Glenn
JF-Expert Member
- May 23, 2015
- 65,822
- 156,966
Hello wakuu sana;
Siku zilizopita nilipoteza bag langu dogo lenye vitu vichache lakini muhimu.
Ndani ya bag kulikuwa na ;
-Suruali 3 za jeans
-Raba za nike pair 2
-shati 2 na nk
-kadi 4 za bank tofauti
-kadi ya gari
-leseni ya udereva
-kadi ya gari
-××pasi ya kusafiria
-cheki ya bank nk.
- kitambulisho cha nida
Mazingira ya kupoteza yalikuwa ni hotelini, hii ni kutokana nilikuwa na mizigo mingi kiasi na nililazimika kuondoka kwa dharura kwani niliitwa kikazi mkoa tofauti.
Baada ya kusafiri na kufika mkoa mwingine, nilihitaji kutoa pesa ATM ndipo nikagundua kuwa sina kadi hata moja ndipo nikakumbuka zilikuwa kwenye bag dogo.
Nilijitahidi kuwasiliana na hotel nilikolala mkoani na kijana mmoja alikiri aliliona bag hilo ndani ya chumba kabatini.
Tuliongea sana kiasi cha kupanga namna ya kunitunzia kwani ningemtuma mshikaji akanichukulie anitumie.
Bahati mbaya kabla niliyetarajia akachukue alibanwa na majukumu.
Baada ya siku 3 alifika pale lakini mhusika alimchenga na hatimaye kijana alipotea ..kumbe aliachishwa kazi kwa makosa ya kazini.
Alichofanya alichambua vinavyomfaa na akachukua hadi bag lakini vitu vingine akavitupia kwenye pipa ndani ya stoo ambapo ilikuwa vigumu mtu mwingine kuviona.
Baada ya kufuatilia sana kwa njia ya simu ilionekana huenda vitu vyote ameondoka navyo na alibadili namba ya simu.
Kosa nililofanya ilikuwa ni kumwamini mtu...ambaye nilipokuwa pale alikula hadi tips zangu na tulijenga ukaribu.
Muda ukapita nililazimika kutoa taarifa ya upotevu wa vitu polisi na kuoewa RB
Ngoma ilikuja kwenye pasi ya kusafiria, awali nilipobadili kutoka pasi ya awali ya kitabu cha kawaida kuja pasi ya kidigitali nilitumia 150k.
Sasa baada ya upotevu nilitakiwa nitoe taarifa gazetini na linalosomwa kila siku na ada yake ya kuomba kupewa pasi mpya ni 500k.
Mungu sio FaizaFoxy walq rafiki yangu malatia 2, akaajiriwa meneja mpya katika hotel hiyo.
Huyu meneja mpya wakati anakagua kila mahali katika maeneo tofauti, ndipo aliingia stoo na kukagua kila kitu na ndipo ndani ya pipa akakutana na vitu tajwa hapo juu kasoro
Bag
Nguo na cheque ya bank.
Baada ya kuona hivyo vitu ilikuwa ni ngumu kutambua ni vya nani kwani hapakuwa na mawasiliano yoyote kwani kwenye kava la mwisho la pasi ya kusafiria ambapo huwa kuna sehemu ya kuandika mawasiliano sikuandika chochote.
Ndipo katika kukagua vitu alikutana na business card yenye majina yanayolingana na vitambulisho na akaona mawasiliano.
Juzi jioni nikiwa nimetulia zangu nilipigiwa simu na kupewa taarifa kuwa kuna vitu vyangu vilionekana na nikaulizwa endapo ninavitambua.
Ilikuwa ni furaha iloyochanganyika na mshituko.
Nafurahi nilifanya jitihada ya kuvifuata hatimaye leo nimevichukua.
Huyu ndugu alikataa katukatu shukrani zangu...lakini amenipa deni kubwa sana nafikiri Mungu akinisaidia nitafanya kitu kwa ajili yake....
Watu wema bado wapo ( Waislam kwa uaminifu mko juu sana)