Bandari yasaka meli 65 zilizotoweka

Hao waliompa Mhe. taarifa kwa nimi walisubiri hadi zimefika meli 65? kama sio kukosa mgao basi nao ni majipu
Hajatamka mwaka lakini hiyo utakuwa CAG report ya mwaka mmoja. Ukumbuke kama TPA waliweza kuiba port charge ya kintena $600 wasingeshindwa kuiba docking fee ya $30,000 kwa meli moja. Wizi ulikuwa kila sekta, kila mtu akijichotea kwa wakati wake.
 
kwa nini mamlaka ya bandari isikabidhiwe kwa kikosi cha JESHI cha wanamaji?? civilians real sucks
 
MAMLAKA ya Bandari Tanzania (TPA) imesema inatafuta taarifa kuweza kubaini meli zaidi ya 65 zilizoingia na kushusha mizigo nchini bila kulipa kodi.
Hiyo ni baada ya Rais Dk. John Magufuli, kueleza madudu aliyoyakuta ndani ya Bandari ikiwamo jinsi meli 65 zilivyoingia na kushusha mizigo bila kulipa ushuru wa Serikali.

Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Gladson Urioh, alisema tangu Rais Magufuli alipotoa kauli hiyo hivi karibuni akiwa wilayani Chato, Mamlaka imekuwa ikifuatilia taarifa hizo.

“Hili suala la meli zaidi ya 65 kuingia na kutolipa kodi tunalifuatilia kwa undani sisi TPA pamoja na wadau wote vikiwamo vyombo vya ulinzi.

“Bandari ina wadau wake ambao ni pamoja na vyombo vya ulinzi, Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi kavu (Sumatra), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Dawa na Chakula (TFDA), Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Idara ya Uhamiaji, Idara ya Afya na Mkemia Mkuu wa Serikali na wengine.

“Tunaamini kwa umoja wetu huu tutapata taarifa kwa undani kuhusu suala hili la meli,” alisema Urioh.

Wiki iliyopita akiwa wilayani Chato, Rais Dk. John Magufuli, alifichua zaidi madudu ndani ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) akieleza jinsi meli 65 zilivyoingia na kushusha mizigo nchini bila kulipa ushuru wa Serikali.

Alisema meli hizo zilishusha mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam na baada ya kupakua mizigo hiyo ziliondoka bila kujulikana zimekwenda wapi.

“Ndugu zangu tusipochukua hatua nchi itatushinda leo (juzi) pale bandari zimeingia zaidi ya meli 65 zimeshusha mizigo na hazikuonekana, hivi inawezekana vipi meli ishushe mizigo na kutokomea bila kulipa mapato ya Serikali?

“Meli zilileta mizigo zikashusha na zikapotea hivyo hivyo na Serikali ikakosa hela. Jamani ndani ya Serikali kuna madudu ya kila aina hivyo ninawaomba mniombee, nimejitoa sadaka kwa ajili ya Watanzania,” alisema Rais Magufuli huku akishangiliwa.

Source: Mtanzania
Ninajiuliza,tumuombee ili iweje? aendelee kujua madudu mengi zaidi,aendelee kua mvumilivu,au asipate taarifa zaidi.Hivi hujui kua wahujumu nao wanaomba na wanakuombea na wewe uwe na subira ya kutowatumbua?Inakuaje umuweke mtu mahali aihujumu nchi usimuwajibishe mapema useme tukuombee? Mh.Raisi kadri unavyo baini huo utumbo wanaoufanya na kutuhabarisha sisi ujue wanafanya wawezalo kuharibu mazingira ya ushahidi.Hapo zishaachezwa rafu za kutosha tangu uyaseme hayo.Nikweli hatua unawachukulia watu lakini kwa hawa umechelewa baba.Napendekeza bunge litunge sheria(kama haipo) ya kunyonga hadharani wahujumu uchumi wa nchi hii hapo ndio tutaheshimiana
 
Hajatamka mwaka lakini hiyo utakuwa CAG report ya mwaka mmoja. Ukumbuke kama TPA waliweza kuiba port charge ya kintena $600 wasingeshindwa kuiba docking fee ya $30,000 kwa meli moja. Wizi ulikuwa kila sekta, kila mtu akijichotea kwa wakati wake.
Rais alitumia neno "juzi" basi hatukumuelewa wengi
 
Mhhhhhhh! hii sasa mimi Napata wasiswasi,, Makontena over 2000 yalitoweka, Hatujui haitima yake mpaka leo hatuambiwi ni wangapi wamekamatwa na wamelipa kiasi gani na wako wapi sasa,,, Tena leo Meli 65!!! Hizi meli kila moja ilikuwa na Contena ngapi??​
 
Nashindwa kuelewa ktk hili. Mhe Rais amebadilisha wateule wote aliowakuta ktk Mamlaka ya Bandari na kuwapa vyeo aliyeona ni watu safi wasio na mawaa. Aidha Mhe Rais alibainisha kuwa yoyote atakayeenda kinyume naye atamwajibisha mara moja.

Sasa anapotueleza wananchi juu ya wizi huo bila kuchukua hatua stahiki, si kama anaendeleza uzoefu wa Viongozi wetu kulalamika tu. Je sisi wananchi si itabidi tuanze kumwaga machozi kwa kitendo cha kiongozi wetu mkuu kushindwa kutekeleza kwa vitendo kauli yake "HAPA KAZI TU" ikishereheshwa na "UTUMBUAJI MAJIPU"
 
Rais alitumia neno "juzi" basi hatukumuelewa wengi
Imebidi nirudie kusoma. Ukweli utabaki kuwa bandari yetu haiwezi kupokea meli 65 kwa siku. Ina gati 9 tu. Bado naamini hiyo ni ripoti ya muda fulani ingawa ametumia neno leo
 
Awatumbue hao wateule wake ndio tutaamini kauli mbiu yake tofauti na hivyo CCM ni ile ile

Mkuu ukisema hivyo utakuwa hujawatendea haki.

Hizi meli ni wakati wa mzee wa kuchekacheka. Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vilikuwa vikifanya kazi kwa moyo wa uzalendo, cha ajabu taarifa zao zilikuwa zikipuuzwa. Kiongozi akiwa na makundi tu mambo hayaendi mkuu. Ndo maana unaona ilifika kipindi nchi ikawa kama haina serikali kwani hata taarifa nyeti mzee wa kuchekacheka alikuwa akizitoa wa watu wake kwa ajili ya ushauri na uamuzi. Mamlaka ya Bandari wasitudanganye sisi wananchi. Wewe Bwana Urioh ni kitu gani usichojua kuwa Mamlaka ya Bandari kupitia kitengo cha operations mumekuwa mkishiriki kwa kiasi kikubwa kuujumu shirika na serikali kwa ujumla. Wewe ni mmoja wapo wa wanufaika wa pesa zinazotokana na ukwepaji ushuru na kodi unaofanywa na meli hizi. Ni kitu gani unachotaka kutuaminisha kuwa hujui wakati siku zote wafanyakazi wa Bandari kupitia kitengo cha operations na Marine wamekuwa wakichukuwa cash money kutoka shipping lines/agents badala ya malipo hayo kufanyika kwa njia ya cheque. Kama hujui kinachoendelea, huo Mgao unaopokea kila baada ya meli kuwa imeondoka hujiulizi hizo pesa zinatoka wapi? na kwanini upokee mgawo wa pesa usiozojua chanzo chake?

Wewe mwenyewe unajua kabisa jinsi watu wako wanavyo shusha masaa ambayo meli imekaa berth kwa ajili ya kupakia au kupakuwa mizigo ili muweze kupata pesa za wizi kutoka shipping lines/agents.

Mchezo wote unaufahamu fika usitake kutudanganya wananchi kuwa mnafuatilia kubaini.

Tunajua kuwa general cargo ships zinakaa wakati mwingine mwezi mzima berth lakini mnafanya ujanja na shipping lines/agents, kwenye documents inaonyesha meli imekaa week moja. Hivyo hela ya week moja ndo kampuni ya meli italipa mamlaka na kiasi kilichobaki mnachukuwa cash mnagawana kuanzia watu wa shipping lines? nanyi watu wa bandari.

Wewe ni mmojawapo wa wajipu yanayosubiri kutumbuliwa.
 
Mshauri wa rais ni mtu mwenye akili nyingi sana kuliko rais mwenyewe na ni mtu ambaye hamtakii mema rais.

Ukisoma majibu ya mamlaka ya bandari kwa undani ni kwamba mamlaka inambishia rais kwamba hakukuwa na kitu kama hicho na kwamba ulinzi uliopo na taratibu zilizopo kamwe meli 65 zisingeshusha mzigo na kutoweka.

Mimi naamini anayempa rais habari hana nia njema naye na kwa ajabu rais hafanyi verification za habari anazopata. Tumeona sehemu nyingi akidanganywa hadi kufanya maamuzi ambayo baade anayabadiri. Mfano, kusitisha ujenzi wa bandarini ya bagamoyo, wafanyakazi hewa BoT, wakurugenzi wanaolipwa 36M, kupiga marufuku uingizaji sukari, nk. Ifike wakati rais awe na uhakika na anachoambiwa na ajiridhishe, raia wa Tz anamshangaa rais anaposema kuna meli 65 zimeshusha bila kulipa kodi kipindi hiki ambacho wakusanya kodi wako macho zaidi. Mwananchi wakawaida anajiuliza kwanini usalama wa taifa unaompa rais taarifa hizo haukuwapo wakati meli zikifunga Nanga? Huyo aliyempa taarifa hizi bado amebaki kazini?
great thinker always think great,inawezekana wanampa matango pori,meli inapo berth pale inajulikana ni shippingline gani meli yao imefunga kama hawajalipa kodi wampe mkuu deatil za kutosha,waseme vessel flan imeberth tar flan nioneshe kodi stahiki wanayopaswa kulipa jee imelipwa. aliempa taarifa labda kaona meli za kichawi zimebeba wazungu sio container
 
Mkuu ukisema hivyo utakuwa hujawatendea haki.

Hizi meli ni wakati wa mzee wa kuchekacheka. Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vilikuwa vikifanya kazi kwa moyo wa uzalendo, cha ajabu taarifa zao zilikuwa zikipuuzwa. Kiongozi akiwa na makundi tu mambo hayaendi mkuu. Ndo maana unaona ilifika kipindi nchi ikawa kama haina serikali kwani hata taarifa nyeti mzee wa kuchekacheka alikuwa akizitoa wa watu wake kwa ajili ya ushauri na uamuzi. Mamlaka ya Bandari wasitudanganye sisi wananchi. Wewe Bwana Urioh ni kitu gani usichojua kuwa Mamlaka ya Bandari kupitia kitengo cha operations mumekuwa mkishiriki kwa kiasi kikubwa kuujumu shirika na serikali kwa ujumla. Wewe ni mmoja wapo wa wanufaika wa pesa zinazotokana na ukwepaji ushuru na kodi unaofanywa na meli hizi. Ni kitu gani unachotaka kutuaminisha kuwa hujui wakati siku zote wafanyakazi wa Bandari kupitia kitengo cha operations na Marine wamekuwa wakichukuwa cash money kutoka shipping lines/agents badala ya malipo hayo kufanyika kwa njia ya cheque. Kama hujui kinachoendelea, huo Mgao unaopokea kila baada ya meli kuwa imeondoka hujiulizi hizo pesa zinatoka wapi? na kwanini upokee mgawo wa pesa usiozojua chanzo chake?

Wewe mwenyewe unajua kabisa jinsi watu wako wanavyo shusha masaa ambayo meli imekaa berth kwa ajili ya kupakia au kupakuwa mizigo ili muweze kupata pesa za wizi kutoka shipping lines/agents.

Mchezo wote unaufahamu fika usitake kutudanganya wananchi kuwa mnafuatilia kubaini.

Tunajua kuwa general cargo ships zinakaa wakati mwingine mwezi mzima berth lakini mnafanya ujanja na shipping lines/agents, kwenye documents inaonyesha meli imekaa week moja. Hivyo hela ya week moja ndo kampuni ya meli italipa mamlaka na kiasi kilichobaki mnachukuwa cash mnagawana kuanzia watu wa shipping lines? nanyi watu wa bandari.

Wewe ni mmojawapo wa wajipu yanayosubiri kutumbuliwa.
Dah, mkuu umeongea kwa machungu sana, tatizo wanaotakiwa kupeleka hizi taarifa kwa Mukulu au sehemu nyeti wanasikia maneno haya??
Au na wao ni wahusika wana kamgawo kao??
 
Nchi yetu inapaswa kuingia kwenye Guinness book of record...
kontena 2000 na zaidi zinapotea
na sasa meli 65 zinatoweka

Kuna mengine unajua unashindwa ata kuyaamini, meli zimefika zikamwaga mizigo kama gari inavyomwaga mchanga then naodha akatimua maji na kutoweka au! haya ukiyasema popote tofauti na Tz unaweza usiaminike kama unamaanishe meli inayobeba matani kwa matani au meli ya kuchora.
 
Dah, mkuu umeongea kwa machungu sana, tatizo wanaotakiwa kupeleka hizi taarifa kwa Mukulu au sehemu nyeti wanasikia maneno haya??
Au na wao ni wahusika wana kamgawo kao??

Mkuu hili liko wazi kabisa, hawajamaa wanajitahidi kufanya kazi kwa bidii. Na taarifa zinafika sehemu husika. Nilichotaka kusema hapa ni kwamba, wakati wa mzee wa kuchekacheka taarifa kama hizi alikuwa anazipata kabisa. Lakini kwa kuwa naye alikuwa kwenye makundi ya kutuibia, basi alikuwa hazifanyii kazi na badala yake alikuwa akivujisha taarifa hizo kwa marafiki wa kundi la upigaji. Taarifa alizosema Mh. Rais akiwa mapumzikoni huko Chato kuhusu meli 65 kutolipa ushuru siyo za kipindi hiki. Hizi taarifa ni za miaka mitatu au minne huko nyuma. Ambazo mzee wa kuchekacheka hakuzifanyia kazi.

Kitendo cha mzee wa kuchekacheka kupuuzia taarifa nyeti za ukwepaji kodi na ushuru kulifanya hata baadhi ya jamaa hawa kutumia mwanya huo kujinufaisha. (Hii ni nature ya binadamu wala mimi siwalaumu. Mfano mdogo ni pale mtoto wako atakapokuletea taarifa za vitendo vya kijana wako mwingine zisivyo nzuri badala ya kuchukuwa hatua wewe ukampuuza. hata ikitoe siku nyingine mtoa taarifa akiona huyo ndugu yake anafanya jambo la kuhatarisha uhai wako hawezi kukwambia kwani anajua huwa unampuuza). Kuwapuuza watoa taarifa kwa mkuu (mzee wa kuchekacheka) ndiko kuliko sababisha nchi ionekane kama haina serikali.

Mimi nazidi kusisitiza kuwa uongozi wa Bandari usijinasibu kuwa wanafuatilia kujua meli hizo 65 zilizokwepa kulipa ushuru ili hali wakijua mchezo walokuwa wakifanya.

Urio usitake kutudanganya kana kwamba hatujui kuwa kabla meli kufunga berth au outer anchorage huwa Mamlaka tayari ina taarifa zote. Unatotwambia huna records za meli hizo, nini umuhimu wa port meetings mnazofanya kati yenu na shipping lines/agents? Urio unajua fika kuwa vikao hivi ni vya ku-update taarifa za meli zinazotarajia kufunga gati bandarini. Leo unakunya na taarifa za kipuuzi eti mnafuatilia hizo meli.

Urio usijitoe ufahamu ili hali ukijua kuwa Mamlaka ya bandari mlikuwa mkivuta pesa haramu kutoka makampuni ya Diamond shipping, Sharaf shipping, Maersk line Barwil shiiping agent na kuwaachia wasilipe ushuru wa bandari au walipe kiasi kidogo kuliko malipo halali??
Acheni kutufanya sisi wananchi hatujui hujuma mnazo zifanya za kukwepa kodi na ushuru kwa kushirikiana na makampuni ya uwakala wa meli.
 
Back
Top Bottom