Ballali aitikisa serikali

Jamani Wakubwa Samaanini Kidogo,naombeni Niwatoeni Nje Ya Mada Kwa Kuuliza Jambo Fulani, Hivi Mrithi Wa Mama Yetu Salome Mbatia Ameshateuliwa ? Mana Ni Muda Mrefu Toka Katutoka Na Mimi Binafsi Sijasikia Lolote So Nikaona Niulize Labda Nilipitwa

Samahanini
 
Hivi JK asipomrudisha Ballali nini kitatokea? Naona sasa anapima upepo
tu kujua kama asuke au anyoe.

Siamini kabisa JK anataka kumshughulikia Ballali maana inaelekea uchafu wa BOT umeishia mlangoni kwake.

Hivi Watanzania pamoja na kujua kote tunaibiwa, tumeendelea kukaa kimya na mwaka 2010 tutamchagua JK na mawaziri wake kwa kishindo?

Tukiruhusu wakaguzi wapitie kila wizara kwenye awamu ya Mkapa, naona tutagundua hatuhitaji misaada wala kukopa. Tunaweza kutandaza reli ya kisasa nchi nzima.


Inabidi kwanza tuhamasishe wananchi waanze kubadilisha kuanzia hizi chaguzi fupifupi. Tuwaombe wapiga kura wa Kiteto watuanzishie safari ya mabadiliko.
 
Balali...Balali.

The best he can do now is hide. Hao wanafamilia wanaomtaka ajisafishe hawaelewi madudu yake, na hawaelewi hivi karibuni atafilisiwa.

Nachoweza kusema alikosea sana sana kuwapa Deloitte kazi ya kumchunguza akidhani anaweza kuficha uozo wake. Ilipofika siku anaona Deloitte wanataka kumexpose akawafire. Angekuwa msafi angeweza kuwashtaki Deloitte for Breach of Confidentiality Clause, lakini alijua ananuka mavi.

Tamaa ya Fisi...
 
Taarifa hizo zilidai zaidi kwamba, Dk. Ballali aliukana uraia wa Tanzania na kuchukua uraia wa Marekani wakati akifanya kazi katika moja ya mashirika makubwa ya kimataifa nchini humo.

Hivi anayesema haya ana akili kweli au ndio hao ambao wanadai kudaanganywa na Babali. Hivi mtu akiwa raia wa nchi fulani je anahitaji visa kuingia nchi ambayo kwayo ana uraia. Kama Balali aliukukana utanzania na akawa raia wa marekanai itakuwaje balozi wa marekani aseme visa yake imefutwa. Na kwa mantiki hiyo Balali alikuwa Gavana akiwa raia wa marekani.. give me a break!

Ukweli ni kwamba serikali haimtaki Balali arudi. Siku za karibuni mama yake na kaka zake wamekuwa wakiandamwa na UWT pale Bongo wakitaka wampelekee ujumbe akae kimya. Wanasema kama atazungumza basi si serikali tu ya sasa itakayoyumbishwa, lakini wote Mkapa na Mwinyi watakuwa hatiani. Nasikia Mwungana ameshapanga plan B.

Now you are talking my brother. Yote yanayotendeka hapa ni execution ya PLAN B, then C hadi Z kama kutakuwa na umuhimu.


And that is the sad story of our land. We as a people are totally resigned to the fact that there is nothing we can do?

Yes I totally agree with you, BUT don't forget there is the next level of which the government will die trying to suppress i.e. People's Revolution, as unknowingly they spent years indoctrinating the masses, they trained the militia ( mgambo), and they even changed their party's name from TANU ( Tanganyika African National Union) to CCM "The Revolutionary Party" - walikuwa wanajichulia bila kujuwa. They just think it is a child play. If this trend goes on at this rate, we are going to kill each other like our neighours. Kwani Kenya wnauana kwa ajil ya kura au ukabila, hizo ni sababu za kuficha ufisadi ulikithiri hadi viongozi wanafikia hali ya kuamini kuwa waliumbwa waongoze, and they will cling to power at any cost. Kwani huyo Kibaki wakati wanamwondoa Moi aliwahamasisha Kenyan's makabila yote, na sasa anaipata joto ya jiwe toka kwa wale aliowahamasisha miaka mitano iliyopita. Wewe ukimsikia Speaker wa bunge tena mwanasheria, anaelezwa kanuni za bunge lake zinnavyoseam, anakurupuka na anajibu kuwa hizo ni hoja za kitoto, ujue kuwa there is something very wrong with the system and I can bet my neck that IT CAN'T GO ON FOREVER. There is a time coming and it could be sooner than you and me anticipate that these leader will be held accountable by those who have put the in power.

Hivi kwa nini Tanzania mtu ukizungumzia haki unapewa label ya MPINZANI, Ukizungumzia rushwa - MPINZANI, Ukizungumzia ubadhirifu wa rasilimali za nchi - MPINZANI. Je hii ina maana kuwa kutopenda kutenda haki na kutozungumzia maouvu ndilo linatakiwa otherwise wewe ni MPINZANI. Au unakuwa MPINZANI kwa vile unapinga uovu, au kwa vile unazuia watu kula!

Kitu ambacho serikali ya CCM lazima ielewe ni kuwa kila chenye mwanzo kina mwisho, na pia uovu haulipi, na za mwizi ni arobaini. These are facts of life ila wao naona hawaamini hayo kabisa, na wale wanowaambia ukweli wanaitwa wachochezi na watu wasiopenda amani (Tanzania kisiwa cha amamni). Hivi nauliza kuibiwa na kunyamaza ndiyo amani? Na wakiiba vyote si inabidi na wewe uanze kudai urudishiwe ulivyo ibiwa, je hapo kutakuwa na amami tena? Hawa jamaa hawasomi dalili, na wanaamini kabisa kuwa watanzania ni mabwege daima.

If our president does not cease this opportunity and distance himself from the existing corrupt system, of which I will forgive him of his past, as he will have at least taken the fist step, he will be a hero for just admitting his wrongs; then he should totally clean house without any exceptions ( including taking back from Mkapa).
 
Hivi anayesema haya ana akili kweli au ndio hao ambao wanadai kudaanganywa na Babali. Hivi mtu akiwa raia wa nchi fulani je anahitaji visa kuingia nchi ambayo kwayo ana uraia. Kama Balali aliukukana utanzania na akawa raia wa marekanai itakuwaje balozi wa marekani aseme visa yake imefutwa. Na kwa mantiki hiyo Balali alikuwa Gavana akiwa raia wa marekani.. give me a break!

[/SIZE]

Mzalendohalisi,

Hicho kitu kinawezekana, Ballali alirudi TZ kama Mtanzania, akaendelea kutumia gamba la Tanzania kwenye safari zake. Kwasababu TZ hairuhusu
uraia wa nchi mbili, yeye akaendelea kutumia gamba la TZ kwa kila kitu, balozi zenyewe hizo usipowaambia wala hata hawawezi kujua wewe ni raia wao
na kwasababu yeye ni gavana wala hawahitaji hata ku check kabla ya kumpa visa.

Jiulize kama Ballali kanyang'anywa visa amewezaje kuendelea kuishi USA?

Nina wasiwasi sana kwamba huenda Ballali ana uraia pia wa USA.

Siku hizi kuna watu wengi tu wana magamba ya nchi zaidi ya moja lakini wakiwa TZ wanatumia gamba la TZ kwa kila kitu.
 
Mfano mzuri ni Amir Jamal aliyekuwa Waziri wa Fedha wa Serikali ya Kwanza huku akiwa Raia wa Canada. Na alipofariki akazikwa kwenye nchi yake ya CANADA. Hivyo sisemi kuwa Ballali ni Raia wa Marekani ila sitashangaa ikithibitika kweli ni raia wa Marekani.
 
JK hawezi kutoa hiyo amri kwa sababu anafahamu fika tukifika hapo hata yeye hayuko salama kwani madhambi yake yanajulikana na uncle Ben.

Basi ajiuzulu ili tufanye uchaguzi mpya wa kupata serikali itakayoweza kuwajibika katika utendaji wake na siyo hii SIRI KALI iliyooza kwa ufisadi kuanzia juu hadi chini.
 
Balali hana uraia wa Marekani. Hili nilishalisema awali. Ila ana residency permit ambayo inaweza tu kuondolewa na immigration department na wala si ubalozi wa Marekani DSM. Walichofanya pale Dar ni ku-revoke visa yake aliyosafiria kwa kutumia paspoti ya Kitanzania. Lakini hawajaondoa residency permit yake. Lakini shida ni nini? Balali haogopi kurudi Tanzania lakini mafisadi ndio hawataki arudi. This is a fact, jamani. Imefikia hatua ya kutumia vitisho asirudi.
 
Balali haogopi kurudi Tanzania lakini mafisadi ndio hawataki arudi. This is a fact, jamani. Imefikia hatua ya kutumia vitisho asirudi.


Mkuu Jasusi,

Heshima mbele, sasa hiii inaanza kuwa Ze-Comedy, wanaogopa nini? Basi asemee huko huko aliko, ukweli hauhitaji kusemewa nyumbani, after all so far ni mchezo wa kwenye public opinion, ambayo so far bado anaongoza against mafisadi kwenye polls, sasa aseme tu hata huko aliko, maana ya kumtishia asirudi hiyo sasa ni serious kama ni kweli, sisi wananchi tunaomba asemee huko huko inatosha the rest atuachie wananchi, yeye aseme tu huko aliko!

Tuwekeeni ka-telegram tu kakumtishia sirudi hapa, tule nao sahani moja hapa!
 

Hivi kwa nini Tanzania mtu ukizungumzia haki unapewa label ya MPINZANI, Ukizungumzia rushwa - MPINZANI, Ukizungumzia ubadhirifu wa rasilimali za nchi - MPINZANI. Je hii ina maana kuwa kutopenda kutenda haki na kutozungumzia maouvu ndilo linatakiwa otherwise wewe ni MPINZANI. Au unakuwa MPINZANI kwa vile unapinga uovu, au kwa vile unazuia watu kula!



Zalendo
Ni kweli kabisa, mtikila alipokuwa anasema saa ya ukombozi ni sasa na kusema wahindi wanatuibia na wanatumika kutuibia watu walimuona mwehu. Kama ulivyosema ukizungumzia rushwa unaonekana hayawani, sasa hivi mambo yako peupe pee, na hapa bongo watu wanaona jinsi gap between rich and poor inavyokuwa kubwa, watu wanatembelea convertibles na wengine hata viatu hawana.
Majambazi walioiba Benki nyingine walikamatwa na sasa wanasota kule Moshi, na wengine waliojaribu kuiba waliuawa, lakini waliobia BOT wanatesa na watendelea kutesa, inauma sana mzee bongo tunaonekana wajinga kabisa, tuko kama vipofu vile!
 
Ndugu wa Balali walia

Na Francis Godwin, Mufindi (Majira)

NDUGU wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Daudi Balali, wameeleza kushangazwa na tuhuma anazoelekezewa ndugu yao huyo.

Akizungumza na gazeti hili kijijini alikozaliwa Gavana huyo cha Luganga, Mufindi, mkoani Iringa, mdogo wake, Bw. Paschal Balali (48), alisema wameshangazwa, kwani wanaamini hakuna mtu mwadilifu kama alivyo kaka yao.

Bw. Paschal alisema ni vyema Watanzania wakaamini kuwa kuondoka kwa Dkt. Balali kwenda Marekani kutibiwa, si kwamba alikimbia tuhuma hizo.

Alisema kabla tuhuma hizo hazijaanza kumkabili, Dkt. Balali alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya kupooza mkono.

Aliongeza kuwa kutokana na wanavyomfahamu ndugu yao huyo, ni mtu mwadilifu asiyependa kujilimbikizia mali kama walivyo viongozi wengine.

"Pamoja na kuwa katika nafasi nzuri, ndugu yetu hawajaweza kunufaika na nafasi hiyo kutokana na jinsi alivyokuwa na uadilifu wa kulitumikia Taifa," alisema.

Bw. Paschal alisema yeye ni mtoto wa nane katika familia ya marehemu Mzee Balali ila hadi leo tangu ndugu yao huyo apate ugavana hajaitumia nafasi hiyo kunufaisha ndugu zake kutokana na "alivyokuwa mwoga wa kuchukua hata shilingi moja kwa ajili ya kuwapa ndugu zake".

Hata hivyo, alisema mbali na ndugu kwa sasa kuwa katika mawazo mazito kutokana na vyombo vya habari vinavyoendelea kutoa taarifa dhidi ya kaka yao, ndivyo wao wanavyoendelea kujaribu kuwasiliana naye kwa njia ya simu lakini bila mafanikio.

Bw. Paschal alisema awali waliwasiliana na Dkt. Balali, ila kwa sasa mawasiliano yamekatika na hawajui hali yake inaendeleaje.

Pia alisema kutokana na nyumba ambayo alizaliwa Gavana huyo kuwekwa alama ya X kutokana na kuwa jirani na barabara, hivi sasa ndugu zake wako katika jitihada za kutafuta fedha za kuendeleza ukarabati wa nyumba hiyo ambayo ipo katika hali mbaya.

Hivyo alisema kutokana na maisha wanayoishi ndugu, ni vigumu kwa Mtanzania kuamini kuwa hapo ni nyumbani kwa Gavana na kuwa hata hao wanaomtuhumu kwa ubadhirifu ni vyema wakafika kuangalia maisha wanayoishi ncugu hao.


Wakati huo huo, baadhi ya wazee wa kijiji cha Luganga wamempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa jitihada zake za kushughulikia watu wanaotuhumiwa katika Serikali yake na kumwomba achunguze kwa kina juu ya Dkt. Balali.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi katika mahojiano maalumu kijijini hapo mwishoni mwa wiki iliyopita, wazee hao Bw. Joseph Kadege (49), Bw. Atilio Katefu (55) na aliyekuwa Mwenyetiki wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Bw. Tasili Mdoga (75), walisema pamoja na kwamba lengo la Serikali ni kuwa na viongozi waadilifu wamesikitishwa sana na hatua ya kumhusisha Dkt. Balali na ufisadi.

Walisema kwa upande wao wamemfahamu Dkt. Balali tangu akiwa mdogo na mwenendo wake wanaujua tofauti na watu wanavyozungumzia kuwa ni fisadi, alisema Bw. Katefu.

“Balali ni kijana wetu safi na ni vigumu kumtofautisha na mwanakijiji wa kawaida ... tangu utoto wake alikuwa hapendi magendo ... na hata ukiangalia nyumbani kwake alikozaliwa, huwezi kuamini kuwa alikuwa mtu mkubwa katika Benki Kuu, hivyo ninachotaka kusema Kikwete bado ana kazi nzito ya kuwapata waliochukua fedha hizo ila kwa Dkt. Balali wanamwonea ... ila tunaomba sana Rais Kikwete kama anatusikia afanye uchunguzi wa kina," alisema Bw. Katefu.

Naye Bw. Kadege alisema maisha ya Dkt. Balali ni vigumu kuamini kuwa ni mtu mkubwa katika Serikali ya Tanzania na duniani kwa ujumla, kwani kati ya viongozi wasiopenda kujilimbikizia mali, basi yeye ni mmojawapo.

Bw. Kadege alisema pamoja na kuwa yeye ni mkulima, maisha ambayo anaishi kijijini hapo hayawezi kulinganishwa na ambayo ndugu wa Dkt. Balali wanaishi kijijini hapo.

“Katika wilaya ya Mufindi na mkoa wa Iringa, ukisikia mtu anafanya kazi ya kuchuma chai, ni kazi ambayo inakwepwa na wakazi wengi kutokana na kutokuwa na heshima ... ila pamoja na Dkt. Balali kuwa katika nafasi nzuri bado hajaweza kuwa msaada kwa ndugu zake, kwani wadogo zake hadi sasa wanafanya kazi katika mashamba ya chai... tena kazi ya kuchuma chai,” alisema Bw. Kadege.

Alisema pamoja na kuwa ni vigumu kwao kupinga kama Dkt. Balali anahusika au hahusiki wanachoweza kusema kuwa kati ya viongozi walioonesha kupenda utaifa ni pamoja na Dkt. Balali.

Hata hivyo wazee hao walisema iwapo wataitwa watu wa kutoa ushahidi jinsi wanavyomfahamu Dkt. Balali na tuhuma zinazoelekezwa kwake wao watakuwa tayari kufanya hivyo.

Pia walisema wanaamini kuwa Dkt. Balali amebambikizwa tuhuma hizo ila iwapo atajitokeza hadharani huenda wahusika kamili wa fedha hizo watapatikana na kutahadharisha kuwa si vyema kwa viongozi wa juu serikalini kuendelea kumsakama Dkt. Balali, kwani wengi wao wanahusika kwa namna moja au nyingine kuchukua fedha katika benki hiyo.

Bw. Mdoga kwa upande wake, mbali ya kupongeza juhudi zinazofanywa na Serikali iliyopo madarakani katika kupambana na ufisadi, alimpongeza Rais Kikwete kwa kufuata mwenendo wa Baba wa Taifa marehemu Mwalimu Julius Nyerere katika kupambana na dhuluma na kutetea utaifa.

Alisema juhudi za Rais Kikwete zinaonekana, ila watendaji wake wamekuwa wakionesha kumkwamisha kwa kushindwa kuwajibika pale wanapotuhumiwa kwa ufisadi.

Hivyo aliwataka viongozi wanaotuhumiwa, kuiga mfano wa Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Peter Siyovelwa, ambao waliwahi kujiuzulu baada ya ofisi zao kutuhumiwa kati ya mwaka 1972 na 1973 baada ya sungusungu kutuhumiwa kuua wazee wenye macho mekundu Shinyanga na wao kutuma viongozi wa usalama ambao pia walionesha kutumia nguvu zaidi.

Bw. Mdoga alisema hana uhakika kuwa Dkt. Balali ndiye anayehusika na upotevu huo wa fedha za BoT peke yake, ila alisema ni vyema Dkt. Balali akajitokeza kama hali yake inaendelea vizuri ili aweze kuanika ukweli badala ya hivi sasa ambapo yeye pekee ndiye anaonekana mbaya.

Akielezea jinsi anavyo anamfahamu Dkt. Balali, alisema anavyosikia juu yake ni tofauti na yeye anavyomjua na kuwa bado hamtetei kuwa hahusiki ila anatambua kuwa kati ya watu ambao wamekuwa katika hali ya uaminifu Dkt. Balali pia yumo.

Alisema kwa nafasi aliyokuwa nayo na maisha anayoishi mtu hawezi kumlinganisha na baadhi ya viongozi wa Serikali ambao wamekuwa wakionesha kujijali wao badala ya jamii.

Aidha, Bw. Mdoga aliwapongeza wapinzani nchini kwa kuanika baadhi ya mambo likiwemo hilo la BoT, ila akasema wanapoendelea kuanika mabaya ya nchi yao, wafanye kwa usiri mkubwa badala ya kuendelea kulipua mambo ambayo yanalidhalilisha Taifa na kuondoa sifa kubwa ambayo iko nje.

Aliwataka Watanzania kuvuta subira hadi Dkt. Balali atakapopona badala ya kuendelea kumtuhumu wakati akiwa mgonjwa, kwani alisema upo uwezekano wa kukosa ukweli wa mambo iwapo Dkt. Balali mwenyewe atashindwa kuonekana.
 
Balali pesa BoT alikuwa anatumbua na vimada Dar hadi akaugua.. sasa aliwasahau ndugu zake wanateseka kule Mufindi ktk mashamba ya chai!
 
Mzalendohalisi,
Uliwahi kumwona Balali na vimada wapi?
Just asking.

Japo sikuwahi muona, ila kumbe habari za ngoma zimetoka wapi kama alikuwa hakimbii na totozi? si nasikia walikuwa wanafanya mchezo wa wa kupokezana na subordinate wake Liumba!!
 
Balali pesa BoT alikuwa anatumbua na vimada Dar hadi akaugua.. sasa aliwasahau ndugu zake wanateseka kule Mufindi ktk mashamba ya chai!

Mzalendohalisi,

Hilo la ndugu wa Ballali kuishi kwenye umaskini hata mimi limenishutua, yaani mshahara wa milioni 25 kwa mwezi, unaweza kusaidia kijiji kizima. Tena unapata mshahara huo baada ya kazi ya IMF miaka zaidi ya 20, ina maana huko una pension ya kutosha ukizeeka, wala alikuwa hahitaji hata ku save.

Labda alijenga kwa wakwe!!! kwi kwi kwi!!!

Maana watanzania kwa hilo tunaweza hasa, yote ni kamba nyingi. Unaacha ndugu zako wanateseka, unaenda kufurahisha ndugu wa mtu mliyekutana ukubwani, ndio maana ukimwi unatumaliza.
 
Rwabugiri,
Hizo habari za ngoma nimezisikia hapa JF. Kwa kadri nijuavyo mimi, na nimeshamwona Balali, shida yake si ngoma hata siku moja. Na kuhusu ndugu zake ni kweli Balali hajajenga Iringa, but then nasikia wasomi wengi kutoka huko hawajengi kwao, lawama ambazo na sisi baadhi tunaotoka Mara tumekuwa nazo. Wote tunapenda kujenga Dar.
 
Rwabugiri,
Hizo habari za ngoma nimezisikia hapa JF. Kwa kadri nijuavyo mimi, na nimeshamwona Balali, shida yake si ngoma hata siku moja. Na kuhusu ndugu zake ni kweli Balali hajajenga Iringa, but then nasikia wasomi wengi kutoka huko hawajengi kwao, lawama ambazo na sisi baadhi tunaotoka Mara tumekuwa nazo. Wote tunapenda kujenga Dar.

Ninavyofahamu mimi, mtu akiwa na ngoma huwa hafanyiwi operation kubwa hata ile ya uzazi. Lakini kama ambavyo inavyojulikana leo, Balali alifanyiwa operation kubwa huko Boston. Kwangu mimi huo ni uthibitisho tosha kuwa kweli hakuwa na Ngoma.


Kuhusu Balali kuwa mlaji wa starehe na kusahau ndugu zake, ninaelekea kushtushwa kidogo has kwa vile huyu Ballali anajulikana kuwa alikwenda kufunga harusi Ufaransa kwa gharama kubwa sana vile.


Hata hivyo jambo la muhimu ninalopenda mimi ni kwa Ballali kujitokeza hadharani na kutuambia ni nani hasa walikula hela zetu. Sipendi kusikia kuwa yeye ni mwadilifu huku anawaficha mafisadi waliokula hela yetu kiharamu.
 
Kuhusu Balali kuwa mlaji wa starehe na kusahau ndugu zake, ninaelekea kushtushwa kidogo has kwa vile huyu Ballali anajulikana kuwa alikwenda kufunga harusi Ufaransa kwa gharama kubwa sana vile.

Kichuguu,

Kama sikosei alienda kufungia Italy, huenda alizunguka kote na Ufaransa.

Mtu anayepata milioni 25 kwa mwezi, nyumba ya bure, magari ya bure, hanunui mafuta, hizo pesa nyingi mno. Ni zaidi ya mshahara wa waziri mkuu wa Uingereza, huenda ni zaidi hata ya mshahara wa rais Bush (sina uhakika). Kweli utashindwa kujenga nyumba ya ukoo kule kijijini?

Jasusi, ndugu yangu changamka, kama hujatengeneza kule Musoma, jitahidi, milioni kumi inatosha kuwa na nyumba ya maana kijijini na unarudi na familia yako bila wasiwasi.

Acheni kuwanufaisha mashemeji tu. Kwa niliko zaliwa mimi kujenga kwa wakwe ina maana umeolewa kwi kwi kwi!!!!.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom