BALOZI MWAMBULUKUTU: Hospitalised Following Attack & Robbery in SA!

Ogah,
Mh Balozi, yeye ni security agenty kwa taaluma hivyo hiyo kozi ni ndogo saana kwake
 
Yes ni Kozi ndogo saana kwake na ndio maana.............unakumbushwa do not take things for granted............ni BIG mistake kudharau ethics za ki-uslama eti kwa kuwa ni kozi ndogo!!!.........hii imewa-cost sana wana usalama wengi..............Mkuu upo?
 
Hawa viongozi wetu wameshatufikisha mahali hatuwezi kuamini anything anymore, kila ubalozi wetu una mtu wa usalama, moja ya kazi zake ni usalama wa ubalozi wetu na maofisa wake, ni wajibu wake kuhakikisha kuwa information za party ya ubalozi haifiki kwa wasiohusika, sasa hapa ilifikaje kwa majambazi?

Katika mazingara ya kimaisha huko South Afrika sasa hivi yeye na HOC wa ubalozi wetu huko walitakiwa kuwa extra careful na hata kuomba ulinzi zaidi kutoka kwa Wizara ya nje ya huko, au wao wenyewe kama ubalozi kuwakodi walinzi wa private kwa bill ya ubalozi, kwa nini hawakufanya hivyo? Je huyo balozi wetu huko is he clean? maana najua kuwa alipelekwa huko na Mkapa, kwa sababu maalum nayo ni kulinda masilahi flani, ambayo yalianzishawa na Mpungwe, sasa kwa mantiki hiyo je is he clean mpaka tushangae haya mazingaombwe?

Wa-Tanzania, tufike mahali tuwaambie hawa viongozi wetu kuwa tumechoka na mzingaombwe haya, hakuna wa kumuamini anymore, wote wamebakia kuwa kichekesho ndio maana hata habari zao sasa ni kichekekesho kitupu, iliyobaki wajiunge na Ze Comedy tu yaishe!
 
FMES

Mkuu wewe unafahamu hakuna hata moja anayejali usalama wa Tanzania wala wa balozi, yote hiyo ni danganya toto. Inabidi tuanze sasa kuweka wafanyakazi ambao wanaweza kufanya kazi zao kwa ufasaha na maswali magumu kuulizwa kasheshe kama hizi zinapotokea.

Ukipewa list ya wafanyakazi wa ubalozi SA na taaluma zao utacheka tu. WE NEED TO BE MORE SERIOUS ON INTERNATIONAL LEVEL.
 
...................................Katika mazingara ya kimaisha huko South Afrika sasa hivi yeye na HOC wa ubalozi wetu huko walitakiwa kuwa extra careful na hata kuomba ulinzi zaidi kutoka kwa Wizara ya nje ya huko, au wao wenyewe kama ubalozi kuwakodi walinzi wa private kwa bill ya ubalozi, kwa nini hawakufanya hivyo? .......................

well said FMES........this is what among other things im trying to explain here.............nahisi kuna mambo yalifanyika kienyeji enyeji hivi..........its too hard to believe this........!!!
 
Ni wajibu wangu kama mTanzania, kuwapa pole wananchi wenzangu kwa haya maovu waliyotendewa.

Having said that, I am perplexed by some of the issues concerning our national representation abroad raised by contributors to this discussion.

Ukiniuliza nikutajie faida za balozi zetu nchi za nje......I'll be hard pressed to list a few .....seriously, I don't know; and I consider myself to be a reasonably enlightened person.

Can someone give us some concrete examples of some beneficial outcomes we have gained as a nation as a result of our representation through our embassies?

Otherwise, mimi pamoja na wengine wengi tutaendelea kuamini kuwa pesa yetu ya kodi tunayowalipa hawa watu, ni kwa manufaa yao binafsi na wala sio kwa manufaa ya taifa.

Balozi zote inafaa zifungwe, watu warudi nyumbani tusaidiane kwenye kilimo cha kufa na kupona.


Seems to be an extreme stand, but that is how I feel about our embassies abroad.
 
South Africa kuna mambo kweli; ndiyo Zuma anahamsisha watu kwa kusema "Give My My Machine GUN"
 
napenda kuwapa pole wote waliopatwa na zanga hili.

nadhani kimsingi ubalozi unatakiwa kuwa jicho na sikio la nchi yake. jicho na sikio hili ni katika nyanja mbalimbali zikiwemo za uchumi, usalama, utamaduni, kijamii nk. katika hali hii ubalozi unatakiwa kuwa wa kwanza kuona/kusikia nafasi (opportunity), tishio nk vinavyoweza kunufaisha au kutishia nchi yake. sasa kama haya yanatekelezwa kwa ufanisi ni suala lingine. hata hivyo inawezekana baadhi ya matunda ya kazi za balozi zetu sio "tangible" hivyo ni vigumu kuyapima na mengine yanapimika kirahisi.

balozi zetu nyingi hazina ulinzi na hili nadhani ni tatizo la kisera (yaani serikali halitilii swala hili mkazo) nadhani hili si tatizo kwa tanzania tuu bali nchi nyingi. naamini wengi wetu tunakumbuka kwamba wamerikani iliwachukua mabomu ya dar na nairobi ili kupitia kwa makini sera zao za ulinzi katika balozi zao.

tuchukua tukio hili kama kengele ya uamsho kwa serikali yetu kuhusu hali ya kiusalama katika balozi zetu
 
Quote:-

"balozi zetu nyingi hazina ulinzi na hili nadhani ni tatizo la kisera (yaani serikali halitilii swala hili mkazo) nadhani hili si tatizo kwa tanzania tuu bali nchi nyingi. naamini wengi wetu tunakumbuka kwamba wamerikani iliwachukua mabomu ya dar na nairobi ili kupitia kwa makini sera zao za ulinzi katika balozi zao."

Mkuu Kafara,

Kupigwa bomu nje ya ofisi sio sawa na majambazi kuingia ndani ya jengo, wa-Marekani, hata hizo enzi usingeweza kuingia ndani ya jengo lao ndio maana jamaa wakatega bomu tu nje ya jengo, na ni something wanaweza hata leo kurudia tena, yaani kutega bomu nje ya jengo la ubalozi wa US bongo, isipokuwa one thing is for sure hakuna anayeweza kuingia ndani ya ubalozi wao, kuanzia zamani mpaka sasa,

Mkuu in the wake of September 11, hakuna nchi duniani inayokaaa tu kama wajinga kuhusiana na usalama wao na wa majengo yao, tena kwa nchi kubwa na inayojulikana kwa ujambazi kama SA, unawezaje kufanya mambo kienyeji namna hii? Ina maana hata rais wetu anweza kwenda huko akakutwa na haya?

Ukweli ni kwamba lazima kuwepo na uwajibikaji hapa, either balozi ndiye anyehusika au HOC, au mtu wa idara, lazima kichwa cha mmojawapo ki-roll, kwenye mahujaji tatizo limetafutwa haraka na hata solution za haraka haraka kwamba mwenyekiti wa bodi ya ATC aondolewe, sasa kwa nini huku kwenye ubalozi isitumike njia ile ile ya mahujaji?

Ndio maana nilisema majuzi kuwa tabia iliyotumika kutafuta tatizo na solution, kwenye mahujaji itumike kwenye kila ishu sio kuishia mahujaji tu! Kilichotokea hapa kwenye uablozi wetu SA, ni uzembe tu wa maofisa wetu huko, FULL STOP!
 
mkuu fmes,

inawezekana kabisa kwamba kuna uzembe umefanyika na maofisa wa ubalozini. lakini pia inabidi tuliangalie hili kwa mapana yake. mfano jee ubalozi umewahi kuomba fungu kwa ajili ya kuimarisha ulinzi? nini sera ya serikali kuhusu ulinzi katika balozi zake?

sasa kama uzembe umefanyika hq basi vichwa vianze kuzunguka huko.

baada ya mabomu ya dar na nairobi wamarekani wamebadilisha kabisa mfumo wa ulinzi katika balozi zao na kuna nchi ambazo wamebidi wabadili hata majengo ili kukidhi mahitaji ya ulinzi wao.

naamini baada ya tukio hili serikali (wizara ya mambo ya nje) na balozi zetu zitakuwa makini zaidi katika masuala ya ulinzi.
 
kumbe uhalifu umetokea nyumbani kwa mtanzania na sio nyumbani kwa balozi wala ubalozini


Balozi mahututi

2007-12-30 09:38:12
Na Dunstan Bahai


Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Bw. Emmanuel Mwambulukutu, amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi nchini humo baada ya kuvamiwa na majambazi na kushambuliwa vibaya usiku wa kuamkia jana akiwa kwenye tafrija ya kuagwa.

Balozi Mwambulukutu amelazwa katika hospitali ya Pretoria East akiwa chini ya uangalizi mkubwa wa madaktari huku akisaidiwa kupumua kwa mashine.

Akizungumza na Nipashe jana kwa simu kutoka Afrika Kusini, Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo, Bw. Felix Mujarubi alisema, madaktari walisema kuwa Balozi Mwambulukutu alipigwa na kitu kizito kichwani hali iliyosababisha damu kuvuja kwenye ubongo.

``Madaktari wamesema kutokana na hali hiyo, hawawezi kumruhusu leo (jana) wala kesho (leo). Yuko kwenye uangalizi wa karibu sana wa madaktari,`` alisema Bw. Mujarubi.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Utawala, Balozi Mwambulukutu ambaye amemaliza muda wake, akiwa na familia yake walialikwa nyumbani kwa Mtanzania mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Dk. Mrosi anayeishi Afrika Kusini kwa ajili ya tafrija ya kumuaga.

``Wakiwa nyumbani kwa Mtanzania huyo, watu wazima walikaa nje na watoto walikaa ndani, mara majambazi manne yalivamia na kuwaamuru watu wazima waliokuwa wamekaa nje akiwamo Balozi, kuingia ndani.

``Wakati wote huo majambazi walikuwa wakiwashambulia kwa makofi na vitu vingine huku wakiwanyang`anya mali zao walifanikiwa pia kuondoka na gari aina ya Benzi la Balozi lakini lilipatikana jana ikiwa imetelekezwa na jambazi mmoja amekamatwa.

Jambazi alishambuliwa na watu wenye hasira na amelazwa hospitalini akiwa chini ya ulinzi,`` alisema Bw. Mujarubi.

Watu wengine ambao walijeruhiwa kidogo ni mke wa Balozi Mwambulukutu na Dk. Mrosi ambao walitibiwa na kuruhusiwa.

Awali Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Seif Ali Idd, aliliambia gazeti hili kuwa, majambazi hayo yalivamia kwenye tafrija hiyo na kuwashambulia waalikwa wote akiwemo Balozi.

Alisema hali ya Balozi Mwambulukutu si mbaya kwani alipata misukosuko kidogo tu ingawa amelazwa katika hospitali hiyo kwa matibabu ya majeraha madogo aliyopata sikioni
Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo, lengo la majambazi hayo lilikuwa kupora gari la Balozi.

SOURCE: Nipashe

http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2007/12/30/105288.html
 
huwa nasoma maoni yako mengi na huwa naona unatoa maoni yaliyo na umakini. Lakini haya maoni uliyoandika hapo chini (nina amini ni wewe) nafikiri yana walakini mkubwa. Ni wazi kuwa Afrika Kusini kuna tatizo la ujambazi wa hali ya juu, na imeelezewa hata kwenye hii taarifa, ikiwemo mabalozi (hata wa UN) na maafisa wa serikali waliozamiwa makwao, jeh na kwa hao nao kuna mazingira ya kutatanisha pia? Jeh Lucky Dube naye na wengine wengi? Hao jamaa wa huko hawaogopi cha balozi wala nani, sitashangaa nikisia hata raisi siku wamejaribu kumuibia au kumpora.

Ni wazi kuwa Afrika Kusini kuna matukio mengi tu ya bila kujali nyadhifa ya mtu. Kwa hiyo nafikiri kama tukio kama hili lingetokea Tanzania, maoni yako yangekuwa yana ukweli lakini kwa Afrika Kusini, ni ngumu kuanza kutilia mashaka wakati hii ni kawaida ya huko.
 
Balozi apigwa risasi Afrika Kusini

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima

BALOZI wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Emmanuel Mwambulukutu amejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa na kushambuliwa kwa risasi na majambazi waliovamia makazi ya Dk. Mlosi mahali ilipokuwa ikifanyika sherehe ya kumuaga, katika Jiji la Pretoria.
Sambamba na balozi Mwambulukutu, mke wake, na Watanzania wengine kadhaa waliohudhuria sherehe hizo, pia walipigwa na kujeruhiwa vibaya na majambazi hayo.

Taarifa zilizopatikana kutoka Pretoria nchini Afrika Kusini, zilieleza kuwa mke wa balozi Mwambulukutu alipigwa na kuchanika katika paji la uso kwa kitako cha bastola, wakati akijaribu kumukoa mumewe aliyekuwa anaopambana na majambazi hayo.

Habari zilieleza kuwa balozi Mwambulukutu alijikuta uso kwa uso na majambazi hao wakati walipokuwa wanamlazimisha awapatie funguo za gari lake.

Hata hivyo, Ofisa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje, Assah Mwambene, alilihakikishia gazeti hili kuwa hali ya balozi Mwambulukutu inaendelea vizuri ingawa hadi jana mchana alikuwa bado yupo hospitali.

"Hatuwezi kutaja jina la hospitali aliyolazwa hivi sasa kutokana na sababu za kiusalama, lakini hali yake inaendelea vizuri ingawa mkewe amepata mshituko kutokana na tukio hilo," alisema Mwambene.

Alisema kuwa kundi la Watanzania walikuwa katika hafla hiyo iliyoandaliwa mahsusi kwa ajili ya kumuaga balozi Mwambulukutu ambaye amemaliza muda wake.

Inaelezwa kuwa Mwambulukutu alivamiwa juzi usiku na majambazi wakati akila chakula cha usiku pamoja na Watanzania wengine wapatao 25 katika makazi ya Dk. Mlosi yaliyoko Garsfontein, jijini Pretoria.

Majambazi hao wapatao watano, wakiwa na bastora, waliruka ukuta na kuingia ndani ya makazi ya Dk. Mlosi na kuwaamuaru watu kulala chini.

Habari zilieleza kuwa majambazi hao waliwapora simu za mkononi, fedha pamoja na vifaa vingine vya ndani, ikiwamo kompyuta.

Baada ya uporaji huo, majambazi hao walitaka kupora gari aina ya Audi lililokuwa limeegeshwa mbele ya Mercedes Benz la Balozi Mwambulukutu, hivyo walimtaka balozi atoe funguo ili gari lake lisogezwe pembeni.

Kwa kuhofia gari lake kuibiwa, Balozi Mwambulukutu alikataa kutoa funguo za gari, kitendo kilichowaudhi majambazi na kuanza kumshambulia kabla hayajampiga risasi.

Habari zilieleza zaidi kwamba mke wa balozi baada ya kuona mumewe ameumizwa vibaya, aliyakabili majambazi hayo ili kumuokoa, hata hivyo, alipigwa na kitako cha bastola katika paji lake la uso na kupoteza fahamu.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya Afrika Kusini, balozi na mkewe pamoja na watu wengine sita walikimbizwa hospitalini ambako wanaendelea kupatiwa matibabu.

Katika shambulio hilo baadhi ya Watanzania walijeruhiwa baada kupigwa na chupa za vinywaji zilizokuwa mahali hapo wakati majambazi hayo yakiwatisha ili watoe vitu walivyokuwa navyo.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa wakati majambazi hao walichukua mali walizoiba na kuzipakia katika gari la Balozi Mwambulukutu kabla ya kutoweka askari waliwasili eneo hilo dakika 25 baadaye baada ya kupigiwa simu.

Polisi wa Afrika Kusini jana walimkamata mtu mmoja akidhaniwa kuhusika na tukio hilo. Mtu huyo, alipambana na polisi katika eneo la Mamelodi Magharibi na kupigwa risasi na hivi sasa amelazwa. Aidha ripoti nyingine zinaeleza kuwa gari la Balozi Mwambulukutu limepatikana.
 
Ukipewa list ya wafanyakazi wa ubalozi SA na taaluma zao utacheka tu. WE NEED TO BE MORE SERIOUS ON INTERNATIONAL LEVEL.

Dua sio South Africa peke yake ni sehemu nyingi. Kuna ambao nimewahi kuwauliza kuwa sera yatu ya mambo ya nje kiufupi inasema nini, walishindwa kujibu walikuwa wanajikanyaga tu. Wakati mwingine hata mission zetu zinakuwa haizna objectives ni kama tu ofisi za kutoa visa na kupokea viongozi wa Tanzania wakienda kutembelea kwenye nchi hizo, unaweza kucheka sana. They are less useful, nyingi hazina mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi. Inasikitisha sana.
Jaribu kuuliza hata leo kazi za balozi zetu ni nini, uulize wenyewe maofisa wa ubalozi utacheka.
 
Mwambulukutu apumua kwa mashine

na Happiness Katabazi
Tanzania Daima

HALI ya Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Emmanuel Mwambulukutu, aliyelazwa katika hospitali moja jijini Pretoria akiuguza majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa na majambazi, inaelezwa kuwa bado ni mbaya.
Habari zilizopatikana jana zinaeleza kuwa balozi huyo bado hajapata fahamu na sasa anapumua kwa msaada wa mashine.

Hata hivyo, mmoja wa madaktari katika Hospitali ya Pretoria East, Dk. Linda Ezekiel, alikaririwa akisema kuwa Mwambulukutu hakuwa katika hali ya hatari.

"Amepata majeraha ya ndani na alikuwa akivuja damu ndani. Hata hivyo, uvujaji wa damu umepungua. Tunatarajia atapata fahamu katika siku chache zijazo na hapo ndipo tutakapoweza kufahamu kiwango cha majeraha aliyoyapata," alisema.

Habari nyingine zilieleza kuwa mke wa Balozi Mwambulukutu, ambaye naye alijeruhiwa katika shambulio hilo, amepata nafuu.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana mchana, Ofisa wa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Assah Mwambene, alisema kutozinduka kwa Mwambulukutu kunatokana na kuchomwa sindano za usingizi ili aweze kupatiwa matibabu.

Mwambene alisema juzi Balozi Mwambulukutu alifanyiwa kipimo cha 'Scaner' kichwani na matokeo ya kipimo hicho yanaonyesha kuwa ubongo wake haujaathirika.

"Nimetoka kuzungumza na Mkuu wa Utawala wa ubalozi wetu nchini Afrika Kusini, Alex Mwijarubi, ambaye amenieleza kuwa kutozinduka kwake hakutokani na majeraha, bali sindano za usingizi," alisisitiza.

Balozi Mwambulukutu bado amelazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi (ICU).

Watanzania wengine pia walijeruhiwa baada ya kuvamiwa na majambazi wapatao wanne mwishoni mwa wiki, wakati walipokuwa katika hafla ya kumuaga balozi huyo, anayekaribia kurejea nchini, baada ya kumaliza muda wake wa kazi.

Inadaiwa kuwa majambazi hao waliwafunga kamba watu waliokuwa katika hafla hiyo na kuwapora vitu vya thamani zikiwemo simu za mkononi na vifaa vya ndani, na wakati wanaondoka walianza kubishana na Balozi Mwambulukutu wakimtaka awapatie funguo za gari lake aina ya Mercedes Benz.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya Afrika Kusini, balozi na mkewe pamoja na watu wengine sita walijeruhiwa katika uvamizi huo na walikimbizwa hospitalini ambako wengine walitibiwa na kuruhusiwa.

Msemaji wa jeshi la Polisi, Dennis Adriao, alikaririwa akisema kuwa mtu mmoja alikwisha kukamatwa Jumamosi asubuhi kuhusiana na tukio hilo.

Mtu huyo alipigwa risasi katika harakati za kumkamata, na hivi sasa amelazwa hospitali chini ya ulinzi mkali wa polisi. Anatarajiwa kufikishwa mahakamani atakaporuhusiwa kutoka hospitali.




 
  • Thanks
Reactions: cds
DAR ES SALAAM.

RAIS Thabo Mbeki wa Afrika Kusini juzi (Jumatano, Januari 2, 2008) alimtembelea hospitali na kumjulia hali Balozi wa Tanzania nchini humo, Emmanuel Mwambulukutu.

Balozi Mwambulukutu alilazwa hospitalini mjini Pretoria/Tshwane wiki iliyopita baada ya kuwa amevamiwa na kuumizwa na majambazi.

Kabla ya kumtembelea Balozi, Rais Mbeki alimpigia simu na kuzungumza na Rais Jakaya Kikwete, akimwelezea masikitiko yake juu ya tukio hilo la kuumizwa kwa Balozi Mwambulukutu.

Rais Mbeki pia alimweleza Rais kuwa hadi juzi hiyo, mmoja kati ya watu wanaosadikiwa kumshambulia Balozi Mwambulukutu, alikuwa tayari amekamatwa na polisi.

Rais Mbeki alimweleza Rais kuwa majambazi wengine watano bado wanatafutwa kuhusiana na tukio hilo . Aliahidi kuwa Polisi wa nchi yake watafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa wote wanapatikana na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Balozi Mwambulukutu aliumizwa wiki iliyopita wakati watu wasiojulikana walipovamia nyumba ambako balozi huyo alikuwa anafanyiwa hafla ya kumwaga, na wakajaribu kuiba gari.

Balozi Mwambulukutu anatarajiwa kurejea nyumbani karibuni baada ya kuwa amemaliza muda wake wa utumishi wa ubalozi wa Tanzania katika Afrika Kusini.

4 January,2008
 
Back
Top Bottom