Barabara kutoka Kongwa mpaka Mpwapwa kujengwa kwa miaka tisa

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,583
11,659
Huenda nitawakera na kuwaudhi wengi,ila sina namna;nitasema ukweli tu,ili wengi wapate kupona. Taifa liko katika mhemko mkubwa. Mhemko uleule wa miaka yote lakini yote yanatokana na kumezwa na ukungu wa hofu na matumaini. Nimekuwa mfutiliaji mkubwa sana katika ujenzi wa barabara ya Kongwa mpaka Mpwapwa; Mpwapwa na Kongwa ni wilaya mbili zinazobatikana mkoa wa Dodoma. Kutoka Kongwa mpaka Mpwapwa mjini ni kilomita 45.

Lakini swali la msingi linakuja kweli kilomita 45 za barabara zinajekwa kwa miaka tisa,yani nikiwa na maana ujenzi wa barabara kutoka Kongwa mpaka Mpwapwa, taarifa zinasema kila awamu wanajenga kilomita 5 yani kwa kilomita 45 ni miaka tisa mbele ndio barabara inamalizika.

Upo msemo wa kiswahili unaoeleza kuwa ni vigumu sana kumfunza mbwa mzee mbinu mpya za kukamata adui.

index2.png

index.jpg
 
Matatizo yanaanzia na sisi wenyewe, maana serikali ni watu na watu ndio sisi. Kama sisi h hatuna uwezo/Mali sasa serikali itaanzaje kuwa pia na uwezo mkubwa wa kugharamia?
 
Hivi yule mbabe kule mjengoni ambaye pia ni Spika na Mbunge wa Kongwa huko si ndio kwake?

Amepasahau kabisa?
 
Huko ni mwendo wa virungu na kuzimishana na bungeni ni kushughulikia wapinzani wa Kike.
 
Weka chanzo cha habari yako mkuu..... maana hear says nilizopata ni tofauti na hizo.
 
Hivi hiyo wilaya ya chamwino imekaaje du na kiutawala wanafanyaje kazi. Huwa nikiwa naenda Kondoa napita chamwino , naenda Moro napita chamwino, iringa road napita chamwino. Kiutawala sizani kama inawezekana ni kuwatesa wananchi tu.
 
Wagogo banaa... Na sisiem yao wenyewe akaaa, hawana shida na mtu. Teh teh teh.. Ujinga mzigo sana
 
Back
Top Bottom