Bajeti 2009/10: Mishahara Vipi?

KUNANI PALE TGA

Senior Member
Feb 6, 2009
138
7
Wakuluu habari za jioni.

Nataka niulize tu vipi mishahara kwenye bajeti imeongezwa kwa upande wa serikali au ndio tutaendelea kusota mpaka CHADEMA kishike hatamu?

Naomba nijibiwe.

Shukran wa jazila.
 
Wandugu wapendwa nauliza hiviii kwanini mishahara ya Wafanyakazi haiongezwi wakati kuna nyongeza mbalimbali kwenye Bajeti ya 2009/2010?Walio karibu na jikoni mtuelimishe.
 
Msubiri mhe. Hawa Ghasia atakapokuwa anatangaza bajeti ya wizara yake hope wataongeza hata kwa 10 %. Ni kawaida kila mwaka lazima mishahara iongezeke. Wakati wa Mkapa ilikuwa inaongezeka kwa asilimia 10 kila mwaka. Hapa katikati wakati wa JK mishahara imeongezeka sana na mwaka jana iliongezeka kwa 23 % na kwa wahadhiri na watafiti mishahara yao imeongezeka zaidi.
 
Mi Naona bora isiongezeke kwani Serikali imeondoa VAT kwenye kodi za pango la nyumba na vile vile imeshusha VAT toka 20% kuwa 18%.


Sasa wakiongeza mishahara basi kila kitu kitapanda kuanzia pango la nyumba, bidhaa madukani na hata usafiri.
 
Ivi alidesign hii PAY AS YOU EARN atakuwa mwehu,hela wanazokatwa wafanyakazi ni nyingi mno hasa wanaoern zaidi ya laki tano kama sikosei unakuta mtu analambwa ela ya kutosha.
Ukiludi mtaani hospital walipia,hao trafic na police mwenod wa rushwa,shule mtoto bila tuisheni ndo basi.
Sikatai fungu kubwa wanalokata ila matumizi yake basi yacreate unafuu wa maisha kwa wanaokatwa
 
Mi Naona bora isiongezeke kwani Serikali imeondoa VAT kwenye kodi za pango la nyumba

Hii si sahihi. Serikali inakusudia kuanza kutoza VAT kwenye nyumba za kupanga (isipokuwa za NHC na TBA).
 
Back
Top Bottom