Bandari ya Zanzibar imeshapita IGA na Oman kwa sasa ni mikataba ya HGA

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,883
109,213
Zanzibar hamuisikii ikiongelewa kwa kuwa yanayofanyika Zanziba sasa hivi ni tayari wapo hatua za utendaji. Mikataba imefikia hatua za kibiashara, siyo IGA tena.

Mikataba ya Kibiashara hatuwezi kuivujisha sisi lakini kwa kuwa wenyewe watendaji wamewachia, sasa hatuna "obligations" za " Non Disclosure agreements": Wale wambea, majibu yenu hayo:

On January 28, Tanzania’s Zanzibar and Oman Investment Authority signed a memorandum of understanding on Thursday to implement a port master plan on the Indian Ocean coastline of the archipelago. The agreement calls for the development of major ports in the coastal areas of Mangapwani and Bumbwini in the Zanzibar Islands.

f75c6c5fa093c7916415572b2365e63b.jpg

According to the memorandum, the two parties will cooperate to build a large modern port in Mangapwani, about 25 kilometers north of Malindi Port on San Island, for loading and unloading containers, general cargo, and oil and gas.

a749066a033b02dc2019bb93786da965.jpg

Mwini said that this is a major measure taken by the San government to develop the blue economy. It will develop San into a commercial and tourist center in East and Central Africa through the construction of necessary infrastructure in the future. He instructed Sang's relevant government departments to immediately conduct a feasibility study on this multi-billion-dollar project and make sure to make it a success. He also said that the Sang government will retain the plan of the previous government to build a new port in Mpiga Duri (about 3 kilometers north of Malindi Port) and build the port into a fishing port. The existing Malindi Port will be transformed into a special tourist port.Editor/Huang Lij

Somma zaidi na Chanzo: Zanzibar, Tanzania and Oman sign agreement on port development master plan--Seetao.
 
Inaumiza sana .
Mwekezaji wa kuendesha bandari ya Zanzibar kapewa miaka mitano tu ya kuendesha bandari,
Mwekezaji huyo kutoka ufaransa ataendesha bandari kwa miaka mitano tu na mkataba utaangaliwa upya kama kafikia malengo ataongezewa muda na kama hajafikia malengo atapewa mwekezaji mwingine upya,
Tanganyika au Tanzania Bara wameshindwa nini kwenda kujifunza kwenye mikataba ya kitaalamu hata hapo Zanzibar?
Tuwaombe sasa mkajifunze ni namna gani Zanzibar kama nchi wameweza kuingia mikataba mizuri tena ya kueleweka kuliko ninyi ambao inaonekana hamuelewi kitu chochote,
Kajifunzeni nchi ya Zanzibar inafanyaje mikataba yenye tija na mizuri sana ,

Kijana wa kichotara, unaonesha huelewi unachokiongea, hebu jionee ji bandari hilo juu linalojengwa, hilo kujenga peke yake mpaka likamilike labda miaka 5, maana hapo ni kisiwa ambacho hakina chochote, wanaanza "from the scratch".

Hicho unachosema wewe labda ni ya vimeli vidogo kama pale kwetu ilipowekwa meli ya samaki ya magufuli mpaka ikafia hapohapo, tunalipa deni.
 
Kutoka mwanzo waTanganyika walikuwa na nia njema sana na muungano. Ndiyo maana walijitolea kila kitu kufanikisha muungano. Hawajibagui wala kuwabagua wenzao. Iwe ni kijamii, kisiasa, kiuchumi na hata kiuongozi. Na wanajisikia vizuri hata pale kiongozi wao anapokuwa ni Mzanzibari. Lakini kinyume chake wazanzibari na Zanzibar kwa ujumla wana ile "CHAKO NI CHETU LAKINI CHANGU NI CHANGU"

Viongozi wa upande moja wanaposhiriki jambo lenye effect upande wa pili wanatakiwa kuwa waangalifu na wazalendo. Na kwa sababu waTanganyika wengi (%kubwa) wameshaonyesha kutaka kuwa chini ya mikataba inayotweza utu wao. Ukarimu wao usifanywe ujinga wao.

Watu wa bara wangefanya kidogo tu kama wazanzibari , ya chako ni chetu lakini yangu ni yangu. Muungano huu ungeshakufa karne iliyopita. So waTanganyika wasifanywe wapumbavu. Mikataba iwe fair na wasilazimishwe, kisa wawekezaji ni wajomba, au wa baba mdogo nk.
 
Mbona Zanzibar inaongozwa na Marais hao unaosema wa bara, awamu ngapi ngapi?

Mama DSamia si kazi ya Mungu haina makosa? Au alienda kugombea Urais?

Hili ni jibu la wale wanaouliza kuhusu bandari.
 
Kumbuka zanzibar kulikuwa na soko la watumwa sasa inauza ardhi iliokuwa ikiwakamata watumwa🤣🤣
Hata bagamoyo lilikuwepo, hata Tabora, Kigoma, yalikuwepo. Soma historia yako vizuri.

Machifu ndiyo walikuwa wanauza nguvu kazi na vidosho na AlhamduliLlah wameelekea dunia nzima siyo Zanzibar tu.

Sasa ndugu yangu, uwe na Bandari kubwa ya pekee Unguja na uwe na soilko kubwa halafu soko la watumwa lisiwepo? Na enzi hizo ni kama sasa tumelainisha tu, tunawaita "watumishi" wa, wa, wa, Siku hizo watumwa. Ni yale yale tu.

Hivi sasa hakuna watu wanaosafirishwa kwenda nchi za nje kwa baraka za serikali yetu? Why?

Tumewatupa huko? Hatuwahitaji?

Au ndiyo "utumwa mambo leo"?
 
On January 28, Tanzania’s Zanzibar and Oman Investment Authority signed a memorandum of understanding on Thursday to implement a port master plan on the Indian Ocean coastline of the archipelago. The agreement calls for the development of major ports in the coastal areas of Mangapwani and Bumbwini in the Zanzibar Islands.

FaizaFoxy hongera kwa jitihada zako kuweka mambo sawa kuhusu uwekezaji bandarini kupitia DPW, kampuni ya Emirate ya Dubai. Pamoja na juhudi zako za utetezi, ikabidi utuwekee mfano huo pasipo kueleza tofauti ya maudhui na utekelezaji, kisheria, wa "MoU" na "IGA".

Nitaendelea kuonesha shaka yangu kuhusu mkataba wa IGA. Ni ukweli tu utaniweka huru na wenye mashaka kama mimi.

Serikali bado inaongelea faida za IGA zaidi kuliko madhara yaliyomo kwenye baadhi ya vifungu vya IGA ambavyo kama mikataba ya utekekezaji (HGAs) itaandaliwa katika misingi hiyo. Na kwa kuwa hiyo mikataba ya utekelezaji inabaki siri, kwa nini tusiwe na mashaka?

Kwa vyovyote vile, wenye mawazo kama mimi, tumetia shaka, pamoja na dhamira nzuri ya Serikali, ikitokea kuna sababu za kusitisha mkataba Kifungu cha 23: Muda na Utaratibu wa Kusitisha Mkataba, kina ukakasi. Ukinieleza ukweli wa hicho kifungu, kwa maslahi mapana ya kitaifa, utakuwa umeniweka huru.

Kifungu kidogo cha 4. Nchi Wanachama hazitakuwa na haki ya kushutumu, kujiondoa, kusimamisha au kusitisha Mkataba huu katika hali yoyote, hata ikitokea ukiukwaji wa mkataba (material breach), mabadiliko ya kimsingi ya hali, kuvunjika kwa uhusiano wa kidiplomasia au kibalozi, au sababu zingine zozote zinazotambuliwa chini ya sheria ya kimataifa. Bila kujali yaliyotajwa hapo juu, mgogoro wowote kati ya Nchi Wanachama kuhusiana na hali kama hizo utashughulikiwa kulingana na mahitaji ya Ibara ya 20 ya Mkataba huu.

Ni nini maana ya material breach?

Kifungu cha 20 kinahusu Utatuzi wa Migogoro, Kifungu kidogo cha 3. Migogoro chini ya Mikataba ya Mradi na HGAs pia itatatuliwa kupitia usuluhishi wa kimataifa katika ukumbi na kiti kisichoegemea upande wowote..

Kifungu kidogo hicho ni kinyume na Kifungu cha 21: Sheria itakayo ongoza Mkataba huu itakuwa Sheria ya Uingereza ambapo sheria ya uongozi wa kila HGA na Mikataba ya Mradi husika itakuwa ni kwa sheria za Tanzania

NASUBIRI UFAFANUZI WAKO

Kazi iendelee.
 
Mbona Zanzibar inaongozwa na Marais hao unaosema wa bara, awamu ngapi ngapi?

Mama DSamia si kazi ya Mungu haina makosa? Au alienda kugombea Urais?

Hili ni jibu la wale wanaouliza kuhusu bandari.
WaTanganyika hawana sera za chako ni chetu changu ni changu. Mbarawa na wanasheria wake walitakiwa kuwa waadilifu vinginevyo yuko pale kimkakati.

Pili draft iliyotumika ni ya Dp world. Kwanini draft ya upande moja ndiyo ifanyiwe kazi. Unatoa rasilimali zako kwa draft ya mtu mwingine ?! . Ni kama vile rasilimali hiyo imekuchosha. Huitaki tena hata ikienda bure milele !! Kwanini sisi wenye rasilimali tusiwe na draft yetu . Kuwe na nipe nikupe !!

Only in Tanganyika
 
Tangayika iko wapi wewe, huna hata haya? Watanganyika ni kama mimi niliezaliwa Tanganyika mpaka cheti changu cha kuzaliwa kimeandikwa nimezaliwa Tanganyika.

Wewe kujiita Mtanganyika ni kujidanganya tu. Jina sahihoi la kujiita wewe ni Mdanganyika.

Kamuulize robot wenu AI Chat GPT, au niwaulizie mimi mlione jibu?

Kama unaipenda sana Tanganyika ingiya mitaani uvunje Muungano, halafu uanze mchakato wa kuifufuwa maiti. Si mmezowea lakini kufufuwa maiti> Au wewe siyo Mkristo?

Unajuwa kuwa Watanganyika wako Fiji? Au elimu yako ni finyu hujakutana nalo hilo?
 
😆😆😆 Hukosi majibu kila swali una jibu lake

404: Page Not Found
Kuhusu Fiji ni kweli kabisa, kuna kabila huko linaitwa "Korobebe" linasemekana lilitokea Tanganyika zamani, Inaweza kuwa waha hawa au Wamanyema hawa, kabisa: Jisomee:

Ratu-Marika-Saukuru.jpg

Ratu Marika Saukuru, the head of the Ne Clan in Korobebe Village in Nadi. Picture: VILIAME RAVAI
The story of how the iTaukei people came to inhabit Fiji initially is a contentious subject.
Some accounts tell of how the ancestors of the first Fijians — Lutunasobasoba and Degei — travelled from Lake Tanganyika in Africa to Fiji.

Huwa sikisii.

Chanzo na soma zaidi:
 
Zanzibar hamuisikii ikiongelewa kwa kuwa yanayofanyika Zanziba sasa hivi ni tayari wapo hatua za utendaji. Mikataba imefikia hatua za kibiashara, siyo IGA tena.

Mikataba ya Kibiashara hatuwezi kuivujisha sisi lakini kwa kuwa wenyewe watendaji wamewachia, sasa hatuna "obligations" za " Non Disclosure agreements": Wale wambea, majibu yenu hayo:

On January 28, Tanzania’s Zanzibar and Oman Investment Authority signed a memorandum of understanding on Thursday to implement a port master plan on the Indian Ocean coastline of the archipelago. The agreement calls for the development of major ports in the coastal areas of Mangapwani and Bumbwini in the Zanzibar Islands.

f75c6c5fa093c7916415572b2365e63b.jpg

According to the memorandum, the two parties will cooperate to build a large modern port in Mangapwani, about 25 kilometers north of Malindi Port on San Island, for loading and unloading containers, general cargo, and oil and gas.

a749066a033b02dc2019bb93786da965.jpg

Mwini said that this is a major measure taken by the San government to develop the blue economy. It will develop San into a commercial and tourist center in East and Central Africa through the construction of necessary infrastructure in the future. He instructed Sang's relevant government departments to immediately conduct a feasibility study on this multi-billion-dollar project and make sure to make it a success. He also said that the Sang government will retain the plan of the previous government to build a new port in Mpiga Duri (about 3 kilometers north of Malindi Port) and build the port into a fishing port. The existing Malindi Port will be transformed into a special tourist port.Editor/Huang Lij

Somma zaidi na Chanzo: Zanzibar, Tanzania and Oman sign agreement on port development master plan--Seetao.
Hayo ni yao
Sisi tunachotaka ni afya ya mkataba baina yetu na Dubai, narudia afya ya mkataba, mbona mnakwepa hoja ya msingi?
 
Kuhusu Fiji ni kweli kabisa, kuna kabila huko linaitwa "Korobebe" linasemekana lilitokea Tanganyika zamani, Inaweza kuwa waha hawa au Wamanyema hawa, kabisa: Jisomee:

Ratu-Marika-Saukuru.jpg

Ratu Marika Saukuru, the head of the Ne Clan in Korobebe Village in Nadi. Picture: VILIAME RAVAI
The story of how the iTaukei people came to inhabit Fiji initially is a contentious subject.
Some accounts tell of how the ancestors of the first Fijians — Lutunasobasoba and Degei — travelled from Lake Tanganyika in Africa to Fiji.

Huwa sikisii.

Chanzo na soma zaidi:
Aiseee kumbe unamaanisha watanganyika wapo Fiji 😁 Ila hawa wanaobaguana huku ni machotara ya wanzanzibar na wazanzibara

404: Page Not Found
 
Pili draft iliyotumika ni ya Dp world. Kwanini draft ya upande moja ndiyo ifanyiwe kazi. Unatoa rasilimali zako kwa draft ya mtu mwingine ?! . Ni kama vile rasilimali hiyo imekuchosha. Huitaki tena hata ikienda bure milele !! Kwanini sisi wenye rasilimali tusiwe na draft yetu . Kuwe na nipe nikupe !!

Only in Tanganyika
Kijana, ya DP World siyo "Draft" ni IGA. Ya Zanzibar ni Contract.

Unafahamu tofauti ya 'agreement" na "contract"?

Mambo mengine muwe mnauliza tuwape darsa, siyo mnajifanya mnajuwa kumbe hamjuwi. Kuuliza si ujinga. Kujifanya unajuwa kumbe hujuwi ndiyo ujinga.

Msikilize Dhahabu nyeusi anawachambuwa wajinga wa Afrika na Ujinga wao. Bofya chini hapo:

Hayo ni yao
Sisi tunachotaka ni afya ya mkataba baina yetu na Dubai, narudia afya ya mkataba, mbona mnakwepa hoja ya msingi?
Afya ipo hospitali.

Hapa sema kinachokusibu kuhusu Zanzibar na bandari. Kama unahitaji ufafanuzi wa IGA. bofya chini hapo, ukapate sindano za Dr. Ally Possy utarudisha tu "afya" yako. Bofya chini hapo:

Kutoka mwanzo waTanganyika walikuwa na nia njema sana na muungano.
...
Viongozi wa upande moja wanaposhiriki jambo lenye effect upande wa pili wanatakiwa kuwa waangalifu na wazalendo. Na kwa sababu waTanganyika wengi (%kubwa) wameshaonyesha kutaka kuwa chini ya mikataba inayotweza utu wao. Ukarimu wao usifanywe ujinga wao.

Mkuu Odhiambo cairo, umeleta hoja inayofikirisha ya Utanganyika. Nasema hivyo kwa sababu ya tukio la uwekezaji bandari za Tanzania bara chini ya utawala wa Mtanzania kutoka Visiwani kama ilivyokufa Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea enzi za Utawala wa Awamu ya Pili kwa Azimio la Zanzibar.

Naamini kwamba WaTanzania bara wengi hawapendi wala wasingependa kuitwa waTanganyika, kama waTanzania au waTanzania wa Visiwani wanavyopenda kujiita au kuitwa waZanzibari, na hawajiiti waTanzania.

Kwa sababu hiyo na hizo ulizotaja Mkuu Odhiambo cairo, ukweli inabidi usemwe kuwa suala la uwekezaji katika bandari za Tanzania bara, kwa mkataba (IGA) wenye vifungu tata, chini ya utawala wa Mzanzibari, wakati makubaliano ya IGA ni kati ya JMT na Serikali ya Dubai, ni dhahiri kunaleta hisia ya Utanganyika.

Moyoni, naomba sana tusifikishwe kuanza kujiita waTanganyika au waZanzibari kukapelekea kudai Tanganyika ndani ya Muungano wa Serikali mbili, moja ikiwa haina jina. Waanzilishi wa Muungano, pamoja na kuwa na nia njema, tofauti hiyo hawakuiona, na kama waliona, hawakutilia maanani, kuwa ingekuja kuleta madhara.

Mungu aipushe mbali fikra potofu, na kama ulivyoshauri Mkuu Odhiambo cairo Viongozi wa upande moja wanaposhiriki jambo lenye effect upande wa pili wanatakiwa kuwa waangalifu na wazalendo
 
Nimeweka link hapo kuna Watanganyika wanawekeza Fiji kwa miaka sasa, sasa waambie Wafiji kwanini hao Watanganyika wanawekeza huko na kwanini wapo serikalini tena viongozi.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Kwa ID yako wewe ni mama FaizaFoxy, naomba sana turejee kwenye hoja yako ya msingi kwenye huu uzi wako badala ya kuhamisha mada. Pia rejea kwenye maswali ya msingi kuhusu utata kwenye vifungu vya mkataba wa IGA.

Japo uliweka maelezo ya Dr Possy (ambatanisho), ni maelezo na tafsiri yake binafsi ya mkataba ambayo mahakamani yanapingwa. Isitoshe, ama unakwepa kujibu au huna majibu ya hoja za bandiko langu #7
 
Back
Top Bottom