barabara ya ikulu iliyofungwa ni mradi wa polisi?

mdawa

Senior Member
Oct 29, 2010
104
37
Ndugu zangu hii barabara ya nyuma ya ikulu ambayo hufungwa saa 12 jioni hadi saa 12 alfajiri inatumika na walinzi kama mradi wa kuwatoa pesa. Kwa mgeni si rahisi kujua njia imefungwa na hawa jamaa wakikushika badala ya kukurudisha wanakutisha ili wafanikiwe kukutoa pesa za kutosha. Kama viongozi wa wangekuwa waungwana wangeweka kizuizi ikifika jioni kinafungwa badala ya kuendelea na hii fedheha inayoendelea karibu na makazi ya rais wa nchi yetu. Naomba maoni yenu jamani.
 
Wangefunga barabara zote zinazoizunguka Ikulu ningeelewa. Hivi kuna mtu anajuwa sababu za kufungwa ile barabara na zingine kuachwa?
 
Jamaa wanalipwa mshahara laki moja na ushee na maisha magumu Dar wameamua kujiongezea kipato kimtindo.
 
Polisi ni Mradi wa Ikulu ya Serikali ya CCM. Hiyo barabara ni mradi wa Ikulu
 
Au waweke tangazo kubwa kujulisha umma mwisho wa matumizi ya barabara hiyo

Tunaendesha magari kulingana na alama za barabarani. Alama ipo na dereva yeyote kutoka popote duniani akiiona atajua kuwa panakatazwa na hataenda. Akileta kiburi basi atkayompata huko kayatafuta mwenyewe.

BInafsi nimeshakumbwa na suluba za kuendesha gari kimazoea. Pale Dodoma ukitoka Dodoma hotela kuelekea Uzunguni, mita kama 20 kuna kona ya kuelekea UDOM. Na ni hapohapo kuna ofisi ya Waziri mkuu nadhani. Miaka ya nyuma nilizoea kuwa napiga kona kushoto na kuelekea Chimwaga kabla hata UDOM haijafikiriwa kuwepo. Wiki juzi nikaenda Dodoma na nikaingia kichwa kichwa bila kuangalia kibao chenye alama. Sikufika mbali askari wakanisimamisha. Nikawabishia kwa nini wananizuia basi wao wenyewe wakanipeleka kwenye kibao. Hakika sikuwa na ubishi tena na nikatoa faini yao.

Ukifikwa na hali kama hiyo huna haja tena ya mjadala. Kwa sababu kosa kama lile tumezoea kupigwa faini lakini usisahau kuwa ukileta ubishi unaweza hata kusondekwa rumande au hata kifungo kisochopungua mwezi mmoja.

Hivyo, tusitafute sympathy kwa makosa yetu kuhusu sheria tunazovunja eti kwa sababu wengi tunazivunja. Tuvne tunachokipada.
 
Kuna sababu gani Kikwete kuifunga njia hiyo? Mbona marais wote waliiacha wazi? Anaogopa nini? Au mwenzetu ndio wale wanaoambiwaga kaoge barabarani saa tisa usiku?
 
Back
Top Bottom