DOKEZO Barabara ya Mihama (Kata ya Kitangiri, Wilaya ya Ilemela) lini itawekwa Lami?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Hii Barabara ina Kibao cha ujenzi wa Lami tangu enzi za JPM. Lakini mpaka sasa haieleweki lini litafanyika zoezi hilo. Barabara inaendelea kuharibika kila kukicha kutokana na mvua za kila siku.

Barabara hii ndio inatumika na wafanya biashara wa Dagaa mjini Mwanza wanapoenda kurangua Dagaa kwa ajili ya Biashara kwani Mwalo wa Dagaa upo huko Mihama.

Kuna Shule ya Mihama Sekondari na Mihama Primary, kuna zahanati ya Mihama, ambazo zinafanya Jamii ya wakazi wa Mihama kuwa Kubwa lakini wakiwa hawana barabara kwa ajili ya Shughuli zao za kila siku.

Shule ya Mihama Primary, imezungukwa na Majaluba na vichochoro ambavyo si salama kwa watoto kwenda Shule hasa kipindi hiki cha mvua.

Mbunge wa Ilemela yupo kimya, Diwani wa Kata ya Kitangiri yupo kimya, na kuna Tetesi kuwa hawaelewani ndio maana Barabara hii ya Mihama inabaki ikiwa haina watetezi.

Jamii Forums mtusaidie kulifikisha hili lipate ufumbuzi.
 
Back
Top Bottom