Game Theory
Platinum Member
- Sep 5, 2006
- 8,545
- 835
Mimi naona tatizo hapa si bendera; bali ni je Tanzania imeishaitambua serikali ya waasi? Na je huyu balozi amewasilisha upya credentials zake kwa Rais kuwa ni mwakilishi wa Utawala mpya!? Kama bado Tanzania inamtambua kama mwakilishi wa Gaddafi hapo ndipo utata wa bendera unakuja.Mabadiliko ya bendera ya Libya yalishafanyika hata huko nyuma.Bendera wanayotumia waasi ndiyo iliyokuwa inatumika wakati wa utawala wa kifalme 1951--1969,Gaddafi alipompinduwa Mfalme Idris.1969--1977 bendera ya Libya ilikuwa na rangi nyekundu,nyeupe na nyeusi. 1977 hadi Gaddafi anajificha bendera ilikuwa ni ya kijani.Hivyo Membe kwa kuwa serikali ya Tanzania haijawatambua rasmi waasi ana haki ya kutoukubali uwakilishi wa waasi.
Good observation bro
the issue hapa ni sovereignty ambayo hawa jamaa wanaclaim wanayo ili hali according to International law hawana.
Nchi 41 Africa hawawatambui