Matanzia kizebazeba
JF-Expert Member
- Feb 12, 2013
- 654
- 630
Ndugu zangu kama sio unafiki ni madharau yaleyale yanaendelezwa mbele ya macho ya watanzania tukiwa tunaona.
Nilianza kuwa na imani na Rais kwamba kwa kuwa ameanza kuonyesha mfano mzuri kwa utendaji kwa mwezi huu mmoja basi atatuletea watu wenye mwenendo mzuri na background yao ni safi.
Kitendo cha kutuletea Mwigulu aliyekuwa naibu waziri wa Fedha ili awe waziri kamili huku akiwa na makashfa kibao ya wizara yao kushindwa kukusanya kodi ni madharau.
Mwakyembe aliyeweka wezi waliofukuzwa siku chache zilizopita kule bandarini na kila siku tunasoma kwenye magazeti jinsi alivyotuletea mabehewa feki leo anarudishwa eti ni msafi anaweza kazi, hayo ni madharau kwa watanzania.
Huyu Makamba naye hana sifa yoyote ya kuwa Waziri ndani ya nchi yetu kwa uwezo wake mdogo na kashfa kibao za majungu na kupepeta maneno hatutaki mtu kama huyu.
Huyu Muhongo aliyerudishwa Nishati si ndiye yuleyule aliyefukuzwa serikali iliyopita kwa kushindwa kazi? Leo hii anarudishwa tena mkifikiri tumesahau hasara aliyotuingizia?
Nilianza kuwa na imani kwa mbaali na huyu Rais japo yupo CCM nilianza kidogo kumuamini lakini sio kuamini chama chake.
Nilikuwa nasubiri nione ni watu gani ataleta ili wawe wasaidizi wake sasa basi kama ndio hao imani yangu imekufa moja kwa moja na huniambii tena kitu mara hii, tusubiri tuone.
Watanzania wenye uwezo na wasomi mbona wapo wengi, mpaka Nape unampa Uwaziri? Kweli upo serious au unatutania?
Sitaki tena kumuamini huyu Rais.
Usimwamini ila ndo Rais wako toa kelele na mihemuko isiyikua na maaana,
Ulio wataja unazifahamu vyema taaluma zao na cv zao ama unaleta kelele tuuuu??? January anapiga kaz kuwashndah kwenye mdomo mkaona ni mtu mbaya hujui mtanga yule?? Aya mwigulu kashndwa vp kukusanya kodi wakati kipindi wanaingi kodi ilikua kias gan inayokusanywa na kias gan wameacha inakisanywa?? Mnaongea bila statistics shdah yenu punguzen mihemuko msiish bila kusoma bhna