Bango la Wafanyakazi - Wafanyakazi Tanzania tuungane! Mei 5th

Yani katika madai yote hili la mshahara ndo amesisitiza? Wakati hili lina majibu rahisi hata kwa hao wazee tayari wanajua nini ameongopea?

Nataka nisikie majibu yao maana njia panda..........................hasa kwa jinsi ambavyo JK hatakuwa na pakujibia ukiachilia mbali hakujibu hoja ila vijembe tu. Maskini Shein, alikuwa hana hata face to smile.
 
Hii itaenda mkuu...

Rais gani anaeringia nguvu za polisi HUYU?
Anasahau kabisa waliomchagua!
Amekuwa bubu kwa wanaompa hela za kampeni, anatubwatukia wafanyakazi...IHATE HIM!
no way out, katika hili tunapimwa uwezo wa kufikili kama upo ama lah, by next periond keep him awaaaay and his MPs, kama yeye anaringia nguvu ya polisi
na sisi turingie maamuzi ya nani awe rais next tyme
 
Hawa viongozi wa TUCTA wakae chonjo......kwa jinsi muungwana anavyoashiria kutokujali sheria kuna uwezekano mkubwa wakakamatwa hata kabla ya hiyo tarehe ya mgono!

.
Kumbe laana ya nchi hii kuchukua sheria mikononi na kuwachoma vibaka imetokana na uongozi uliopo usiojali haki za binadamu. Maana kama tunaraisi anaedai watu watakuwa na bandegi usoni ni dhahiri kwamba tuna rais anayewasukuma polisi kuwapiga raia marungu badala ya kazi zao za kusimamia sheria. Mawazo kama haya ndio yalisukuma watu kama kina zombe kugeuka vampire jijini Dar wakijua ikulu iko nyuma nyao.
 
Wana Jamii, nadhani muda wa vitendo umefika.. Hongera sana TuCta kwa elimu waliyoitoa siku ya kuadhimisha sikukuu ya wafanyakazi duniani. Na hakika wamesikika kuliko wakati wowote wa mapambano ya haki za wafanyakazi na wakulima. JK asijidanganye kabisa kwamba vitisho vinaweza kumsaidia.. tatizo hili lipo kwa miaka na pengijne anapaswa klufahamu kwamba uchumi wa nchi unakua tu ikiwa wananchi wanaweza kununua mali inayozalishwa hivyo kuuwezesha mzunguko wa fedha na mali.
Mishahara hatoshi na hata kama ikifikia laki 3 bado ipo chini ya mpasuko wa bei uliopo. Anachoshindwakuelewa ni kwamba wafanyakazi wengi huunganisha daladala tatu toka majumbani mwao kufika kazini hivyo hulipa nauli mara sita kwa siku. Na sababu kubwa ni kwamba uwezo wao kifedha hauwezi kulipia pango la makazi mjini. Chumba kimoja tu maeneo ya Kinondoni, Chang'ombe, Magomeni, Ilala, Temeke ni zaidi ya Tsh 50,000 kwa mwezi na inatakiwa kodi ya mwaka mzima. Hakuna sheria yoyote ya kuthibiti uporaji huu.

Nyumba za kupanga hazitoshelezi mahitaji na vibaya zaidi ni kwamba kila nyumba hupangisha maduka kuliko makazi. Chumba kidogo cha Biashara hupangishwa Tsh laki tatu hadi tano ukilinganisha na chumba cha makazi..Hivyo nguvu kubwa imewekwa ktk ujenzi wa maduka na sehemu za biashara kuliko makazi ya wananchi...Chakula kimepanda bei mara mbili (asilimia 200) toka kuingia kwake madarakani pamoja na kwamba thamani ya shilingi imebadilika kidogo sana.
Umaskini umekithiri, kila mtu ni mhitaji na inapotokea serikali kuthibiti Ufisadi ngazi ya chini haya ndio matokeo kwani haikuwa makusudi wafanyakazi kupokea hongo ama kuiba.. Wamechoka kuona wao wakimezwa na sheria hali viongozi ngazi za juu wakipeta na ufisadi...

majuzi tu nikiwa Bongo mdogo wangu alifanyiwa Operation ndogo ya Apendix...Niulize mimi nilitozwa kiasi gani?.. Jumla ya operation ilikuwa laki nane. Laki mbili za vipimo kwa madaktari kisha nikatozwa laki sita na utawala wa Hospital ya Muhimbili. Naambiwa hii ndio bei ya Apendix operation sasa hivi! Hivi kweli tumefikia kiasi hiki bado serikali inawapa watu mishahara tosha! Ni watanzania wangapi wanaweza kulipia gharama kama hizi..Hata malaria inaua zaidi nchi maskini sii kwa sababu mbu ni wengi isipokuwa wananchi wengi hawana uwezo wa kununua hizo dawa. Watoto wanakufa kwa sababu ya uwezo mdogo wa wananchi kutibia maradhi haya... Vyandarua na madawa zinazoletwa kama kampeni ya biashara tu..Kwani nina hakika wapo wananchi waliokwisha dhulika namatumizi ya dawa ile ya mseto. Wengine wamevimba macho, miguu na kadhalika. wapo waliokufa kutokana na allergies zinazopingana na matumizi ya dawa hii..Sidhani kama JK anazo taarifa hizi..
Ushauri wa bure, rais wasikilize wananchi kilio chao, kuwa mwepesi kupokea kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi badala ya kubishana kwani huwezi kushinda hata siku moja...Kiongozi makini hutafuta suluhu pale penye utata na hukemea yale yanayopingana na haki za wananchi hata kama utashindwa kuchukua hatua za haraka.
 
Hivi jamani JK zimo kichwani au ameanza kuumwa zile homa zake za kunmwangusha jukwaani??.

Ni nani wanaomsahuri kiongozi wa nchi adiriki kuzungumza kwa kujiamini kiasi ambacho anashau kuwa hao wafanyakazi ndio hao waliomponya alipopata na mawenge jukwani, ndio wanaoijua siri ya Serikali yake, ndio atakaowatumia katika uchaguzi ujaokumsaidia kuiba kura??.
 
Hivi jamani JK zimo kichwani au ameanza kuumwa zile homa zake za kunmwangusha jukwaani??.

Ni nani wanaomsahuri kiongozi wa nchi adiriki kuzungumza kwa kujiamini kiasi ambacho anashau kuwa hao wafanyakazi ndio hao waliomponya alipopatwa na mawenge jukwani, ndio wanaoijua siri ya Serikali yake, ndio atakao watumia katika uchaguzi ujao kumsaidia kuiba kura??.

#!

http://www.youtube.com/v/AJ9KoGRl7m...&feature=player_embedded&fs=1"></param><param

#!

Hakika angelijua madhara ya kauli zake, asingethubutu kuongea haya na wazee waliositaafu ambao wanaishi kwa kurubuniwa na Sera za CCM. Asidhani mgomo ni kutokwenda kazini tu, akumbuke hizo siri za ndani ya Serikali yake wamekuwa wakizitoa hao wafanyakazi ambao wana njaa na wakati wote wamekuwa wakidhihakiwa kama hivi kana kwamba hawana akili na hawajui yale wanayofanya...so shame to the President to speak like that kama mwalimu wa shule ya Msingi akikemea wanafunzi ambao hawajui iwapo watamaliza shule.....
 
Last edited by a moderator:
Mlishaambiwa kwamba aliwekwa madarakani na wanamtandao na ameshindwa kuwadhibiti.

Ila hili la wafanyakazi alishwahi kutabiri Maganga yule aliyeshiriki uhaini miaka ya themanini kuwa serikali isidhani itapewa msukosuko na jeshi tena bali rai tena ni WAFANYAKAZI. kama Kikwete haamini aende kumuuliza mzee Kaunda kilichomkuta. Pia asidhani kama raisi wetu huwa anafikiria kabla ya kusema. maana hii ya leo ni kali kuliko hata makamba mpayukaji
 
jinsi tunavyoogopa FFU sijui lini tutaweza kuandamana kwa pamoja.maandamano yanasaidia nchi nyingi sana raia wao kupata haki lakini sie watanzania uoga wetu ndio unatuponza.

ttunajisifia amani,ukweli amani yetu inatokana na uoga wetu wa kudai haki zetu na amani ya haina hio sio ya kujivunia hata siku moja kwani inapelekea serikali kutumia madaraka hovyo kama (ufisadi).maovu yote yanaotendwa na viongozi wetu ni kwa sababu sisi wananchi ni waoga .


kama generation moja haito amua kukitokeza kwa pamoja kudai haki basi mpaka vitukuu vyetu vitaendelea kutawaliwa na washenzi.

wafanyakazi tujitokeze kwa pamoja jumatano,umoja ni nguvu.
 
Mlishaambiwa kwamba aliwekwa madarakani na wanamtandao na ameshindwa kuwadhibiti.

Ila hili la wafanyakazi alishwahi kutabiri Maganga yule aliyeshiriki uhaini miaka ya themanini kuwa serikali isidhani itapewa msukosuko na jeshi tena bali rai tena ni WAFANYAKAZI. kama Kikwete haamini aende kumuuliza mzee Kaunda kilichomkuta. Pia asidhani kama raisi wetu huwa anafikiria kabla ya kusema. maana hii ya leo ni kali kuliko hata makamba mpayukaji

Kama kuna familia imewahi kufanya upumbavu, ni ile ambayo inadiriki kumtukana "mtumishi wa ndani" ambaye ndie anayejua unga upo wapi, mboga ipo wapi na moto upo wapi...na apike chakua gani na aweke nini kwenye hicho chakula. Ikiwa mazungumzo kati ya Serikali na Jumuiya ya Wafanyakazi yanaendele, ya nini kwa Kiongozi wa nchi kusimamama na kuanza kuropoka kwa kuwatishia wafanyakazi kama watoto??
 
Huyu anahitaji kupumzika naona hizi safari zake za hapa na pale zimemvuruga akili. Ukitaka kusikia maajabu basi njoo Tz. utakutana na vituko maana huyu mtu ameshindwa kuwaheshimu watanzania kabisa kwa kutaka kuongoza nchi kimabavu. Kazi ipo kweli kweli. Wanasema ukipiga ngumi ukuta utaumia wewe tusubiri tuone. Sijui tujipe pole tulie tuhame sijui tufanye vipi?
 
Chonde chonde TUCTA hamasisheni wafanyakazi ktk sekta zote waweze kugoma na mtafutieni majibu ya uhakika bwana JK kwa sababu amekosa heshima kwa wananchi.
 
Hizi ni dalili nzuri sana, kafika mwisho tumtoeni jamani shibe mwanaalevya atolewe imetosha sasa, inamaana hana masikio? muongo mkubwa awadanganye hao hao hela zipo nyingi tu anazozungukia nje mpaka viongozi wa nchi hizo wamemdharau hawana muda wa kumpokea, alifuata lini juzi new york kwani yeye waziri wa afya ama UMATI? hizo ndege anazozunguka huku na huku bila agenda anatoa wapi mafuta? tumfukuzeni kazi maana ikulu haina kiwanda cha kuzalishia anakula vyetu halafu anatunyea? hela zipo za EPA na Richmond aliyotia sahihi yeye na sasa kamsukumia Lowasa, IPTL pia aliyoweka sahihi wakati akiwa waziri kule na sasa kamrudisha shoga yake Jairo kuhakikisha inaanza kuuzia umeme serikali waendelee kula, zipo za serikali mbili za wakati mmoja za mkewe kuwa na convoy sawa na ya rais na kujipangia ziara ya kitaifa wakati WAMA wafanyakazi hawalipwi miezi na miezi na hakijulikani kinachofanya mikakati hakuna hakieleweki kitu hata bodi ya watu wenye akili wamebaki wanaangalia tu. Fedha ni zile zilizopotezwa kuwahamisha ma DC ili kumu accomodate Husna Mwilima tatizo huyu mtu hasomi mbona yote keshaambiwa na wafanyakazi? Jamani gomeni na sisi tutawaunga mkono mbona Pakistan wametoa dictator tena mwenye manguvu na connections za Alkaida itakua yeye? kuogopa kunatuponya vipi wakati hakuna tulichobakiza maisha magumu wao wanapeta. ALUTA CONTINUE TUCTA msirudi nyuma ubora mkae nyumbani gharama ni chache kuliko kwenda kazini acheni ku subsidize serikali yake kwa akiba yenu hafifu. Ni kweli nawashangaa hao DAWASCO na hayo mabenki si tu ni wasaliti ni wapumbavu maana kama kina Nyerere wasingejitoa wao hivyo vibarua vya kunyonywa kama mbwa wangevipata wapi? hapo walipo hivyo vijinshahara ni asilimio ndogo sana ya wenzao wa afrika kusini na wadachi waache wabakie hapo hapo kwa kuishi kwa ten percent siku wakitoka hapo ndio watalijua jiji kwa pension za elfu sita badala ya kupigania kitu sustanable, cheap Tanzanians hao walaaniwe kabisa wanafiki wakubwa
 
"..hata wakigoma miaka minane wakarejea tena 315,000 hazipo.."!

Hivi hawa Wazee walilipwa kuhudhuria huu mkutano? Ni kipi hasa walichokuwa wanashangilia?

This is disgusting!
 
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]How Big is a Trillion?[/FONT]

[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]In the U.S., one trillion is written as the number "1" followed by 12 zeros (1,000,000,000,000). One year of clock time [/FONT]​

Sasa Muheshimiwa anaposema kuwa ana wafanyakazi 350,000 na kama akiwalipa Tsha 315,000 serikali itakuwa imetumia Tsha Trillion 6 hii ni kweli jamani? hebu tuone
Watu 350,000 X Tshs 315,000= 110,250,000,000 kwa mwezi .( hizi ni 1,323,000,000,000 tu au mnasemaje?).
Na yeye kasema kuwa pato letu la taifa linafika trillion 6 ( 6,000,000,000,000). Ukichukua kuwa watu wachache sana wanaopata mshahara ulio zaidi ya huu wa Tsha 315,000 basi sema inafika two trillion na kubaki na hizo nne a kutumbua na kununua mashangingi.

Haishangazi sana lakini kwani alikuwa anaongea na watu walio choka sana kimaisha na fikra!
 
Shalom.. kwa maneno yake mwenyewe alisema kuwa asilimia 30 ya bajeti yetu (ambayo yenyewe ni trilioni 6) huishia mikononi mwa mafisadi..... je kiasi hicho (cha asilimia 30) kinalipa watu wangapi kwa 315,000 ?
 
Back
Top Bottom