Hivi JK asipomrudisha Ballali nini kitatokea? Naona sasa anapima upepo
tu kujua kama asuke au anyoe.
Siamini kabisa JK anataka kumshughulikia Ballali maana inaelekea uchafu wa BOT umeishia mlangoni kwake.
Hivi Watanzania pamoja na kujua kote tunaibiwa, tumeendelea kukaa kimya na mwaka 2010 tutamchagua JK na mawaziri wake kwa kishindo?
Tukiruhusu wakaguzi wapitie kila wizara kwenye awamu ya Mkapa, naona tutagundua hatuhitaji misaada wala kukopa. Tunaweza kutandaza reli ya kisasa nchi nzima.
Taarifa hizo zilidai zaidi kwamba, Dk. Ballali aliukana uraia wa Tanzania na kuchukua uraia wa Marekani wakati akifanya kazi katika moja ya mashirika makubwa ya kimataifa nchini humo.
Ukweli ni kwamba serikali haimtaki Balali arudi. Siku za karibuni mama yake na kaka zake wamekuwa wakiandamwa na UWT pale Bongo wakitaka wampelekee ujumbe akae kimya. Wanasema kama atazungumza basi si serikali tu ya sasa itakayoyumbishwa, lakini wote Mkapa na Mwinyi watakuwa hatiani. Nasikia Mwungana ameshapanga plan B.
And that is the sad story of our land. We as a people are totally resigned to the fact that there is nothing we can do?
Hivi anayesema haya ana akili kweli au ndio hao ambao wanadai kudaanganywa na Babali. Hivi mtu akiwa raia wa nchi fulani je anahitaji visa kuingia nchi ambayo kwayo ana uraia. Kama Balali aliukukana utanzania na akawa raia wa marekanai itakuwaje balozi wa marekani aseme visa yake imefutwa. Na kwa mantiki hiyo Balali alikuwa Gavana akiwa raia wa marekani.. give me a break!
[/SIZE]
JK hawezi kutoa hiyo amri kwa sababu anafahamu fika tukifika hapo hata yeye hayuko salama kwani madhambi yake yanajulikana na uncle Ben.
Balali haogopi kurudi Tanzania lakini mafisadi ndio hawataki arudi. This is a fact, jamani. Imefikia hatua ya kutumia vitisho asirudi.
Hivi kwa nini Tanzania mtu ukizungumzia haki unapewa label ya MPINZANI, Ukizungumzia rushwa - MPINZANI, Ukizungumzia ubadhirifu wa rasilimali za nchi - MPINZANI. Je hii ina maana kuwa kutopenda kutenda haki na kutozungumzia maouvu ndilo linatakiwa otherwise wewe ni MPINZANI. Au unakuwa MPINZANI kwa vile unapinga uovu, au kwa vile unazuia watu kula!
Mzalendohalisi,
Uliwahi kumwona Balali na vimada wapi?
Just asking.
Balali pesa BoT alikuwa anatumbua na vimada Dar hadi akaugua.. sasa aliwasahau ndugu zake wanateseka kule Mufindi ktk mashamba ya chai!
Rwabugiri,
Hizo habari za ngoma nimezisikia hapa JF. Kwa kadri nijuavyo mimi, na nimeshamwona Balali, shida yake si ngoma hata siku moja. Na kuhusu ndugu zake ni kweli Balali hajajenga Iringa, but then nasikia wasomi wengi kutoka huko hawajengi kwao, lawama ambazo na sisi baadhi tunaotoka Mara tumekuwa nazo. Wote tunapenda kujenga Dar.
Kuhusu Balali kuwa mlaji wa starehe na kusahau ndugu zake, ninaelekea kushtushwa kidogo has kwa vile huyu Ballali anajulikana kuwa alikwenda kufunga harusi Ufaransa kwa gharama kubwa sana vile.