Baraza la Mawaziri Kutangazwa Leo...Tetesi za Wanaotajwa Sura Mpya...

KWA MWENDO HUU MWAKA KESHO TENA TUNAVUNJA BARAZA LA MAWAZIRI, Maana yangu ni kwamba ripoti ya mwaka kesho ya CAG itasheheni mambo yale yale kama ndo wale wale wanao ingia. Tutegemee mabadiliko ya majina na sio utendaji.
 
Kama hujui kucheza chess hujui tu. Kama huna kete na mfumo, huna tu.

Kubadilisha rangi za kete za chess kutoka nyeupe kwenda nyeusi kama huna strategy hakuwezi kukupa ushindi.

Kubadili mawaziri bila kubadili mkakati ni danganya toto.
 
Team ni ilele na kocha ni yuleyule,tusitegemee mabadiriko kwa kubadirisha wachezaji,wote wanamfumo mmoja hapa cha msingi ni kumng'oa kocha tu.
 
Nasikiliza Clouds sasa hivi kwamba Baraza La Mawaziri huenda likatajwa muda wowote leo hii na baadhi ya wanaotajwa.......... na Dalali Kafumu

Mikataba ya kupora madini ya nchi yetu ina sahihi yake! Cry, my beloved country Tanzania!!!
 
Kama hujui kucheza chess hujui tu. Kama huna kete na mfumo, huna tu.

Kubadilisha rangi za kete za chess kutoka nyeupe kwenda nyeusi kama huna strategy hakuwezi kukupa ushindi.

Kubadili mawaziri bila kubadili mkakati ni danganya toto.
Ni sawa na kubadili jezi wakati wa mapumziko ukiamini kua umefanya "sub"
 
Kwa kweli tumechoka kuletewa sura zilezile

Unapomuita tena David Mwakyusa, au Kigoda (ambao aliwatema) ina maana anakula matapishi yake mwenyewe? ...Anne Kilango nina mashaka na uwezo wake katika hadhi ya Uwaziri, sioni kama anaweza kumpa nafasi! Ni mtu ambaye hana "staha" hataweza uwaziri!..Jenista Mhagama?....no way
 
Ha ha ha haa, Mwigulu? Huyu anayeshindwa hata kujieleza hapa JF? Kama ndo hivyo bora baraza libaki hilohilo lililopo tu. Naona CCM ishaishiwa man power hivi sasa. Mtaji mzuri upo CHADEMA kuliko hata CCM kwenyewe. Sioni kipya katika orodha hiyo. Eti hadi Kilango, mnafiki huyo?

Mwigulu kamata wizara ya Fedha ili kuboresha uchumi wa nchi
 
KWA MWENDO HUU MWAKA KESHO TENA TUNAVUNJA BARAZA LA MAWAZIRI, Maana yangu ni kwamba ripoti ya mwaka kesho ya CAG itasheheni mambo yale yale kama ndo wale wale wanao ingia. Tutegemee mabadiliko ya majina na sio utendaji.

Uko sahihi mkuu hii ni kutokana na udhaifu wa kiongozi mkuu kuweka washikaji zake
 
Back
Top Bottom