijaona ushahidi wowote kuonyesha tofauti. Nawaomba viongozi wa Chadema walichukulie swala hili umuhimu zaidi kwa sababu karata ya dini inapotumika inaweza kabisa kukisambaratisha chama.

Zamani sikuwa naamini kabisa kwamba tofauti zetu za dini zinaweza kuingia ktk utawala na hasa serikali lakini sivyo tena hasa baada ya serikali yetu kurudisha mfumo wa mkoloni ktk elimu na Afya. Na zipo kauli za Dr.Slaa ktk utoaji wa elimu bure zinatatanisha, hivyo maadam ni mwanachama wa JF tunamuomba sana aje hapa kukisafisha chama na hatua kali zichukuliwe dhidi ya gazeti hili laa sivyo sioni sababu kabisa ya watu kutetea kitu wasichojua ukweli ni upi..
Ulitaka Slaa aje kuthibitisha habari zinazotoka gazetini kuhusu chadema kujihusisha na Kanisa Katoliki, lakini hii barua ya Waislam ya kwenda kwa Katibu Mkuu wa CCM wala hutaki hata kuiamini. Hapo ndipo nilipokuona kwamba jicho lako limekaa kukosoa tu upande mmoja na ndiyo maana nikakuambia umevimbiwa na Udini.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/315041-kashfa-chadema-na-kanisa-katoliki-10.html
 
Kwani mimi nimekuambia unamuhusisha Slaaa na Ukristu?
Nilichokuambia ni hiki

Nikikumbuka posts zako za kwenye ile thread ya Zomba/na threads nyingine.
Post ya 183 page ya 10 kwenye uzi wa Zomba(Kashfa ya Chadema na Kanisa Katoliki)

Ulitaka Slaa aje kuthibitisha habari zinazotoka gazetini kuhusu chadema kujihusisha na Kanisa Katoliki, lakini hii barua ya Waislam ya kwenda kwa Katibu Mkuu wa CCM wala hutaki hata kuiamini. Hapo ndipo nilipokuona kwamba jicho lako limekaa kukosoa tu upande mmoja na ndiyo maana nikakuambia umevimbiwa na Udini.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/315041-kashfa-chadema-na-kanisa-katoliki-10.html
Tatizo lako mkuu wanug unasoma vitu na kuanza kuchukia pasipo kupima. Tofauti yako na mimi ni kuelewa maana ya maelezo na kuyapima maana kwa mwenye kuelewa atagundua kwamba nina uchungu zaidi na chama (CHADEMA) kiasi kwamba siyachukulii mabandiko kama haya kuwa ni upuuzi bali yanaweza kweli kukisambaratisha chama..

Ila ukirudi ktk barua ya hao Waislaam kwa katibu mkuu wa CCM, hawa ni kundi dogo la watu (walounda NGO yao)ambao kwanza wanajihusisha na siasa kama UAMSHO kule Zanzibar wanajiita wao ni Aswal Sunni - wanaodai kwamba wao ni wenye ushawishi mkubwa kwa waislaam Tanzania (uongo) hivyo kuitumia dini kisiasa tena wakiandika barua kwa Chama cha CCM, leo hii mnakuja kuwapa PONGEZI za ajabu kabisa kuwa hawa ndio watu wazuri sana kwa sababu tu wanapinga kuwepo kwa Mahakama ya kadhi.. Fikiria hilo kwanza. Je, wewe unaipongeza CCM kwa Udini wake (sera zake on ground) wanapotumia watu kama hawa au Upo na Chadema chama kinachopinga Udini nchini..

Hivyo utagundua ya kwamba kinachowakwaza nyie sio swala la siasa isipokuwa UDINI wenu na hivyo mtu yeyote anayeonekana kupingana na mahakama ya kadhi hata kama ni mtu mbaya kiasi gani KISIASA bado mnamuona wa maana sana. Nimekusomeni sana ktk maelezo ya Mohamed mtoi ambaye kwa kiwango kikubwa alipotoka lakini kwa sababu alionekana kuwashambulia waislaam, sifa kibao alipewa pasipo kupima maneno yake yanaweza leta madhara gani upande wa pili..

Huyu ndiye Mkandara mkuu wangu, hizi habari za kusema TUKO PAMOJA ilihali kila siku hamuishi kututukana humu zinanipa mashaka kama kweli tuko pamoja kuna Udini mbele ya kuwa pamoja.
 
Mkuu Mkandara,
Hoja kuhusu "Zitto kuchukiwa kuhusu Uislamu wake," napenda kuizungumzia kama ifuatavyo:
1. Imeonekana kama Zitto ni mwislamu pekee aliyepo CDM kwa vile kila anapokuwa critisized hukingiwa kifua cha udini! Kwa namna hiyo mtamwangamiza kisiasa badala ya kumsaidia kama kweli anataka kuwa Rais wa nchi! Hoja ya udini wake inafaa sana kama anataka kuwa kiongozi ndani ya chama kingine, km CUF, CCM, nk
2. Maneno na Matendo ya Zitto yanaonesha anatumiwa na CCM kwa ajili ya kuangamiza upinzani, hili liliwahi kusemwa hata na mama yake Zitto! Lisemwalo lipo, kama halipo liko njiani linakuja!
3. Zitto amebadilika sana tangu alipoteuliwa kwenye Tume ya Mikataba ya Madini, sio Zitto yule ambaye gari lake liliwahi kusukumwa alipofukuzwa Bungeni! Zitto wa sasa ni "Shibuda type" anayetaka kuwa Rais huku akijua umri wake hauruhusu! Ni mtu ambaye amekuwa mtetezi kiaina wa mafisadi:
(a) Hakutaja orodha ya walioficha fedha nje ya nchi. Zitto wa zamani hilo lisingempa tabu,
(b) Alitetea ununuzi wa mitambo chakavu ya Dowans huku akijua kuwa Sheria ya Manunuzi ya wakati huo hairuhusu. After all kampuni yenyewe ni ya kifisadi! Zitto wa zamani asingefanya upuuzi huo.
4. Zitto mpya atafanya fyongo kisha mkimsema atakimbilia mwavuli wa udini! Kama hajui Zitto anajiangamiza zaidi kisiasa kwa karata hii!
5. Zitto angejifunza kwa akina Abdallah Safari, Arfi na wengineo ambao hatujaona wakieneza "kuonewa" kwa sababu ya Uislamu wao, otherwise Ikulu ataiona tu akialikwa na Rais atakayekuwepo!
Mkuu wangu swala sio Zitto huyo ni kachumbari tu ya swala zima. Unaposoma hoja ya mtu ni vizuri uisome yote na utazame kwa nini mhusika ameandika hivyo.

Swala langu ni kwamba ikiwa nyie mnawachukia waislaam kiasi hiki mnawatenga kiasi hiki hizi habari za kuwa tuko pamoja zina maana gani?.. Hivyo nikiunganisha maneno yenu humu JF na jinsi mnavyomchukia Zitto nina hakika kabisa uoandika hapo juu ni uongo mwingine. Zitto hawezi kwenda CUF wala CCM yupo nanyi CDM na wengine mmemkuta, kwa nini mnashindwa kumkubali kama alivyo wakati huo huo mkiwatukana waislaam kuwa hawakusoma, hawana akili na kama wakitaka shule wajenge zao! nyie mmerithi zile za mkoloni ilihali mna waislaam ndani ya Chadema. Hii kujiweka tofauti na kuwa NYIE mna maanisha nini?

Sasa najiuliza tulioko Chadema tuna tofauti gani na hao mnaowatukana maana kila tusi lenu najiona kama mnanitukana miye halafu mnasema tuko pamoja..Fikiria hilo kwanza halafu nipeni jibu hii kitu TUKO PAMOJA huwa mna maana gani?
 
acheni unafiki bwana hakuna nn wala nn kadhi awe na kazi asiwe nayo lazima apatkane ni swala la waislam liachen na nyny wakristo mkitaka anzishen yenu kama zile za Roma haina shida hiyo ni barua ya kinafiki kutaka kuwagawa waislam wala ansar hawana kupinga kadhi na hakuna muislam wa kwel anayepinga kadhi bali ni wanafiki wanaotumiwa na makafiri kadhi haiwahusu nyinyi, mbona nyerere ametenga fungu kwa kanisa hizo pesa si za waislam na wakristo mbona mnapokea hamsemi za walipa Kodi nyie mbuzi kweli hata walipwe pesa waachen walipwe.....SMT inatoa pesa kwa makanisa mnaona raha Kadhi anawauma nyie nn bwana acheni ushamba
 
Napenda sana pale mtu anaponiita mnafiki wakati hana mfano zaidi ya kwamba nimpendeze yeye...na sidhani kama unaelewa maana ya Mnafiki isipokuwa unalitumia tu neno hili kama mnavyotumia Pepo....

Mkuu wangu simtishi mtu wala hakuna anayetishika hapa JF.. bali nawaambia ukweli usoupenda kuusikia. Mnafiki yeyote angesema uongo, akaahidi asitimize na hata akiaminiwa haaminiki, hivyo sijasema uongo bali ukweli unaojieleza wazi kabisa hapa hapa JF kutoka vivyanu mwenu. Itakuwaje nyie mseme hamna Udini lakini kila siku hamkosi kuandika mada zisizopungua mbili kuhusu Waislaam tena kwa ubaya na dharau - watu ambao mnadai ni ndugu zenu, majirani zenu (Uongo mkubwa) kuwasema hawakusoma, wajinga tena mnamtukana hadi mtume wao halafu mnataka sisi tuwaamini kwa lipi.

Nimesema mnamchukia Zitto kutokana na imani yake maana mnazo agenda zenu na sasa zinajitokeza wazi kabisa na narudia kusema itakula kwenu. Zitto ana matatizo yake lakini sii wa kumchukia kiasi hicho - hapana kuna siri nyuma yake maana huyu huyu Zitto akifanya vizuri bungeni, Oooh! Zitto wetu wa Chadema... akiharibu anaitwa kibaraka kwa nini asiwe kibaraka hata anapowakilisha hoja mnazopenda kuzisikia!..Hivyo wala usinishtukie miye bali jishukieni wewe mwenyewe maana tumeshawagundua janja yenu na haitafika mahala...Kila siku tuko pamoja - Pamoja wapi?..
Mzee natofautiana na wewe, Zito anapoungwa mkono huwa hajabadili imani yake, lakini bado anaungwa mkono! Kwasababu ya complement tu. atalaumiwa anapoonekana amekwenda astray! Swala la imani yake linaingiaje? Hapo ju umeandika akiwasilisha hoja wanayo ipenda wanasema "ooh Zito wetu", kumbuka anakuwa na imani yake ileile, ambayo unadai kuwa wanaichukia.
 
6. Waislamu (wanaharakati) dai lao la msingi ni MGAWANYO SAWA WA MADARAKA. Hivyo Serikali inapounda Wizara, wao hutizama Baraza la Mawaziri, WAISLAMU NI WANGAPI NA WAKRISTO NI WANGAPI NDIO MAANA WANAIUNGA MKONO CUF, KWA VILE CUF IMEELEWA TATIZO LAO NA WAO WAKAJA NA KAULIMBIU YA HAKI SAWA KWA WOTE, yaani kwa Wakristo na Waislamu, wala Ilani ya Uchaguzi ya CUF haisemi lolote kuhusu Mahakama ya Kadhi WALA HAITOSEMA!!

Sasa NImeelewa kwa nini CUF ni chama cha Dini. Fulani , si mnaona hapo juu
 
Miminafikiri kama kweli ungataka kusema kweli UNGEJIULIZA KWANINI mUHASISI WA CHADEMA MZEE EDWIN MTEI alipotoa comment zake kuhusu Tume ya taifa ya kukusanya maoni ya Katiba mpya huko Tanzania alinena TUME IMEJAA WAISLAMU WENGI.

Je unajuwa kwanini muasisi huyu alisema hivyo?

Mkuu wangu swala sio Zitto huyo ni kachumbari tu ya swala zima. Unaposoma hoja ya mtu ni vizuri uisome yote na utazame kwa nini mhusika ameandika hivyo. Swala langu ni kwamba ikiwa nyie mnawachukia waislaam kiasi hiki mnawatenga kiasi hiki hizi habari za kuwa tuko pamoja zina maana gani?.. Hivyo nikiunganisha maneno yenu humu JF na jinsi mnavyomchukia Zitto nina hakika kabisa uoandika hapo juu ni uongo mwingine. Zitto hawezi kwenda CUF wala CCM yupo nanyi CDM na wengine mmemkuta, kwa nini mnashindwa kumkubali kama alivyo wakati huo huo mkiwatukana waislaam kuwa hawakusoma, hawana akili na kama wakitaka shule wajenge zao! nyie mmerithi zile za mkoloni ilihali mna waislaam ndani ya Chadema. Hii kujiweka tofauti na kuwa NYIE mna maanisha nini? Sasa najiuliza tulioko Chadema tuna tofauti gani na hao mnaowatukana maana kila tusi lenu najiona kama mnanitukana miye halafu mnasema tuko pamoja..Fikiria hilo kwanza halafu nipeni jibu hii kitu TUKO PAMOJA huwa mna maana gani?
Mkuu Mkandara, Hoja zinapokuja kijumlajumla hujibiwa kijumlajumla vile vile! Kwa mfano Wakristo wanapoambiwa kuwa wanakula kitimoto ili hali baadhi yao hawali (eg Wasabato), Waislamu nao huambiwa hawajasoma na ni watu wa kulalamika tu! Ukweli nionavyo mimi sio Waislamu wote ambao hawajasoma! Wapo maprofesa waliobobea kama akina Issa Shivji, Safari, nk. Kwa hiyo kama pande zote mbili zingekuwa zinajadili mambo kwa kutumia isolated incidences tusingefika huko! Kwa hiyo ukileta hoja za jumla dhidi ya Dini nyingine utegemee majibu ya jumla! Pia umenishangaza sana unapokuwa na makengeza kiasi kwamba huoni matusi tunayoporomoshewa sisi Wakristo! Kwa hiyo Mkristo yeyote akisoma hoja zako zilizokuwa biased naye atatoa hoja zilizokuwa biased, mwisho wa siku utadai kuwa HATUKO PAMOJA! Wewe unachangia kwenye juhudi za kutaka TUSIWE PAMOJA kisha mwisho wa siku unadai tuko pamoja kivipi! Pamoja na hayo Wakristo wamekewa wanawa-criticise akina Mkapa, Lowassa, nk hapa JF, hatujaona wakikingiwa kifua kwa sababu ya Ukristo wao! Mtikila pamoja na wachungaji waliojihusisha na DECI wamefikishwa mahakamani, Wakristo wameacha Sheria ichukue mkondo wake. Kwa upande wa baadhi ya Waislamu hali ni tofauti! Kwanza waliochoma makanisa tuliambiwa kuwa ni "wahuni!" Kisha "wahuni" hao walikamatwa tuliona CUF ilivyofanya juhudi kubwa ya kuwatetea "wahuni!" Mpaka sasa hatuelewi kwa nini baadhi ya Waislamu hao wametuchomea Makanisa yetu moto na mbaya sana kutuibia vifaa vya Kanisa! Utani wa watoto ulichukuliwa kama ugomvi wa Wakristo na Waislamu! Suala la Muungano kule Zanzibar limechukuliwa kuwa ni la "kikanisa" zaidi! Hatujui baadaye litaibuka lipi! Kuhusu Zitto, akiona CDM hawamkubali dawa si kuibua hoja ya kidini, aende Chama ambacho anaona kinamfaa! It is strange kuwatuhumu watu hawakupendi ili wakupende! Just like Mwakyembe alipodai Serikali inataka kumuua huku akiendelea kuwa kwenye Serikali hiyo hiyo! Tena anapoweka hoja hizi dhaifu anazidi kujimaliza kisiasa zaidi! Wewe endelea tu kumchimbia shimo! Nawasilisha!
 
Last edited by a moderator:
Mzee natofautiana na wewe, Zito anapoungwa mkono huwa hajabadili imani yake, lakini bado anaungwa mkono! Kwasababu ya complement tu. atalaumiwa anapoonekana amekwenda astray! Swala la imani yake linaingiaje? Hapo ju umeandika akiwasilisha hoja wanayo ipenda wanasema "ooh Zito wetu", kumbuka anakuwa na imani yake ileile, ambayo unadai kuwa wanaichukia.

Mkuu hawa watu hujigeuza rangi kama kinyonga!
 
Waislam nawaonea huruma elimu hamna,baada ya kujifunza elimu ya dunia mna jifunza lugha za mashetan zitawasaidia nini
mtashindana na wakristo mtaweza?
 
Wakuu,

Nimeiona hii barua ya Waislamu kupinga Mahakama ya Kadhi, imenukuliwa toka katika Kitabu cha MAHAKAMA YA KADHI NI NINI? kilichoandikwa na C. Simbaulanga, 2012 (uk. 53 - 58) kwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba.

Nitanukuu baadhi ya mambo muhimu kuhusu barua hiyo ya Ustadhi A. S. Mkambaku, Katibu Mkuu wa Khidmat Dwaat Lisiamiyat Centre Registered Trustees. Haijaandikwa tarehe lakini ukisoma utaona iliandikwa kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010:

KHIDMAT DWAAT LISIAMIYAT CENTRE REGISTERED TRUSTEES
P. O. BOX 16106, MOB. 0713-290272, 0784-403020.

1. Uanzishaji wa Mahakama ya Kadhi utaleta madahara makubwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa vile Wakristo hawagawanyiki katika suala la kuipinga, lakini sisi Waislamu tunagawanyika katika suala hilo. Kwa taarifa yako napenda nikuhakikishie kuwa Waislamu wa Madhehebu ya AnsarSunna HAWAIKUBALI Mahakama hiyo kwa vile wanaelewa kuwa itakuwa chini ya BAKWATA.

2. Pia wanaelewa kuwa miongoni mwa mamlaka ya Kadhi ni kutangaza mwezi wa Ramadhani kufunga na kufungua na wao wanaye Amir wao ambaye hutangaza mwezi kwa kufuata mwezi unaoandama Saudia (Saud Arabia). Kwa maana hiyo katika nchi yenye Kadhi kutokea mtu mwingine nje ya Kadhi kutangaza mwezi ni kosa la jinai.

3. Kitu ambacho kitaleta madhara makubwa kuliko mafanikio ingawa AnsarSunna ni kundi dogo lakini wanaburuza kundi kubwa sana la Waislamu, kuliko Taasisi yoyote ya Kiislamu hapa Tanzania kwa vile ushawishi wao ni mkubwa sana katika jamii ya Kiislamu.

4. ANSAR SUNNA ndio wanaoendesha Shuura ya Maimam, GAZETI LA AN-NUUR, AL-HUDA, NASAHA na RADIO IMANI. Pia wana ushawishi mkubwa TIMES FM. Je, BAKWATA wana uwezo wa kupambana na vyombo hivyo?

5. Je, Serikali inaweza kukabidhi Mahakama ya Kadhi kwa wanaharakati wa Kiislamu? Nina hakika haiwezi kufanya jambo hilo na kama haitofanya hivyo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaweza kupata hasara zifuatazo:
(a) Wakristo wote wanaweza kujitoa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga katika chama cha CHADEMA ambacho hakina Mahakama ya Kadhi katika Ilani yake.
(b) Waislamu wote walioko chini ya Shuura ya Maimamu ambayo ni Mpinzani Mkuu wa BAKWATA wataendelea kuipinga Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuikumbatia BAKWATA na huku wakiendelea kuiunga mkono CUF, hivyo CCM itajikuta imebakia na Waislamu wanaoiunga mkono BAKWATA tu. Suala la wanaharakati kuipinga Mahakama ya Kadhi ni jambo rahisi sana kwa vile Mahakama ya Kadhi sio madai yao ya msingi.

6. Waislamu (wanaharakati) dai lao la msingi ni MGAWANYO SAWA WA MADARAKA. Hivyo Serikali inapounda Wizara, wao hutizama Baraza la Mawaziri, WAISLAMU NI WANGAPI NA WAKRISTO NI WANGAPI NDIO MAANA WANAIUNGA MKONO CUF, KWA VILE CUF IMEELEWA TATIZO LAO NA WAO WAKAJA NA KAULIMBIU YA HAKI SAWA KWA WOTE, yaani kwa Wakristo na Waislamu, wala Ilani ya Uchaguzi ya CUF haisemi lolote kuhusu Mahakama ya Kadhi WALA HAITOSEMA!!

7. Pia Waislamu wanaharakati wanaelewa kuwa Mahakama ya Kadhi haina manufaa yoyote kwa Waislamu, kwa vile Zanzibar ipo na WAISLAMU WA ZANZIBAR HAWANA MAENDELEO YOYOTE KUWAPITA WALE WA BARA, NA UISLAMU SI NDOA NA MIRATHI TU WALA MUNGU HASEMI "SOMETHING IS BETTER THAN NOTHING." Huu ni msemo wa Wazungu.

8. Mwenyezi Mungu anasema: INGIENI KATIKA UISLAMU WOTE NA MSIFE BALI MMEKUWA WAISLAMU KAMILI (Surat Baqarah ya 2 aya ya 208). Kwa hiyo mimi nikiwa kama Mwislamu nashauri kuwa Mahakama hiyo ISIWEPO kwani haitakuwa na manufaa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) na italeta mgawanyiko miongoni mwa wanachama wako, chukulia mfano Zanzibar, Mufti na Kadhi wanavyopingwa na wanauamsho ambao wanaongozwa na Sheikh Farid hali wanauamsho ndio Shura ya Maimam na Shuura ya Maimam ndiyo Uamsho.

KWANINI MASHEIKH WA BAKWATA WANAITAKA?
9. Wanaelewa wanachokifanya, wao wanajua fika kuwa Serikali itakapoanzisha Mahakama ya Kadhi watakuwa wamepata AJIRA, kwa hiyo wao wanapigania maslahi yao tu, hawawezi kuangalia madhara yatakayokikumba Chama Cha Mapinduzi (CCM) na huku wakijua kuwa ushawishi wao ni mdogo katika Jamii ya Kiislamu na hawana hata Miundumbinu ya kuwashawishi Waislamu wote waweze kumkubali Mufti, na hali ya Mufti ameshaweka wazi milango kwa Taasisi zote za Kiislamu na Waislamu waje washirikiane naye.

10. Masheikhe hawa wanaelewa kuwa hakuna Hakimu anayehukumu makosa mawili tu, yaani NDOA na MIRATHI, ukiletewa mzinifu huruhusiwi kumhukumu, ukiletewa mwizi huruhusiwi, nk. lakini wanang'ang'ania hivyo hivyo kwa ajili ya mishahara tu na hiyo ni hatari.

11. Hujaribu kutoa hata mifano ya Serikali ya Uingereza kwamba mwaka 1920 iliweka Mahakama hizo, ukweli ni kwamba Serikali ya Uingereza haikuweka Mahakama za Kadhi tu bali za Maakida na Maliwali, lakini pia sababu ya kuziweka Mahakama hizo siyo kwa ajili ya kuutunza Uislamu au uliwali bali ilikuwa ni mbinu ya kuwatuliza Viongozi hao ili waweze kuwatawala bila vurugu kwani mkoloni aligundua kuwa ni watu wenye ushawishi katika jamii kwa hiyo ile ilikuwa ni mbinu ya kiutawala ili Masheikhe, Maliwali na Maakida wajione kuwa na wao ni sehemu ya Serikali ya Muingereza, kumbe ni watawaliwa, hivyo bado hoja hiyo haina msingi wowote wala haina maana kwamba Serikali ya Mkoloni ilikuwa nzuri kwa Waislamu kuliko hii ya CCM, na huku tukiambiwa kuwa Waislamu ndiyo walioanzisha harakati za kudai Uhuru, kama walikuwa wazuri kwa nini tuliwaondoa.

12. CCM inayo mambo mengi ya kujivunia kwa Waislamu kama vile kuwapatia Chuo Kikuu, na hilo ni jambo muhimu na la msingi kwa maendeleo ya Uislamu na Waislamu, kwa hiyo JAMBO HILO LA MAHAKAMA YA KADHI mnapaswa kuliangalia kwa umakini ijapokuwa limo ndani ya Ilani yenu. Lakini si kila jambo lililomo ndani ya Ilani litekelezwe, mengine yanaweza kushindikana kwa matatizo mbalimbali na hili ni tatizo kubwa KWANI LINAWEZA KUZAA MGOGORO WA KIDINI!!

WAKRISTO WANA HAKI YA KUPINGA MAHAKAMA YA KADHI
13. Sehemu kama Zanzibar ni rahisi kuweka Mahakama ya Kadhi kwa vile Waislamu kule ni asilimia 99.99 hali kama hiyo Wakristo kule ni kama hawapo wamemezwa kwa uchache wao. Lakini BARA NI PAGUMU kwa vile HUENDA WAKRISTO NI WENGI KULIKO WAISLAMU. KWA VILE WAISLAMU KWA UHAKIKA HUPATIKANA MIKOA ISIYOZIDI SITA AMBAYO NI DAR ES SALAAM, LINDI, TANGA, MTWARA, KIGOMA NA TABORA, pia katika mikoa hiyo siyo Wilaya zote, kwa mfano Mkoa wa Kigoma ni Ujiji na Kigoma Mjini tu.

14. Pamoja na hayo Masheikhe wa BAKWATA wanaoshikilia suala la kuwepo kwa Mahakama ya Kadhi bado hawajafahamu nini tatizo la Wakristo, hata hawakubali kuwepo kwa Mahakama hiyo, siyo kweli kabisa kwamba Wakristo hudhani Mahakama hizo zitawahukumu wao, la hasha na Masheikhe hutumia muda mwingi kuwaelimisha juu ya hilo, wakati hilo sio tatizo lao, na ni udhaifu wa kutokujua madai au matatizo ya mpinzani wako, ni nini tatizo la Wakristo ni hili:
(a) Mkumbuke kwamba mwaka 1993 hapa Tanzania kulikuwa na mgogoro wa bucha za nguruwe, mgogoro huo ulizaa harakati kubwa za Waislamu ambazo makao yake makuu yalikuwa msikiti wa Mtoro na kiongozi mkuu alikuwa marehemu Kasim bin Juma. Waislamu walipinga kuwepo Ubalozi wa Vatican hapa Tanzania na bado wanaendelea na msimamo huo hadi leo, wakati ubalozi huo hauendeshwi kwa Fedha za walipa kodi wa Tanzania bali ni Vatican yenyewe. JE, ITAKUWAJE LEO WAKRISTO WAKUBALI ZIWEPO MAHAKAMA AMBAZO ZITATOA AJIRA KWA WAISLAMU, KUANZIA MTAA, KATA, TARAFA, WILAYA, MKOA HADI TAIFA, TENA KWA FEDHA ZA WALIPA KODI WA TANZANIA WAKIWAMO NA WAO WAKRISTO? Hilo ndilo tatizo lao na hapo ndipo BAKWATA wanatakiwa wapatolee maelezo.
(b) Kwamba, mabilioni ya Watanzania yatakayowalipa Masheikhe kila mwezi nao wao watanufaikaje? Huo ndio mgogoro uliotengenezwa na Ilani yenu na ambao unaweza kuwagharimu katika uchaguzi ujao wa mwaka 2010 ENDAPO WAKRISTO WAKIIGA MFANO WA WAISLAMU WA MSIKITI WA MTORO walipoamua kukusanya Kadi za CCM mwaka 1993 ingawa jaribio hilo lilizimwa na Viongozi wa CCM.

HOJA ZA SHEIKH BASALEH
15. Sheikh Ali Basaleh ndiye ambaye amelielewa tatizo la Maaskofu ingawa ametoa mfano mzuri wa kuwatuliza katika kipeperushi chake cha Wito cha tarehe18/08/2006. Ijumaa kuwa kama mtu ana watoto wawili mmoja anakula sana na mwingine hali sana, Je, baba atamzuia yule anayekula sana ili alingane na yule asiyekula sana? Mfano wake ni mzuri lakini haufanani na tatizo lililopo kwani fedha za baba hazichangiwi na watoto wake, bali baba huzitafuta yeye mwenyewe kwa nguvu zake, LAKINI FEDHA ZA BABA SERIKALI ZINATOKANA NA KODI YA WAISLAMU NA WAKRISTO, HIVYO SERIKALI HAIPASWI KUTUMIA FEDHA NYINGI KWA DINI MOJA LAZIMA ITALETA MGOGORO NA NDIYO MAANA SISI WAISLAMU TUMEKUWA TUKIDAI HAKI SAWA!

16. Katibu Mkuu ni matumaini yangu kuwa hekima itatumika katika kulitatua tatizo hilo kwani ni rahisi kuziba ufa kuliko gharama za kujenga ukuta mwisho nakutakia kazi njema pamoja na afya njema.

WABILAH TAUFIQ,
ASANTE.
USTADH A. S. MKAMBAKU,
KATIBU MKUU.
Mkuu nashukuru saana kwa taarifa hii ingawa nimeiona nikiwa nimechelewa lakini sina budi kukupongeza ili tujue kuwa kuna watu wahusika wenyewe wanapinga hii mahakama ya kadhi hapa Tanzania!!!!
 
Masuala ya dini ni ya mtu binafsi. Ni imani yake mwenyewe. Imani yake hiyo haina haja kwa mtu mwingine kujihusisha nayo, na wala Serikali (dola) haina sababu kujihusisha nayo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom