Balali Atoweka

Pole sana, ndipo ilipofikishwa nchi yetu hapo. Serikali inaposhindwa kuwatafuta watu waliothibitika kusababisha wizi wa mabilioni...
 
Ikulu imetangaza leo kuwa serikali haimtafuti wala haina shida na kujua mahali alipo gavana aliyetimuliwa kazi kutokana na kashfa ya ufisadi, Daudi Ballali.
Kaka kawaida, salva aliitisha press conference leo na kati ya maswali aliyoulizwa ni hilo la Ballai na yeye akabainisha wazi kuwa kwa sasa Ballali ni RAIA HURU hivyo anaweza kuishi mahali popote anapopenda kwa sababu serikali haina shida naye kwa sasa.
Alisema baadaye itakapomuhitaji, kwa kuwa serikali ina mkono mrefu, itampata tu.

Wazee wa mizaha inayoumiza wananchi masikini. Lakini waswahili wanamsemo "mzaha mzaha....."

JJ
 
Mkulo umetumwa na giza gani lililozidi hilo lilipo? What are you trying to win out of all This? You need an elecric shock treament to bring to your sense!!
 
Nadhani kuna haja ya kuanzisha somo la "art of public speaking"! lakini sinihuyu mkulo aliyemkopesha sumaye 50m! wakati akiwa bosi wa npf! kama nimekosea mnisamehe! wakati Yusuf Manji anafanya madudu yake mkullo alikuwa wapi?
 
Ni kweli kabisa mwafrika wa kike yaani Watanzania ni watu wa ajabu sana. Kama inavyosemekana kuwa Tanzania ndio origin of mankind basi nina wasiwasi mkubwa kuwa our Intelligence decreases with time and changes in genomic makeup. Yaani ni aibu kubwa sana huku watanzania wenyewe wametulia kimya kabisa.

Mkuu unamaanisha kwamba sisi Watanzania ni wa ajabu sana, sure we are. Wepesi kurubuniwa, wagumu kugundua makosa ya wadanganyao, wapole sana hata kwenye mali zetu nk. But don't forget kwamba watu wa namna hii, wakiujua ukweli huwapati tena na hili CCM bado hawalijui ati.
 
Mimi nadhani hapa kuna maswali mengi sana ya kuuliza kutokana na maelezo yaliyotolewa na pin head Mkulo , kwanza kabisa anasema alimtafuta sana Washington anaweza kuwa more specific na kutueleza alimtafuta sehemu gani haswa ? Je sio serikali iliyosema aijui huyu mtu alipo , sasa yeye alimtafuta vipi kama hajui huyu muungwana yuko wapi ?

Pili , Balozi wa Marekani nchini Tanzania alisema ya kuwa Balali alipewa viza ya kuingilia Marekani na kama alipewa hiyo viza ina maana alipewa risiti ya I - 94 mara tuu baada ya kuingia . Kwa sheria za marekani mtu yeyote aliyeingia kwa viza ni lazima arudishe hii risiti wakati anapoondoka . Kwa hiyo kama serikali inataka kumtruck Balali waombe uhamiaji wa marekani uwasaidie ni kitu cha dakika kumi tuu , wanaweza kujua kama yupo au keshatoka.
 
Huyu Mkullo anaaibisha taifa kwa kila anachosema. Kuna watu wa nchi zingine wanajiuliza kama katika watu wote Tanzania wenye elimu ya kutosha kwenye uchumi na fedha, Huyu Mkullo ndiye pekee yake anayefaa!!!!
 
Ikulu imetangaza leo kuwa serikali haimtafuti wala haina shida na kujua mahali alipo gavana aliyetimuliwa kazi kutokana na kashfa ya ufisadi, Daudi Ballali.
Kaka kawaida, salva aliitisha press conference leo na kati ya maswali aliyoulizwa ni hilo la Ballai na yeye akabainisha wazi kuwa kwa sasa Ballali ni RAIA HURU hivyo anaweza kuishi mahali popote anapopenda kwa sababu serikali haina shida naye kwa sasa.
Alisema baadaye itakapomuhitaji, kwa kuwa serikali ina mkono mrefu, itampata tu.


Hii inauhusiano wowote na kauli ya Mkullo kumtafuta Balali MArekani???
 
Mimi sitaki kupata "headache" sasa, bado nasubiri ripoti ya EPA kutoka kwa Mwanasheria Mkuu, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, TAKUKURU, Mwema, ..

Sitaki kuamini hawa wote watakuja na majibu mepesi kama haya ya Salva!!
 
Ikulu imetangaza leo kuwa serikali haimtafuti wala haina shida na kujua mahali alipo gavana aliyetimuliwa kazi kutokana na kashfa ya ufisadi, Daudi Ballali.
Kaka kawaida, salva aliitisha press conference leo na kati ya maswali aliyoulizwa ni hilo la Ballai na yeye akabainisha wazi kuwa kwa sasa Ballali ni RAIA HURU hivyo anaweza kuishi mahali popote anapopenda kwa sababu serikali haina shida naye kwa sasa.
Alisema baadaye itakapomuhitaji, kwa kuwa serikali ina mkono mrefu, itampata tu.

Duh! Aliyekuwa Gavana wa BoT wakati mabilioni ya shilingi yanachotwa na mafisadi na ndugu zake wa karibu wamezungumza hadharani kwamba angependa kurudi ili kutoa ushahidi kuhusiana na ufisadi huo mkubwa wa mabilioni ya shilingi, leo SIRI KALI inasema haimtafuti!!!!

Na hakuna cha kushangaza hapa maana kuna mafisadi wengine wapo bongo akina Mkapa, Chenge, Karamagi, Mramba nao bado wanapeta tu, kama wanashindwa kuwatia hatiani mafisadi walio ndani ya Tanzania wataweza kumtafuta fisadi aliye nje ya nchi!!!?

Halafu wafadhili wanadai "wanaridhishwa na bidii" za siri kali katika kupambana na ufisadi!!!!! Ama kweli ukistaajabu ya Mussa utaona ya firauni!!
 
Huyu anaonekana anataka kupima maji tuu sasa yeye kumtafuta Balali anahusikaji
Yaani mkulo ni bure kabisa bora hata Sumaye huyu ni Ziro la nguvu
 
Hao waandishi wa Nipashe walikuwa wapi kumbana huyo Mkullo na maswali?..
Hivi hawa waandishi wetu kazi yao ni kureport kile kinachosemwa hata kama kuna Uongo?....
Mimi nadhani wandishi wetu wenmgi bado wapo ktk mtindo wa Kikomunist yaani zile kasumba za kijamaa bado hazijawatoka bado.
nambieni jamani hivi kweli unaweza kuandika vitu kama hivi ktk gazeti lako kama sio nia ya kuupotosha Umma..
Inasikitisha sana huko tunakoelekea...
 
Huyu Mkullo anaaibisha taifa kwa kila anachosema. Kuna watu wa nchi zingine wanajiuliza kama katika watu wote Tanzania wenye elimu ya kutosha kwenye uchumi na fedha, Huyu Mkullo ndiye pekee yake anayefaa!!!!

Ina maana tatizo sio Mkullo. Yeye ni jitu moja tu halina akili limechaguliwa. Lingekataa? Kosa la Kikwete. Lakini ngoja. Huwa tunasema Rais ameshauriwa vibaya. Washauri wa Rais ndio kina Mkullo. Kwa hiyo kosa la... No, tuanze tena...

You know what, to heck with it, mwingine anisaidie ku solve hili puzzle la uongozi Bongo manake ni li mess lisilo na kipimo...
 
Salva Rweyemamu keshajibu mapigo kuwa Balali ana hiari ya kuishi popote pale anapotaka kwa vile si mfanyakazi wa serikali, na hatafutwi na mtu yoyote, ila serikali ikimtaka hadhani kama itashindwa kumpata!
yaani serikali haina consistency hata kidogo, aibu gani hii
 
kweli serikali ya Tanzania ni ya aina yake!
kila anayetaka kusema anakuja na lake na kusema tu, hivi mkullo alikuwa anafikiria nini alivyoropokwa vile?
na Salva kutuambia mtu anayehusika moja kwa moja naEPA kuwa ni raia huru na serikali haimtafuti ni kutufanyia kejeli wananchi au?
 
Balali hatafutwi na serikali wajameni. Eleweni hivyo.

Kinachoendelea katika media ni spinning na ku divert attention yetu kutoka kwa Chenge Karamagi Lowassa na mafisadi wengine.

Kuweni macho wabongo!
 
Balali hatafutwi na serikali wajameni. Eleweni hivyo.

Kinachoendelea katika media ni spinning na ku divert attention yetu kutoka kwa Chenge Karamagi Lowassa na mafisadi wengine.

Kuweni macho wabongo!

sawa lakini suala la Balali haliwezi kukaliwa kimya, Mwanakijiji ametoa hoja je uchunguzi wa EPA unaofanywa na AG, IGP, Mkuu wa PCCB et al utakamilika vipi bila kumhoji Balali? Sisi tunatambua kwamba Balali ni hot cake katika suala la ufisadi wa BOT. Balali asipotafutwa na Serikali, atatafutwa na wananchi ili aseme kile anachokijua kuhusu EPA.

Hivi hao vigogo walioiba BOT watakuwa salama mpaka lini? lazima siku moja mambo yatakuwa wazi na itakuwa aibu kubwa kwa Serikali. Serikali ingekuwa serious kupambana na ufisadi, Balali angekuwa yupo chini ya ulinzi na anatoa taarifa za mtandao wa ufisadi.

Mkuu FD, sawa akina LA, karamagi et al ni sehemu ya mafisadi kama Balali tu. Hakuna wa kuachwa nyuma. Najua Balali anaogopwa kwa kuwa anasiri kubwa za mtandao wao.
 
Balali kusakwa

2008-05-09 09:07:43
Na Mashaka Mgeta


Serikali imesema itamsaka Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Daudi Balali mahali popote alipo muda utakapowadia.

Kwa mujibu wa ofisi ya Rais, mbali na Dk. Balali, aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Bw. Andrew Chenge, `amewekwa kiporo` ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili kufanyika, na hatimaye kuchukuliwa hatua kulingana na matokeo yatakayopatikana.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Bw. Salva Rweyemamu, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Ikulu, jijini Dar es Salaam jana.

Jana, gazeti hili lilimkariri Waziri wa Fedha na Mambo ya Uchumi, Bw. Mustafa Mkulo, akisema serikali haijui mahali alipo Dk. Balali, na kwamba timu iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete, inaendelea kushughulikia masuala yote yanayohusiana na Gavana huyo wa zamani wa BoT.

Hata hivyo, katika maelezo yake, Bw. Rweyemamu alisema hatua ya Rais Kikwete kumfukuza kazi Dk. Balali, ilimfanya (Balali) kuwa raia wa kawaida, mwenye uhuru wa kuishi mahali popote anapotaka, alimradi havunji sheria.

Taarifa zilizotolewa kwa mara ya mwisho na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Bi. Zakhia Meghji, zilisema Dk. Balali alikuwa katika hospitali moja huko Boston nchini Uingereza, akipata matibabu ya ugonjwa ambao hata hivyo haukujulikana.
``Balali ni raia wa kawaida mwenye mambo binafsi, hivi sasa hatafutwi, lakini ukifika wakati wa kufanya hivyo, serikali itajua yupo wapi na tutampata tu,`` alisema.
Dk. Balali alifukuzwa kazi na Rais Kikwete, baada ya ripoti ya ukaguzi iliyofanywa na kampuni ya Ernst and Young kubaini vitendo vya ufisadi, vilivyosabaisha upotevu wa mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

Hatua ya kufukuzwa kazi ilitangazwa wakati Dk. Balali, akidaiwa kuwa Marekani kwa ajili ya matibabu.

Kwa upande mwingine, Bw. Rweyemamu, alisema uamuzi wa kumkamata na kumfungulia mashtaka Bw. Chenge, utafikiwa baada ya uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili kukamilika.

Bw. Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi, anatuhumiwa kuhifadhi takribani Dola 1,000,000 za Marekani kwenye benki iliyoko katika visiwa vya Jersey, Uingereza, fedha zinazohisiwa zilipatikana kwa njia ya ufisadi katika ununuzi wa rada, wakati wa serikali ya awamu ya tatu, iliyoongozwa na Bw. Benjamin Mkapa.

``Tukisema tumkamate Chenge sasa hivi, kutakuwa na kelele kutoka kwa wanaharakati wa haki za binadamu na hata ninyi waandishi wa habari. Tusubiri uchunguzi ukamilike,`` alisema.

Aidha, alisema Rais Jakaya Kikwete, bado hajafikia uamuzi wa kumtangaza Waziri wa Miundombinu, kuziba nafasi iliyoachwa na Bw. Chenge.

``Suala la kumtangaza Waziri wa Miundombinu litafanywa kwa umma na si kificho, hivyo wananchi wasubiri tu, kwa sababu suala hili haliwezi kufanyika kinyemela,`` alisema.

Pia Bw. Rweyemamu, alisema suluhu ya mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar baina ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), inastahili kufikiwa kwenye meza ya mazungumzo.

CUF ilitangaza kutoendelea na mazungumzo hayo baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, kuazimia kuwa makubaliano ya kuundwa serikali ya mseto visiwani humo, yanapaswa kupata ridhaa ya wananchi, kupitia kura za maoni.

Msimamo wa CUF ni kwamba suala la kura ya maoni halikuwepo katika ajenda za mazungumzo baina ya vyama hivyo.

SOURCE: Nipashe
 
Wakati gani watamuhitaji Balali zaidi ya sasa ambapo watuhumiwa wote wanachunguzwa. Inamana Balali hachunguzwi? kama wangekuwa wanamchunguza wangekuwa wanafahamu yuko wapi.
 
``Awali tuliambiwa kwamba Balali alikuwa anatibiwa Marekani, lakini nilipokuwa huko (Marekani) hivi karibuni, nilimtafuta sana katika jiji la Washington, hakuonekana... Hatujui yupo wapi,`` alisema Bw. Mkulo, wakati akihojiwa na Nipashe jijini Dar es Salaam jana.

``Vyombo vya dola vinashughulikia suala hilo, kwa kushirikiana na polisi wa kimataifa, Interpol,`` -Mkulo

Kauli hiyo ya Ikulu ilitolewa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bw. Salva Rweyemamu, wakati akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine, walitaka kujua alipo sasa Bw. Balali.

"Inabidi kujua kuwa Bw. Balali sio mtumishi wa serikali, serikali haimtafuti hivyo ana haki ya kuishi popote," alisema Bw. Rweyemamu na kuongeza; "Sidhani kama serikali ikimhitaji hatapatikana, nadhani atapatikana na sasa hatafutwi na mtu yeyote



Hivi hapa sasa kipi ni kipi hapa?? huyu mmwandishi kwanini asinge muhoji Salva juu ya matamshi ya Mkulo na ni nani aliemtuma mkulo???
 
Back
Top Bottom