Baraza Kuu la Uongozi la Taifa CUF, kwa kutumia uwezo wake limemfukuza uanachama Profesa Lipumba

Duh.... Siasa za nchi hii ni pasua kichwa kabisa!

Kuna wengine wanashangilia aliye mtusi JPM kukutetewa mahakamani na Lisu, lakini hapo hapo hawatwambii ishu ya UKUTA imeishia wapi!

Ni vigumu sana kuwaelewa wapinzani wa nchii!

Najiuliza sana hata Lowassa wa level za akina Jk anawezaje kukaa na wababaishaji kiasi hiki?
Kutetewa ni khaki ya kila Mtanzania labda kwàsababu ya ukipofu wako unaona ni ajabu.
 
CUF sasa imesalimika upande, jitahidi muweke mikakati ya kukisuka CHAMA na tayari kuongeza WABUNGE mnamo majaaliws 2020,maana tayari mtakuwa mmejenga kajiuaminifu fulani kwa hawa Wabara na waTanganyika kwa ujumla,

Na Mungu awasaidie mfike salama, yale ya kuwekwa wazi msisite wekeni wazi, kwani tunataraji kusikia mengi MACHAFU kutoka upande wa pili jumlisha na support ya...mmeshanielewa maana nyie ni waelewa wazuri.
 
Mai wee Namuona Lipumba kama kambale mkubwa aliyejitamba ndani ya maji na kuwanyanyasa SAMAKI wenzake.
Leo yuko nje ya maji ubabe umeyeyuka nakugeuka kuwa majuto na kutweta. Tusubiri tuone wakati utazungumza.
 
Haya ndiyo maneno ya mwisho ya mtu anayekaribia kifo; kwa taarifa yako kazi ya kwanza ya kumfukuza prof. Uchwara imekamilika sasa kakaeni naye lumumba mumpe plan B. Kama ni marehemu tayari keshazikwa kinachoangaliwa ni siku ya kuhitimisha watu wale ubwabwa na kutawanyika
Huyo ni profesa...................Seif akileta mchezo chama kitafutika na kubaki historia. akumbuke alivumiliwa baada ya kulambishwa umakamu wa urais zanzibar na CCM aliweka shughuli za ukatibu Mkuu CUF pembeni.
 
Kosa kubwa alilolifanya lipumba ni kujivua uenyekiti ktk wakati muhimu tena kwa mbwembwe zote mbele ya waandishi wa habari.
Angejitoa kimya kimya na angetaka kurudi kwa sasa,nadhani ndio angepata support kubwa toka kwa wanachama na hapo.mgawanyiko ungetokea.
Sio kwa style ile kiongozi,chukulia mfano wa ukimya wa Dr Slaa wakati ule ulivyowaweka wanachama wengi ktk sintofaham,akaja kujiharibia alipoenda serena hotel kulalamika alishindia mihogo na maharage ili kujenga chama
Kwa upande wangu naona Prof. Lipumba alikua sahihi sana kuliko Dr. slaa ukiwa katika ngazi kubwa za uongozi halafu wenzako wakafanya maamuzi bila ya kukubaliana lazima jambo kama lile litokee kwa sababu tu mmedharau kiongozi wenu, hata kama wewe ndio mwenyekiti, Busara kubwa aliyoifanya hakwenda kuponda UKAWA alijiweka pembeni na kubaki kama mwanachama wa kawaida, ili wale mliowapa heshima kubwa wawapitishe katika safari yenu, baada ya kuona mambo yameenda mrama na chama kinaelekea kusiko, ameamua kurudi nalo si kosa vilevile kwa mtazamo wangu. Ila propaganda za kuchafuana, mara kapewa hela katumika, ndio zilizoifikisha kafu hapa. MOTO HAUZIMWI KWA PETROL, na kwa waliodhani kwamba UNAWEZA FUKUZA MWENYEKT bila madhara kweny chama ANAJIDANGANYA SANA.
 
Hakika Lipumba Kawatukanisha Ma-profesa. Kuwa msomi na kushindwa kusimamia msimamo wako ni kitu kibaya sana, kusema kuwa aliombwa na wazee kutengua kujiuzulu kwake akusaidii tusimwone kama mtu asiye na msimamo.
Je anafikiri Dr.Silaa hakuna wazee walio mfuata na kumshauri ageuze msimamo wake?
My take:
Ni bora kuwa na msimamo mbaya kuliko kutokuwa na msimamo kabisa.
 
Back
Top Bottom