Baraza la vijana la CHADEMA(BAVICHA) na "Umbumbumbu" dhidi ya usawa wa kijinsia

njundelekajo

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
310
227
BARAZA LA VIJANA LA CHADEMA(BAVICHA) NA "UMBUMBUMBU" DHIDI YA USAWA WA KIJINSIA

Jumuiya ya kimataifa ina malengo 17 ya maendeleo endelevu(SDGs) ambayo yaliidhinishwa mwaka 2015 na yanatakiwa kutekelezwa kwa miaka 15 mpaka mwaka 2030, ikiwemo kuleta usawa wa kijinsia.

Lakini pia mojawapo kati ya malengo ya milenia kwa umoja wa mataifa kumaliza tatizo la umaskini ifikapo mwaka 2015,lengo lilikusudiwa moja kwa moja ni usawa wa kijinsia na haki za wanawake.Haitoshi mfuko wa idadi ya watu wa umoja wa mataifa(United nations population Funds) unaamini usawa wa kijinsia ni sehemu ya haki za binadamu.

Wakati dunia ikitambua hivyo na siasa kama chombo kinachoaminika kusimamia ushawishi na upatikanaji wa usawa wa kijinsia,baraza la vijana la chama cha Demokresia na Maendeleo (BAVICHA),linaonekana haliamini katika usawa wakijinsia kivitendo.

Baraza hilo la vijana la chama kikuu cha upinzani nchini lililoanzishwa kama mbadala wa kuregenzi ya vijana wa chama hilo si tu halina kiongozi wa kike katika safu ya juu lakini pia historia inaonesha limekua likijitahidi kufanya hila zote kusiwepo na sura ya mwanamke kwenye safu ya uongozi wake.

Historia inaonesha wakati wa uenyekiti wa John Heche (2011-2014)baraza hilo lilimfukuza makamu wake Julian Shonza kwa sababu za kuokoteza ambazo wachambuzi wa masuala ya siasa wanasa ni kasumba ya baraza hilo kutokua na sura ya mwanamke kwenye safu yake ya uongozi.

Shonza aliyezaliwa 23/4/1987, ambaye sasa ni naibu waziri wa habari,michezo na utamaduni alifukuzwa kwenye baraza hilo akifuatiwa na mwanamke mwingine aliyekua naibu katibu mkuu Getruda Ndibalema.

Ndibalema ambaye sasa ni mtangazaji wa kipinda marufu cha runinga inadaiwa aliondoka ndani ya baraza hilo tarehe 11/3/2018 baada ya kutolewa maneno ya kasha na katibu wa baraza hilo Julius Mwita.

Tofauti na umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi(UVCCM),BAVICHA haina sura ya kike kwenye uingozi wake ngazi ya taifa.Inajulikana kwa upande wa UVCCM mwenyekiti ni Kheri Denis James na makamu wake ni Bi Tabia Mwita,wakati Bavicha mwenyekiti ni Patrick Ole Sosopi aliyerithi nafasi ya Patrobasi Katambi aliyehamia chama cha mapinduzi mwishoni mwa mwaka 2017,na katibu wake ni Julius Mwita huku kukiwa hakuna makamu mwenyekiti.

Kasumba hii ya BAVICHA iliyofanya uchaguzi kwa mara ya kwanza mwaka 2009 dhidi ya wanawake ni urithi uliotoka kwa mwenyekiti wa kwanza wa baraza hilo John Heche.Heche ambaye aliyeiingoza BAVICHa 2011 hadi 2014 kwa kumshinda "kimazabe" aliyekua mpinzani wake kwenye nafasi ya uenyekiti wa BAVICHA uchaguzi wa 2011 baada ya kuhairishwa uchaguzi wa 2009 ,David Kafulila alihasisi kasumba hii mara baada ya kumfukuza makamu mwenyekiti wake Julian Shonza na Mtela Mwampamba.

Ni katika kasumba hii,watu wengi wanahoji sababu inayowafanya BAVICHA kusambaza mitandaoni pongezi za kipropaganda kwa Ester Bulaya kama mwanamke wa nguvu anayepaswa kua mfano wa wanawake wote kwa kusimamia hoja ya kikokotoo.

Yapo maswali yanaulizwa kama BAVICHA inataka kuhamasisha wanawake katika harakati,kwa nini safu yake ya uongozi taifa haina hata mwanamke mmoja?.Lisilojulikana ni kwamba wanawake ni kundi kubwa linaloundwa na wapiga kura waaminifu na ushindi wa chama cha mapinduzi (CCM). umejificha ndani ya makundi kama haya yanayopuuzwa na vyama vya upinzani.

Uongozi pekee ambao wanawake wanao ndani ya CHADEMA ni kwenye baraza la wanawake linaoongozwa na Halima Jamesa Mdee na mke wa wa diwani wa kata ya Sombetini mkoani Arusha Ally Bananga,bi Hawa Bananga mbunge wa viti maalumu.

Mwaka 2019, ni wakati wa Baraza la vijana la chadema (BAVICHA)kutambua uwepo wa wanawake kwenye nchi hii na kuwatambua kama ilivyo kwa chama cha mapinduzi kilichotambua uwepo wa kundi hilo tangu kabla ya uhuru nyakati za kina Bibi Titi Mohamed.

Noel Nguzo.R.
 
Back
Top Bottom