Balozi wa Tanzania DRC hana msaada

BarakaJr

JF-Expert Member
May 4, 2014
289
78
Rais amefanya mabadiliko ya wakuu wa Wilaya, sasa ni wakati wa kufanya mabadiliko kwa hawa mabalozi wetu hasa huyu aliyeko huku D.R.C kwani hana msaada kwa waTanzania hata pale anapopewa taarifa.

Amekua ni mtu mwenye kiburi na jeuri.

Rais tunakuomba utuondolee huyu mtu.Na pia imefikia mahali sasa Tanzania iwe na ofisi ya mwakilishi wa balozi mjini Lubumbashi mkoa wa Katanga, kwani ndipo waTanzania wanafika kwa wingi kuliko huko Kinshasa.

HUYU MTU NI TATIZO SANA.
 
Huenda yupo bize akigegeda madini ,tayari kawa bilionea,kwani mabalozi wetu kazi yao ni kujitajirisha wao na familia zao,huoni yule alikuwa balozi wetu kule SA alivyovuna tu utajiri kwa kuleta makaburu na ubalozi akauacha.
 
Mimi nisaidiwe kufahamu ni balozi aliye nchi gani anayefanya la maana!!??
 
Kama Hana Msaada Kwako, anamsaada Kwa Mahawara Zake Na Familia Yake.

Fahamu Kuwa Hakuna Balozi Hata Mmoja Anayeweza Kutetea Mtanzania! Kama Yupo Aliyewah Mtaje Na Utaje Alimtetea Nani?

Suluhisho Wahamasishe Ndg,jamaa Na Marafiki Zako Wasirudie Makosa Uchaguzi Ujao Wa Rais Na Wabunge Hapo Tutakuwa Tumemg'oa Si Huyo Balozi Wako Bali Mpaka Na Majanga Mengine Walioteuliwa Kwa Kujuana Tutakuwa Tumewang'oa.

USIRUDIE MAKOSA MUNGU AMEKUSAMEHE DHAMBI ZAKO.
 
hahahaaaaa! ila mm huwa najiuliza, hawa mabalozi wanapewa job description kweli? ivi huwa wanaleta faida yenye mashiko au wanaenda kuuza sura tu nchi za watu?
 
Hujasema msaada gani.

Isije kuwa umempiga mzinga akakutolea nje unalalama.

Ndugu huwezi kutoka kwako uende ukaanze kuombaomba tena kwa waTz,sisi tuko na kazi zinazotufanya tuwe huku,kuna maswala ya kidiplomasia anatakiwa aahughulikie lakini yeye ni kiburi tu,ni wiki mbili tu zilizopita limetokea tatizo eneo la Brassimba Lubumbashi,alipewa taarifa lakini hakusaidia lolote.Inatuuma sana kuona mabalozi wa Zambia,Zimbabwe na wengine wanavyokua na ushirikiano wa raia wao,wakipewa taarifa mara moja wanatatua
 
BarakaJr;

Ni vyema kuweka haya wazi tangu mwanzo, iki watu wasiweze kuweka shaka kwamba lawama zako zimekaa kikazi zaidi na si masuala ya kupiga mzinga na kunyimwa hela.

Ukimuandikia balozi barua ya kumfahamisha matatizo kwa style hii ya habari nusunusu, siwezi kushangaa akikupotezea.
 
Last edited by a moderator:
BarakaJr;

Weka Wazi Nini Kilitokea?Na Uthibitisho Wa Taarifa Kupewa Na Yeye Alitakiwa Afanye Nini?Na Nini Ambacho Hakukifanya?
 
Last edited by a moderator:
Poleni watanzania wenzangu naelewa hisia zenu zenye uchungu kwa mtu ambaye hajawai kusafiri nje ya nchi au kupata tatizo akiwa nje hawezi kuelewa atawasanifu tu!

Mimi nina wasiwasi uwenda hawa mabalozi hawana JD hivyo uelewa wa upana wa majukumu yao ni tatizo pia.

JK tunakuomba ufagie na huko uwamlike mabalozi wasiowajibika warudi tu home uteue wawajibikaji wanaoelewa kazi ya ubalozi.
 
Weka Wazi Nini Kilitokea?Na Uthibitisho Wa Taarifa Kupewa Na Yeye Alitakiwa Afanye Nini?Na Nini Ambacho Hakukifanya?

Mm naona unacholeta hapa ni ubishani na kutaka kujua tu nini kimetokea,Ninapoandika lalamiko hili mm mwenyewe niko ndani ya DRC,na nimekuwepo ktk vikao vya kutafuta ufumbuzi wa hilo tatizo,na kwa bahati nzuri mengine yote ya mwaka juzi na mwaka jana pia nilikuwepo,Ila wewe kwa kua bado hujakumbana na kadhia kama tunazokumbana nazo ugenini,ndio maana unahoji kimizaha
 
Back
Top Bottom