Game Theory
Platinum Member
- Sep 5, 2006
- 8,545
- 835
mbona unamnyima haki yake ya msingi Mbopo ya kuchangia thread, kwann akae pembeni? wewe leta zako hoja nae aendelee kuleta zake kadiri anavofahamu na wengineo!
nothing wrong with that
mbona unamnyima haki yake ya msingi Mbopo ya kuchangia thread, kwann akae pembeni? wewe leta zako hoja nae aendelee kuleta zake kadiri anavofahamu na wengineo!
i like it when you say nonsense, halafu unaishia hapo.
Kwanini unataka kuhamisha mjadala kwenye legal bases na kukataa opinion za watu kwenye jambo hili?
Sioni unachochangia angalau Mbopo alikuwa analeta changamoto.nonesense
lete legal evidence kusupport argument yako
What kind of legal evidence do you want? i am not here for political purpose like you!
Je unaelewa maana ya mahusiano ya kidiplomasia?...Suppose membe angemuuliza balozi hii bendera ya utawala wa ghadafi si bendera ya libyani people kwa sasa je balozi angejibu nini??
Balozi wa nchi haletwi kumwakilisha Rais kwa sababu amemteua yeye kwa ajili ya ujomba wala ushemeji!!!....ila huletwa kuwawakilisha wananchi wa nchi husika....so whatch-out!!
Labda useme tuvunje uhusiano kwa sababu kumfukuza utakuwa huja solve kitu serikali ile ile ya NTC itamleta mwingine na bendera ileile sijui utamfukuza tena.Serikali imtimue huyu Balozi kilaza wa rebels asilete jeuri hapa manake Kuna utaratibu wa kufanya haya mambo wasiojua wanadhani bendera ni kama suruali unavua na kuvaaa tu!!! someni Viena Convetion muone what does the word National Symbol means ndio mje kuongea upupu hapa..wale ni Rebels na wamewekwa na NATO kwanza ningelikua mimi ni Rais ningewatimua mda mref na kamwe nisingewatambua!!! Africa Must stand tall against Colonialist from Europe and US..
Hivi hata UK , USA na france hao NTC wamerushisiwa ubadilisha bendera. ? Mi nadhanikuna taratibu zataiwa kufuatwa kabla ya hiyo bdenra haijabadilishwa.
Kama ni mwakilishi wa Gaddafi sawa bora aondoke maana hata anayemwakilisha ameshaondolewa lakini kama anawakilisha wananchi lazima aheshimiwe.Mimi naona tatizo hapa si bendera; bali ni je Tanzania imeishaitambua serikali ya waasi? Na je huyu balozi amewasilisha upya credentials zake kwa Rais kuwa ni mwakilishi wa Utawala mpya!? Kama bado Tanzania inamtambua kama mwakilishi wa Gaddafi hapo ndipo utata wa bendera unakuja.
Mabadiliko ya bendera ya Libya yalishafanyika hata huko nyuma.Bendera wanayotumia waasi ndiyo iliyokuwa inatumika wakati wa utawala wa kifalme 1951--1969,Gaddafi alipompinduwa Mfalme Idris.1969--1977 bendera ya Libya ilikuwa na rangi nyekundu,nyeupe na nyeusi. 1977 hadi Gaddafi anajificha bendera ilikuwa ni ya kijani.
Hivyo Membe kwa kuwa serikali ya Tanzania haijawatambua rasmi waasi ana haki ya kutoukubali uwakilishi wa waasi.
Cut Mbopo and Membe some slack
Hakuna critic wa Membe na Foreign anayeongoza humu JF kama mimi na kwenye hili niko naye through and through na kama kuna mtu anazo arguments why we should recognise these rebels then aje nazo lakini pia aje na citations za ku back up arguments zake
Mbopo hii niachie. wewe kaa pembeni hawa nitawajibu vilivyo
Balozi wa Libya hakuwa anamwakilisha Gaddafi, alikuwa anaiwakilisha nchi na watu wa Libya na utawala wao. Utawala wa Gaddafi umeporomoka na kuondolewa uhalali wake na kwa maoni ya Walibya ulipoteza uhalali ule pale ulipoamua kuwageuka na kuwashambulia; na japo wengine tunafikiria labda uligeuka baada ya waasi kuanza Benghazi ukweli ni kuwa kwenye mioyo ya baadhi ya wananchi wa Libya ulikuwa umepoteza uhalali wake muda mrefu sana.
Sasa watu wa Libya wapo, wananchi wa Libya wapo, na utawala mpya ulioongoza maasi upo na umekubaliwa kuwa ndio unajukumu la kutawala kama serikali ya mpito kuelekea utawala mpya.
Mkuu hebu tuambie ni kwa nini ubalozi wa Libya hauwezi kubadilisha bendera? Hebu tupe grounds. Labda wengine hatuzijui. Inawezekana zipo taratibu. Tufafanulie mkuu. Utakuwa umetusaidia sana.
Dude this is not a CHADEMA vs CCM episode....Membe amekosa kazi nyingine za maana za kufanya mpaka afuatilie aina ya bendera inayopeperushwa kwenye ubalozi wa Libya? Je huyo balozi akiamua kutopeperusha bendera yoyote hapa ofisini kwake itakuwa ni kosa?
Halafu wakati mwingine inabidi tu watu wakubali hali halisi ilivyo. Sasa serikali ya Tanzania isipoitambua serikali mpya ya Libya itapata faida gani? Kwanza sidhani kama hiyo serikali ya Libya inahitaji sana Tanzania. Mataifa makubwa na yenye nguvu za kiuchumi na kijeshi duniani tayari yameshaitambua hiyo serikali mpya ya Libya, what is Tanzania government? What Tanzania government can offer to the new Libya government?.
Ukiangalia serikali ambazo bado hazijaitambua hiyo serikali mpya ya Libya nazo zina matatizo. Mfano mzuri ni Zimbabwe, Mugabe matatizo yake yanajulikana. Kikwete naye alishaonyesha wasiwasi kuwa maandamano ya CHADEMA yana nia ya kumtoa madarakani kabla ya wakati.
Kwa hiyo sio jambo la kushangaa kusikia serikali yake inakataa kuitambua serikali mpya ya Libya iliongia kwa nguvu ya umma ambao hata hivyo ilibidi watumie silaha na kumwaga sana damu baada ya Gadaffi kuanza kuwashambulia kijeshi ili kulinda utawala wake, lakini hata hivyo umma umepambana naye vilivyo mpaka sasa amejificha kwenye mapango kama panya buku.