Balali Atoweka

Inawezekena Balalai anaishi kwenye moja ya zile twin towers pale BOT! Just a dream...
Twin Towers za nini?
Unaweza kuta yuko ufukweni na mademu wawili kushoto na kulia huku waki sip champainge na Margaritas!
Next time usishangae kifo chake kikiwa faked!
 
Sometimes viongozi wetu wanatia kichefuchefu, kama huyu Nkullo. Actually sometimes ni vigumu kujuwa nani kasoma na nani hakusoma maana wote waropokaji tu. Nafikiri ni kwa ajili ya dharau kwa Wadanganyika kwamba hatuwezi kufanya kitu. Hivi Nkullo mpaka kwa Director wa NSSF kwa miaka nenda miaka rudi bado busara hana. Hivi CV yake ikoje. Mwnye CV ya Nkullo atuletee hapa maana inawezekana hata huo uDG wa NSSF alipewa tu kisiasa!!!!!!
 
Ndugu Wana JF:
Nimepost thread yenye kichwa cha habari"Sheria ya kumkamata Balali hii Hapa"
Ni wazi kuwa nchi wahisani mara nyingi wamekuwa wakijaribu kusikiliza vilio vya wananchi!
Ni mara chache huwa wamekuwa wakipingana na mawazo ya wananchi!
Mfano halisi ni Hamas ya huko Palestina ambapo wananchi wameichagua lakini wamarekani wamesema NO!
Kwa upande wetu hilo sio tatizo!
Tayari tuna makubaliano na Wamarekani ya kukabidhiana wahalifu!
Sasa ni jambo la busara wananchi waandamane mpaka kwenye Ubalozi wa Marekani ili kuwaeleza dhamira ya wananchi ya kumtaka Balali!
Wao wameshasema sisi tukimtaka tutapewa! Kama serikali haimtaki..Haina maana kuwa wananchi nao hawamtaki!
Hivyo basi maoni yangu ni kuwa ni wakati wa kuwaambia wahisani kuwa thisi time its THE PEOPLE who have the say and not our corrupt leaders!
Hivi kweli how can you prosecute your own self?!
 
Kweli kabisa,
Na ni lazima tuwafahamishe hao Wamarekani kuwa kwetu BALALI ni muhimu kumpata kama ilivyo OSAMA kwao. Jee Wamarekani wanajisikiaje wanapodhani nchi fulani inamficha OSAMA? the same to us kwa BALALI.
Walisema wako tayari kuturudishia mtu wetu,ila serikali ya wenzake waliokwiba pamoja inaleta porojo za kipumbavu.
Nakubaliana na MushiI,kuwepo maandamano ili tumfahamishe balozi kuwa Balali ni Osama kwa TZ na wananchi wenye hasira kali wanamtaka, vinginevyo hadithi zao za ugaidi na kutaka ushirikiano kuutokomeza wazipeleke huko kwao.
 
CHAKAZA NA AK-47! HABAKI MTU! Kwi kwi kwi!
 
Hivi wanamtafuta Balali kwa misingi gani? Hivi uchunguzi wa EPA unaweza kuwa kamili bila kumhoji Balali?

Sasa kesho mkiambiwa Mwanyika alienda Marekani na kumhoji Balali si ndo mtasikia kizunguzungu?
 
Lakini watz nnavyowajua hata huyu Mkulo akigombea "urahisi" kupitia Chama Cha Mabazazi atapeta tuuuuuuuu!!!!!!!!!

Ila tutakujakuchekwa sana na generation ijayo!!!!!!
!!

Nyambala hii ni quote of the hour (if not a day). Yaani nakuambia kuwa akishapewa magwanda ya kijani na njano basi nchi nzima "itampigia kura" na atashinda kwa kishindo huku kina mama wakicheza mdundiko na kupiga vigelegele kuwa "mkombozi" wao amepatikana!

Nimeiongezea font post yako .... that is wassuuup!
 
Balali atoweka

2008-05-08 10:36:59
Na Mashaka Mgeta

Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania aliyefukuzwa kazi, Dk. Daudi Balali, ametoweka nchini Marekani, na serikali haijui mahali alipo.

Jitihada za serikali, kupitia kwa Waziri wa Fedha na Mambo ya Uchumi, Bw. Mustapha Mkulo, kumsaka Bw. Balali anayehusishwa katika kashfa ya ufisadi kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika jiji la Washington nchini humo hivi karibuni, hazikufanikiwa.

``Awali tuliambiwa kwamba Balali alikuwa anatibiwa Marekani, lakini nilipokuwa huko (Marekani) hivi karibuni, nilimtafuta sana katika jiji la Washington, hakuonekana... Hatujui yupo wapi,`` alisema Bw. Mkulo, wakati akihojiwa na Nipashe jijini Dar es Salaam jana.

HUYU NDIO WAZIRI WETU WA FEDHA JAMANI..........KWELI ZIMO HUYU MKULLA?
 
Nyambala hii ni quote of the hour (if not a day). Yaani nakuambia kuwa akishapewa magwanda ya kijani na njano basi nchi nzima "itampigia kura" na atashinda kwa kishindo huku kina mama wakicheza mdundiko na kupiga vigelegele kuwa "mkombozi" wao amepatikana!

Nimeiongezea font post yako .... that is wassuuup!
Ni kweli kabisa mwafrika wa kike yaani Watanzania ni watu wa ajabu sana. Kama inavyosemekana kuwa Tanzania ndio origin of mankind basi nina wasiwasi mkubwa kuwa our Intelligence decreases with time and changes in genomic makeup. Yaani ni aibu kubwa sana huku watanzania wenyewe wametulia kimya kabisa.
 
Huu ni utapeli wa kisayansi kuwa Balili kapotea.

Tena ni upunguani kwa kiongozi yeyote kusimama na kueleza kuwa Balali haonekani wakati kaondoka hapa akiwa mikononi mwao.

Ukiona hivyo ripoti ya Uchunguzi wa EPA na mazagazaga mengine ya BOT karibu yaipuliwe jikoni na waandishi watakapohoji wajibiwe katoweka.
Mkillo(Mkulo) Usanii mpaka lini?Umekuwa manju unatunga nyimbo za kumhusu Balali kila siku.Mara kalazwa,mara katoweka.
 
Hivi wanamtafuta Balali kwa misingi gani? Hivi uchunguzi wa EPA unaweza kuwa kamili bila kumhoji Balali?

Sasa kesho mkiambiwa Mwanyika alienda Marekani na kumhoji Balali si ndo mtasikia kizunguzungu?
Kwi kwi kwi kwi!
This is not funny though!
 
Ni kweli kabisa mwafrika wa kike yaani Watanzania ni watu wa ajabu sana. Kama inavyosemekana kuwa Tanzania ndio origin of mankind basi nina wasiwasi mkubwa kuwa our Intelligence decreases with time and changes in genomic makeup. Yaani ni aibu kubwa sana huku watanzania wenyewe wametulia kimya kabisa.

Mazee GQ,

aliyesema kuwa Tanzania ndio origin of mankind alikuwa amepata kilauri kidogo or sumt'n. Nakuhakikishia kuwa hata Karamagi naye akipewa magwanda ya kijani na njano na akawa mgombea wa ccm basi atachaguliwa kwa "kishindo"!!!!! grrrrrrrrrrr
 
Wewe si umeona picha za jana Jambazi Vijisenti Andrew Harvard Chenge alivyopokewa kama shujaa na wadanganyika. Yaani ni aibu kubwa. Utawakuta wenyewe na magwanda yao ya njano na kijani yaani wanatisha kama clowns.
 
Wanasiasa wetu hebu wajitahidi kuacha upuuzi na kujivisha madaraka waiyo nayo. Mkullo ni nani na anajukumu gani kumtafuta Balali?

Yeye ni FBI au Interpol? Kwa kweli huyu jamaa Mkullo amenichefua kwa kauli yake ya kitoto (kama amaenukuliwa vema na mwandishi).

Serikali ya Marekani imeshasema iko tayari kumrudisha Balali nyumbani ikiwa Serikali itataka, ni lini serikali imepeleka ombi na MArekani wakashindwa kumpata Balali? Wanasiasa wengine bwana!
 
Wananchi wenzangu nchi yetu tumiachiwa wenyewe, nchi haina kiongozi wala uwajibikaji. Viongozi wa kuu wa serikali wanajua ni wapi alipo balali. Inasadikika kwamba Kikwete alipo kuja Marekani desemba 12 2007 alikutatana na balali Washington DC kwa siri kubwa. Wanausalama wa mafisadi walimlinda ili asionekane kwa wanausalama wa taifa.

Mkullo ni mwizi, jambazi tangia NSSF, naye aseme ni kwa mshahara gani ameweza kujilimbikizia mali nyingi, kabla hatujaanza kutafuta account zake za nje.

Balali yupo na wanajua yuko wapi????

Wananchi tumtafute huyu mtu halafu tumfungulie mashitaka popote alipo, nasikia kichefu chefu kikubwa.....
 
Mtz, si kutufanya wajinga tu yawezekana wanatu-beep waone kama tutawapigia nadhani kuna haja siku tutoe mfano kuwa yawezekana kuna wakati wa-tz wakishindwa kuvumilia wanaweza kujitoa muhanga angalau hata hiyo sirikali ya JK na mabishoo wenzake wakatia akili. Mi naamini sana katika nguvu ya uma kuwa siku uma utakaposema sasa basi inatosha hatutaangalia sura ya mtu. Haya ni mambo ya kihuni kabisa...

Wake up Tanzanians jahazi linazama hili jamani...
 
Mi'nahisi sasa iko haja ya kujifunza uchawi tu!...maana mtu unaelezwa vitu vya ajabu mpaka unasikia kicheua-chefua. "Balali hajulikani aliko" Mhh!!! Nikifahamu uchawi nawaacha mafisadi kwanza, naanza na hawawafuga Mafisadi akiwamo Nkullo, Mwema nawengineo..maana wamenishinda!
 
hii sasa imekuwa hadithi ya abunuwasi. anamtafuta mtu Washington wakati anajua fika kuwa hayupo huko na wlaa yeye hana madaraka ya kumtafuta!
he problem with these guys wanafikiri kuwa watanzania wa sasa bado ni wale wa miaka ya nyuma, ambao walikuwa hawaulizi chochote wanachombiwa.
amka baba, zama hizo zimepita. na kwa ushauri tu, bora unyamaze kama huna cha kusema
 
Ikulu imetangaza leo kuwa serikali haimtafuti wala haina shida na kujua mahali alipo gavana aliyetimuliwa kazi kutokana na kashfa ya ufisadi, Daudi Ballali.
Kaka kawaida, salva aliitisha press conference leo na kati ya maswali aliyoulizwa ni hilo la Ballai na yeye akabainisha wazi kuwa kwa sasa Ballali ni RAIA HURU hivyo anaweza kuishi mahali popote anapopenda kwa sababu serikali haina shida naye kwa sasa.
Alisema baadaye itakapomuhitaji, kwa kuwa serikali ina mkono mrefu, itampata tu.
 
Hivi hawa watu wanazungumza huko maofisini kwao? Hivi wamewahi kusikia kitu kinaitwa "talking memos"..

Na kesho akija Hosea na kusema "Balali tunamtafuta" nani tumuamini?

Yawezekana huyo Bw. Mkullo alikuwa anamtafuta ili anywe naye chai tu na haihusiani na mambo ya serikali? Kama ni hivyo kwanini alitangaza hadharani kuwa alikuwa anamtafuta?

grrrrrrrrrrrrrrr, my head is spinning!!!!
 
Back
Top Bottom