Baraza la Iddi: Mahakama ya Kadhi ni suala la Waislamu wenyewe - Kikwete

Huitaji kujua yaliyomo ndani moyo wa mtu hadi uangalie matendo yake. Siku zote JK mlikuwa mnamuona rais legelege leo hii kwavile kawaumiza waislamu yaliyo moyoni mwao unasema ndio rahisi amekamilika kweli wajinga ndio waliwao. Let me see hii movie itaisha wapi kwani wakati wewe unafurahia ujue mwengine anaumia halafu unasema Tanzania kisiwa cha amani . St Augustine aliwahi kusema an unjust law or society is similar to no law or society of lawlessness wait and see.

Kwani waislam mlikuwa mnataka nini hasa? ebu kuweni wawazi kidogo labda mnaweza kusaidika kwa kipindi hiki! au mnataka kuwa na taifa lenu?

pale alikwa kwa waislam na yeye ni mwislam.angeonekana kukubaliana na mombi yao hakika leo ndio ingekuwa kifo chake ....kwa hiyo ilibidi awapinge na kuwageuka waslamu wote.na ndio maana wale wote waliokuwepo pale dodoma leo wengi wamechukizwa na hawakutegema majibu ya jk.........

Ni kukosa vipaumbele, tatizo waislamu hata wakirudishiwa shule wanazodai..... kama zipo watazigeuza zote madrasa....

nini maana ya madrasa? madrasa ni shule kwa kiarabu.madrasa za hapa bongo zime base kiimani zaidi lkn madrasa za iraq pakistan saudi india misri ni elimu zote za duniani na kiimani.

ilibidi awe kinyume nao lakini pia yule jamaa huwa haaminiki.nyuma ya pazia anaweza kuwatekeleza matakwa yao halafu mkashangaa....jk ni kinyonga eti................

iti is very clear sasa kila mtu atajua watu wa hapa JF na chadema ni watu waaina gani.

ndo maana nilisema na narudia kusema kuwa uongozi wa JK umechukiwa kwa sababu ya hii mahakama ya kadhi, kujiunga na OIC na muafaka wa zenji. Sio hizi sababu zinazotolewa.

kabla ya hapo hamna hata mmoja anayeweza kunithibitishia kinyume chake. ona leo mlivyofurahi. Sitaki kuwa bias, bias kwangu mwiko.

wrong!

Kwa sisi waislam tunaona ametugeuka kwa kutoa majibu tofauti na alivyo tuahidi msikitini kipindi cha uchaguzi!! Kweli wanasiasa vigeugeu kikwete kigeugeu!!!

Acha unafiki wako.
Msikiti upi jk alikuja kukuahidi mahakam ya kadhi?
Nyie ndio manaotaka kutugawa kwa masuala ya udini.
WATU WENGINE HOVYO KABISA.

Amejivua gamba juu ya mahakama ya kadhi

Mmh si kwamba alipofika hapo akakumbuka kilichomtokea mwenye jina la mahala pale; oohooh hivi nimesema nini vile? Tatizo anatatua tatizo hili ana create lingine lakini bora zimwi likujualo halikuli likakwisha!

Heri wapole na wanyenyekevu wa moyo maana hao watarithi nchi....Lakini anguko la mafisadi bado liko pale pale come rain come sunshine!

Kawambia ukweli hata mimi nimefurahishwa kidogo, ule mfano wa kuwa mwenzako kaomba kapewa we hujaomba unalalamika kwanini mwenzio kapewa ulimewauma sana. Pia alipaswa kuwambia wanaolalamika waseme ni taasisi ipi ambayo inapewa fungu naserikali then inawabagua wao niiipi? wakati kama shule zote vyuo vyote havibagui mtu kwa dini yake kwahiyo hayo mafungu waislam pia wanafaidi hayo mafungu hizo taasisi ni njia tu.
Lakini pia waislam waache kulalamika wajenge shule zao vyuo vikuu vyao sio kubakiwa na chuo ambacho walipewa na Mkapa inamana wasingekuwa na chuo mpaka leo hii wao nikulalama tuuuuuuuuuuuu. Haya malalalamiko hayana tija kwenu mjikite katika elimu kuwasomesha watoto wenu.

Nimefuatilia kwa karibu hotuba ya JK iliyorushwa LIVE na TBC katika baraza la Idd pale msikiti wa Gaddafi Dodoma. Nilikuwa natafuta tu channel yenye habari nzuri ila nilipofungua TBC nikamkuta Live na nikasema nisikilize angalau kwa DK 2 kwani siku nyingi nilikuwa sipotezi muda wangu kuangalia hotuba na mzee wa kaya.

Kwa mara ya kwanza tangu nianze kumsikia JK leo ameongea kwa ujasiri kama rais wa nchi kuwajibu sio waislam tu bali viongozi wengi wa dini including za Kikristo. JK ameonyesha tabia ambayo sijawahi iona tangu aingie madarakani kwa kuongea kwa ujasiri na msisitizo na serious huku akimwaangalia machoni Sheikh Mkuu kuhusu serikali kukataa kurudisha shule zilizokuwa za dini na suala la mahakama ya kadhi.

Issue hapa siyo mambo aliyoongea ila alivyoongea ameni bariki sana kwani nimejisikia nikilazimika kusikiliza hadi mwisho hotuba ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa na hadhi ya ki urais tofauti na hotuba zoote alizowahi kufanya.
Katiba hotuba hii JK hakuwa nacheka cheka kama ilivyo kawaida jambo ambalo limefanya niamini kwamba amepata mwana saikolojia wa kumpa shule ya essentials of public speech.

Issues hizi nzito ameongea kama rais bila kuzunguka, kutetereka wala kuuma maneno huku wakuu wa dini hiyo wakimwangalia kwa kutoonyesha kuridhika na wengine wakaanza kunongonezana.

Mzee wa Kaya usiishie hapo bali anza kwa usiriazi huo kupambana na mafisadi, majairo, kushughulikia umeme na masuala mengine yanayodidimiza taifa. Naamini kwa spidi hiyo hiyo mtazamo wetu kwako lazima utakuwa positive!!

@Mvumbuzi, mbali na body-language unaweza kutujuza nini hasa kaongea? Umeme, mafuta, sukari, UDA kasema nini kuhusu haya mambo?

Hasa Mwembechai; kwa sababu kwa kiasi kikubwa ameonesha kile ambacho serikali ya CCM haikutaka wananchi wakijue kuhusiana na uhusiano wake na masuala kadhaa ya Waislamu - na hapa nazungumza kwa ujumla tu. Nashukuru niliwahi kufanya naye mahojiano ya kina sana kuhusu kitabu chake hicho.

Lakini katika hili pia kuna suala la hekima. Sidhani - katika kufikiri kwangu - ilikuwa ni proper channel kuwateremshia Waislamu jambo hili siku ya Idi na kwa namna ya kisiasa jinsi ilivyotolewa.

Kwa mtazamo wangu katika hili Kikwete angatakiwa kupongezwa, na amelisema sehemu na nafasi husika. Uwaji huo ndio unaotakiwa kusemwa moja kwa moja kwa madhehebu ya kiislamu kwa vile ni ndoto na maombi yao ya siku nyingi sana. Ameisafisha serikali kwamba wakianzisha mahakama hiyo serikali haihusiki kuiendesha na sheria lazima zifuate sheria za nchi.
Thats true.

Kwa hili nampongeza sana Kikwete kwani pamoja na mapungufu mengine, katika hili amefanya vema tumpongeze. Ingawa kuna wenye kutoa tafsiri nyingi, lakini sisi wengine tunaichambua hoja na kuitathmini kama ilivyo na nafasi aliyoitoa kwa wahusika. Vinginevyo tuachane na ushabiki tunaopangalima mambo muhimu kitaifa.

ukweli ni kwamba pale dodoma kwa gadafi(msikitini) wengi walichukia na majibu ya jk........wamechukia sana walikuwa wanamwamgalia kwa jicho la ndege.na hawakupiga hata makofi.hahaha

SINA IMANI NA JK HATA KIDOGO, SIYAAMINI MANENO YAKE WALA MATENDO YAKE! Subirini mtaona

1. Dodoma Secondary
2. Kizunguzi Secondary
3. Kondoa Secondary
4. Kwamire Girls
5. Hijra Secondary
6. Takwa Secondary
7. Jabal Hila Secondary

Ni hizo 7 tu nchi nzima?..tafadhali, naomba utusaidie pia orodha ya shule za kikristo ambazo serikali ilizichukua nasikia na wenyewe wanataka warudishiwe shule zao.

Back
Top Bottom