Baraza jipya la Mawaziri kujulikana Feb 12

Jamani mi kwa hivi sasa nipo dodoma, maeneo ya kilimani kwenye pub ya kilimani, kuna waheshimiwa wabunge wengi sana wanaangalia television hapa, na mimi nipo jirani na fanta yangu. Nimejaribu kunukuu mawili matatu waliyokuwa wanaongea .

Wanasema kuwa haijawahi kutokea katika historia ya tz rais akawaita watule wake na kuanza kupanga nao mikakati ya nini kifanyike katika utawala wake , na kamwe haitakuja kutokea. kwani inambidi awateua kwanza kisha awape mikakati yake.

nikatoka hapo nikaingia kwenye baa maarufu mjini kapa ya chako ni chako iliyo jirani kabisa na uwanja wa ndege wa dodoma nikakuta waheshimiwa fulani wakidiscuss ishu hii, walikuwa wanasema kuwa kuna tetesi kuwa jk badala ya kuwasiliana na aliowateua anawasiliana na wale wote aliowamwaga katika awamu iliyopita.na tetesi hizi nimesikia kwa watu wengi wa mjini hapa kuwa anachofanya hivi sasa ni kuwasiliana na wale wote aliowamwaga.

Na hivi sasa ndio naelekea dodoma hotel mana hapa ndo nchi ilipo hivi sasa na mabreaking news yote ya nani yumo nani hayumo yapo hapa ,any way sijui kama wataniruhusu niingie mana wah hawataki kuonana na waandishi wa habari so wanaweza wakajua mimi ni mwandishi wa habari kumbe nipo kwenye vacation.
Anyway yatakayojiri nitawataarifu
 
nimepishana na msafara wa RO na yeye akiwa kwenye range yake maeneo ya railway ,nahisi alikuwa anatikea kwa waziri mkuu maana tumepishana hapa railway na pm anaishi kwa nyuma tu ya railway.
kuna kila dalili ya cabinet kuwa kweli saa 9.ndo niko kwenye parking ya railway natafakari niingiaje dodoma hotel.
 
Habari zilizonifikia Punde,Basil Mramba kapata Presha na yuko Hospitali
 
nimepishana na msafara wa RO na yeye akiwa kwenye range yake maeneo ya railway ,nahisi alikuwa anatikea kwa waziri mkuu maana tumepishana hapa railway na pm anaishi kwa nyuma tu ya railway.
kuna kila dalili ya cabinet kuwa kweli saa 9.ndo niko kwenye parking ya railway natafakari niingiaje dodoma hotel.
Rostam naye vp?au ndio yale Jk anampa Uwaziri?
 
nuliza ni kwa nini waliohusishwa na kashfa ya Richmond warudi tema kwenye nyazifa hata kama wamehamishwa je huko hakuna mianya ya rushwa angalieni haya mambo.
 
huyu rostam sidhani kama hatakuwepo.naona gari(landcruiser nyeupe ) ya mwakyembe imepaki hapa dodoma hotel nashangaa.mana yeye amefikia nam hotel maeneo ya area d. na tunamtakia sana pole labda hiyo saa tisa anaweza akapona
 
Source: Habari kwa ufupi RTD
Kwa mujibu wa RTD,taarifa toka ofisi ya rais, baraza litatangazwa katika ikulu ndogo dodoma saa tisa mchana huu. Kwasasa rais anashauriana na viongozi wakuu wa kitaifa. Mlio Dodoma,Gembe na wengineo,twasubiri taarifa
 
Acheni hizo, hakuna sababu ya kupaparikia haya majina. Hakuna hata jina moja litakalowa-surprise. Ni wana CCM haohao ambao tunawajua. Kwa hiyo tujadili mambo mengine ya maana badala ya kukaa tunasubiri majina kama vile nasi tumekuwa magazeti ya jioni yanayosubiri kuuza. Majina yatatoka, tutayajua na kukaa nayo for the next three years, so why this papara? Tusiwe cheap sana!
 
yani bongo tumeendelea, maana waandishi wa habari are online while there are mobile. hebu mkuu mwana siasa niambie kuwa are you using a Laptop ama simu kuwasiliana na sisi. you guys are doing a great job out there.
 
Admin na timu yako ya udadavuzi mumetuangusha wanachama wenu ktk mtego huu wa JK.

muda uliopo utumike vema kutupasha ukweli.

Ahsanteni
 
Source: Habari kwa ufupi RTD
Kwa mujibu wa RTD,taarifa toka ofisi ya rais, baraza litatangazwa katika ikulu ndogo dodoma saa tisa mchana huu. Kwasasa rais anashauriana na viongozi wakuu wa kitaifa. Mlio Dodoma,Gembe na wengineo,twasubiri taarifa
Kwa sasa niko dar,ila nitaelekea Dodoma,muda Mfupi baada ya Rais Kutangaza Baraza la Mawaziri kujua nini kitajiri katika Makatibu wakuu wa wizara,Mwansiasa yuko dodoma naamini atatupa Feedaback.

kwa source zangu,inaonekana kuna usiri mkubwa katika baraza la jipya la Mawaziri,na limechangiwa na kuanguka kwa Lowassa.

WAtu wote ambao wanatakiwa kuwa Mawaziri wapo na simu zao hazijazimwa,Nimeweza kuwasiliana na Mawaziri na manaibu waziri waliopita na wenyewe wanajidahi hawajui kama watabaki ila wanasema wanauhakika kuwamo.

kuna habari za jana jk kutea watu ambao si wabunge kuwa Mawaziri,ila habari hizi zilimshtua Jk na nasikia akaamua kubadili na atawapa madaraka Mengine ikiwamo Ukatibu Mkuu katika Wizara.
 
Mimi nina amani zangu wala sina wasiwasi...

  • Baraza litarudi lile!
  • Mabadiliko haya hayazidi mawaziri kumi
  • sasa sijui mnaparanganyikiwa kwa sababu gani?

Kwa maoni yangu haya yanawezekana kutokea... wala sijasikia kutoka Dodoma...

1. Naibu waziri wa Usalama wa Raia, Africa Mashariki... wanaweza pandishwa cheo.
2. Tyson, Nagu au Mwangunga anaweza hamishiwa Tamisemi
3. Rais anaweza kuacha kujaza wizara moja, kwa ajili ya watu kama Prof. Wangwe kupewa au Mboja kupewa Ubunge na Kupewa Wizara ya Mipango.
 
Enyi watu wangu watanzania mbona mnaangamia kwa kukosa maarifa, je ni nani aliewaloga? Ni nani aliewaambia ya kwamba baraza`la mawaziri litaleta mabadiliko!
 
nimepishana na msafara wa RO na yeye akiwa kwenye range yake maeneo ya railway ,nahisi alikuwa anatikea kwa waziri mkuu maana tumepishana hapa railway na pm anaishi kwa nyuma tu ya railway.
kuna kila dalili ya cabinet kuwa kweli saa 9.ndo niko kwenye parking ya railway natafakari niingiaje dodoma hotel.

Hongera sana mwanasiasa kweli uko kazini sasa ni hivi hapo linapotangaziwa baraza si unapajua,hapo ndo penye kila kitu nenda unaweza kuleta nyepesi zenye uzito-tena hongera sana
 
Sitegemei kitu kipya cha kutia matumaini katika hao mawaziri wapya. Hata wakichimbwa mkwara kwa kutumia katapila hakuna cha maana watakachokifanya kama wale walio fanya madudu hawajachukuliwa hatua za kisheria.

Ilibidi mafisadi yachukuliwe hatua za nguvu kama vile kufungwa, kuporwa mali zao, na kuzuiwa kugombea/kuchaguliwa uongozi maishani mwao then ndiyo atuletee mawaziri wengine. Na hawa wapya wakiona kwamba wenzao waliopita walifanywa nini baada ya kupatikana na maskendo ndipo watakapokuwa makini na kuheshimu kazi zao, lakini kwa hali ilivyo nao watavuta chao wakijua kwamba wataachishwa tu uwaziri na maisha yao yataendelea kama kawaida. Sasa hivi kila mtu anaongelea kuhusu Lowasa, lakini yeye mwenyewe Lowasa hana pressure kwani mshiko aliovuta katika dili la richmond ni mamilioni ya dola na anakula kilaiini kama kumsukuma mlevi, lakini huyu tungemkamata na kumrundika ndani, tufunge maakanti yake na turudishe mapesa yetu yote aliyochukua angepata feelings fulani za maumivu.
 
Enyi watu wangu watanzania mbona mnaangamia kwa kukosa maarifa, je ni nani aliewaloga? Ni nani aliewaambia ya kwamba baraza`la mawaziri litaleta mabadiliko!

Chizzo mbona unakuwa kama umekuja leo duniani hujui kwamba kiongozi anayo nafasi kubwa sana ya kuleta mabadiliko kwa wale anaowangoza-umesahau kwamba nchi nyingi(Duniani) zilipata uhuru kutokana na umahili na uongozi mzuri wa viongozi wa wakati ule,hebu usitupotoshe tunataka viongozi wenye nia ya kuleta maendeleo nasio mapendeleo.
Tena nikwambie kipofu akimwongoza kipofu mwenzake wote watatumbukia shimoni upo hapo. (ina maana hilo hulijui)JK fanya mambo viongozi wazembe toa nje wote.
 
Acheni hizo, hakuna sababu ya kupaparikia haya majina. Hakuna hata jina moja litakalowa-surprise. Ni wana CCM haohao ambao tunawajua. Kwa hiyo tujadili mambo mengine ya maana badala ya kukaa tunasubiri majina kama vile nasi tumekuwa magazeti ya jioni yanayosubiri kuuza. Majina yatatoka, tutayajua na kukaa nayo for the next three years, so why this papara? Tusiwe cheap sana!

Hii mkuu sikubaliani na wewe kabisa, Taifa lililohai, lenye kujali mustakbali wake lazima liwe curious kujua ni nini kinaendelea katika mchakato mzima wa uongozi. Hii ni siasa na manjonjo yake!, tunajuwa ndio kwamba tutawajua hao, lakini kila kitu na majira yake, wakati wa krismass habari za wapi miti ya krisimasi inapatikana inakuwa ni habari kubwa kwa wauzaji na pia kwa kutangaza baraza jipya, ni habari kubwa pia kwa wapenda siasa. kwa hiyo tuwaacheni wananchi wawe Curious!
 
Back
Top Bottom