Barabara ya Chalinze - Segera yafungwa

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,650
Wananchi wa Lugoba wamefunga njia kuu ya dar arusha eneo la lugoba baada ya mwenzao mmoja kugongwa na gari. Wasafiri wanaosafiri kati ya mikoa ya arusha, tanga na dar wamekwama kwa muda wa saa moja hadi sasa kufuatia wakazi wa eneo hilo kuweka magogo barabarani na kusababisha magari kushindwa kupita.

Wameahidi kutoondoa vizuizi hivyo hadi hapo atakapokuja kamanda wa polisi mkoa wa pwani kuwahakikishia ni lini ataweka matuta kuondoa uwezekano wa vifo kuendelea kutokea eneo hilo. Tukio hili limesababisha foleni kubwa sana ya magari na kama hatua za kuleta suluhu hazitachukuliwa kuna uwezekano foleni ikafika chalinze. Naona wakwere wameamua!

Tanzania bado inaendelea kukua, ikikomaa mengi ya haya mambo yatapungua au kukoma kabisa kutokea!
 
wananchi wamefunga njia wakidai matuta baada ya gar kugonga mtu, kuna folen ya kufa mtu
 
Na kuna baadhi ya maeneo ya barabara tayari matuta yameanza kuondolewa nafikiri ni kutokana na maagizo ya Magufuli kuwa kwenye highway hakuna sheria inayosema kuwepo na matuta.
 
kijiji gani,mkuu? Mbona asilimia 80 ya road ina matuta? Wale tunaoenda kuhiji moshi sijui itakuwaje
 
ni kweli hakuna sheria ya matuta highway. wananchi wanatakiwa waeleweshwe kuwa na taadhari wanapovuka au kupita pembeni mwa highways thats all
 
duh! Poleni.Maeneo hayo jirani na kwao mkuu wa kaya.Hapo foleni wami,upande mwingine chalinze.
 
Hapo Usa river mwezi ulopita tu, Wanachuo wa Tumaini nao walifanya hivyo hivyo mwenzao kagongwa wakaja kufunga njia eti wanataka matuta, FFU ikapitisha kichapo wakatakimbia njia ikafunguliwa na hadi leo hakuna tuta pale
 
Msata - kiwangwa(lami), kiwangwa - bagamoyo(vumbi) road boamba unawahi safi dar
 
Watz bwana hiyo ndio njia rahisi kukabiri tatizo??? hata kama kosa ni la huyo aliyegongwa???waishio karibu na hizi barabara ni wajibu wao kujua sheria za usalama barabarani.Nina imani kwenye hiyo foleni kuna wagonjwa wanaletwa dar kwa matibabu zaidi wanaumia tu hapo lugoda.
 
ni kweli hakuna sheria ya matuta highway. wananchi wanatakiwa waeleweshwe kuwa na taadhari wanapovuka au kupita pembeni mwa highways thats all
Kwani sheria zinadondoka toka mbinguni ili tusema sheria kama hii bado haijadondoka? Siku zote sheria hutungwa kulingana na mahitaji ya wakati na mahali. Hakuna dhambi kuweka matuta kwenye sehemu ambazo watu huvuka kwa wingi kwa miguu ili kuzuia ajali. Tuacheni ubifsi kwa kuwa tuna magari na hatuishi kwenye hayo maeneo basi tujifanye hatuoni umuhimu wa kuokoa maisha. By the way..... highway unazijua au unazisikia?
 
Acha kudanganya watu wewe, matuta yamewekwa kuanzia Kilala mpaka karibu na Leganga. Kiujumla sasa hivi wanafunzi wapo salama kwa asilimia kubwa kiasi kwamba hata aki gongwa mtu possibility ya kufa ni ndogo. Watu wengine bana masaburi at work.
 
ni kweli hakuna sheria ya matuta highway. wananchi wanatakiwa waeleweshwe kuwa na taadhari wanapovuka au kupita pembeni mwa highways thats all
Highway ndio nini? Je ulimaanisha expressway au freeway? Kama ni hivyo Tanzania hatuna freeways.

Freeway = mwendo mkali
Highway= barabara yoyote inayofuata viwango.
Sasa hio highway inapita kwenye vijiji haiwezi kuwa freeway. Lazima mwendo upunguzwe, na matuta ni aina mojawapo ya vipunguza mwendo, vinginevyo weka mapolisi kuhakikisha madereva hawazidishi mwendo kuhatarisha maisha ya watembea kwa miguu.
Kama serikali inataka kuzifanya freeways, basi inabidi itenganishe magari na watembea kwa miguu.
 
Unajua wakati mwingine wananchi huwa tunachemka, kwani huyo aliyegongwa hakuliona gari??? au gari liliacha njia likamfuata pembeni? watu hawako makini wanapotembea barabarani, kuweka matuta High ways ni ujinga na yanawachelewesha wasafiri.
watu wawe makini mabarabarani
 
Highway ndio nini? Je ulimaanisha expressway au freeway? Kama ni hivyo Tanzania hatuna freeways.

Freeway = mwendo mkali
Highway= barabara yoyote inayofuata viwango.
Sasa hio highway inapita kwenye vijiji haiwezi kuwa freeway. Lazima mwendo upunguzwe, na matuta ni aina mojawapo ya vipunguza mwendo, vinginevyo weka mapolisi kuhakikisha madereva hawazidishi mwendo kuhatarisha maisha ya watembea kwa miguu.
Kama serikali inataka kuzifanya freeways, basi inabidi itenganishe magari na watembea kwa miguu.
Watz kwa kawaida hatuko makini, inatakiwa sasa tujirekebishe,njia zetu zina vijiji kibao sasa ukisema waweke matuta si njia nzima itakuwa matuta???????????????????????
 
Hapo Usa river mwezi ulopita tu, Wanachuo wa Tumaini nao walifanya hivyo hivyo mwenzao kagongwa wakaja kufunga njia eti wanataka matuta, FFU ikapitisha kichapo wakatakimbia njia ikafunguliwa na hadi leo hakuna tuta pale

Arusha mara ya mwisho umeenda lini?
 
wananchi wamefunga njia wakidai matuta baada ya gar kugonga mtu, kuna folen ya kufa mtu

Hapo ndipo kwenye utata wa usimamiaji wa sheria zetu. Ukiangalia kati ya barabara na wananchi utagundua kuwa barabara ilianza na wananchi wakafuata kwani sheria inasema wazi kuwa barabara kuu ni lazima ipishe makazi ya watu kwa ajili ya usalama, sasa watu wanajenga kandokando ya barabara kuu wanaangaliwa tu haya ndiyo matatizo.

Katika nchi za watu wanaojali maisha ya wananchi wao wamejenga barabara zao kuu na kuziwekea uzio wa kuzuia watu na wanyama kuvuka toka upande mmoja kwenda mwingine isipokuwa tu katika sehemu maalum ambazo wamewekewa madaraja ya kuvukia kwa juu ama kwa chini ya barabara. Sisi lile daraja la manzese tu tumeshindwa kulipromote na matokeo yake kuwa kijiwe cha vibaka na wavuta bangi.

Ila tusiwalaumu hawa wananchi, maana kila wakati mtu anapovunja sheria tena na tena na tena bila kuchukuliwa hatua huona kuwa ununjaji huo wa sheria ni haki yake.
 
Watz kwa kawaida hatuko makini, inatakiwa sasa tujirekebishe,njia zetu zina vijiji kibao sasa ukisema waweke matuta si njia nzima itakuwa matuta???????????????????????
Barabara zinatumika na watu wa aina mbalimbali vichaa, watoto, walevi nk... Sehemu wanakovuka watu kwa wingi kuna vibao vya kuelekeza madereva waendeshe kwa speed ndogo lakini hawafuati....Matuta ni lazima
 
Watz bwana hiyo ndio njia rahisi kukabiri tatizo??? hata kama kosa ni la huyo aliyegongwa???waishio karibu na hizi barabara ni wajibu wao kujua sheria za usalama barabarani.Nina imani kwenye hiyo foleni kuna wagonjwa wanaletwa dar kwa matibabu zaidi wanaumia tu hapo lugoda.
Ndio maana tunadharauliwa na wenzetu wa nchi za EAC na kungwineko, uwezo wa watanzania kufikiri ni hafifu sana. kwanza barabara ni nyembamba, single lane eti ndo inaitwa highway bora zingekuwa dual carriage. halafu highway inapopita maeneo ya watu lazima iwekewe fensi pande zote ili kuzuia watu na wananyama kukatisha ovyoovyo. barabara hazina road sign, zikiwekwa inakuwa ni halali ya raia wema kutengenezea majiko ya mkaa. Raia mbumbu vijijini hawajui namna ya kukatisha barabara wala hakuna anaye jali kuwafundisha. Magamba wao wanakazi moja tu kulala maskini na kuamka billionea.
Hii nchi imelaanika hakuna matumaini hata kidogo labda turudishe ubalozi wa Israel labda tutapata msamaha.
 
Back
Top Bottom