Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,483
- 40,010
sambaza kwa email za wafanyakazi wenzako! Inaonekana serikali imeamua ubabe badala ya maelewano; hakuna serikali duniani imewahi kushindana na nguvu za wafanyakazi ikasimama!
Mgomo: Tucta yawaonya wafanyakazi waoga, wasaliti
Jackson Kimambo
Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini (Tucta) limesema wafanyakazi waoga, wanafiki na wasaliti watakaoshindwa kushiriki katika mgomo Mei tano mwaka huu ni vyema wakafahamika na kushughulikiwa.
Hayo yalisemwa na mjumbe wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi (Tucta) kutoka makao makuu, Ernest Kangwa, katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani yaliyofanyikia kimkoa katika uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi juzi.
Hata hivyo, Kangwa hakufafanua wafanyakazi waoga na wasaliti watashughulikuwa namna gani.
Alisema anatambua wapo wafanyakazi wasaliti watakaoshindwa kufanya mgomo kutokana na kuwaogopa waajiri na kwamba kamwe shirikisho la vyama vya wafanyakazi haliwezi kuwavumilia wafanyakazi wasaliti.
Kangwa alisema wafanyakazi wasikubali kugawanyika kwa vitisho toka kwa waajiri na kuwa shirikisho limeandaa mgomo wa kisheria hivyo hakuna mfanyakazi atakayechukuliwa hatua za kisheria ama kufukuzwa kazi.
Alisema mgomo huo ni wa amani mpaka hapo madai yao yatakapotekelezwa na kwamba wafanyakazi watambue kuwa haki haiji hivi hivi hivyo ni lazima itafutwe na kudaiwa kwa namna na hali yoyote ile .
Alisema hakuna ubishi kwamba serikali imeshindwa kutatua kero za wafanyakazi ikiwa ni pamoja na mishahara duni, makato makubwa ya kodi na malipo duni ya uzeeni.
Alisema serikali imeshindwa kudhibiti na kuwashughulikia wahujumu wa uchumi ambao wanachangia kwa kiasi kikubwa katika kuikosesha uwezo wa kuwahudumia wafanyakazi.
NIPASHE