Bado tunapwaya katika Suala la Makazi Tanzania, Tunahitaji Sera madhubuti ya Nyumba!

ExpertBroker

JF-Expert Member
Jun 1, 2009
454
107
slumoi-jpg.80801

Kiujumla hatuna housing policy hapa Bongo ndio maana suala la makazi halipewi kipaumbele! Economic Development Planning inafanywa na wachumi ambao huwa hawaoni kama suala la nyumba linachangia katika pato la taifa(GDP) directly, na hivyo issue ya housing kunyimwa umuhimu!

Ndio maana Dr. Slaa kwenye kampeni zake alitumia sana suala la makazi as his selling campaign weapon, kwani makazi yanamgusa kila mtu!

Kutopewa kipaumbele suala la makazi na hivyo kutakuwa na housing policy, ndio maana tumekuwa tukisonga kwa miaka mingi bila sheria za ardhi zinazoleweka, poor planning policy, and even those policies existing, no enforcement, no strict follow-up!

Na ndio maana over 70% ya jiji ni unplanned, na still the government is zipping his lips big time! Hakuna mkakati madhubuti wakutatua tatizo hili zaidi ya miradii ya kifisadi, mfano 20,000 plots projects ambapo plots zenyewe huambuliwa na wenye mikono mirefu! Kuna issue ya haki ya mpangaji, just imagine kodi inalipwa kwa mwaka au miezi sita na serikali imeendelea kupotezea wananchi waumie! Hii yote ni kukosekana housing policy na suala la makazi kupewa kipaumbele na hivyo kujali hali ya mwananchi wa kawaida!

Tukirudi kwenye hiyo miradi ya mashirika, hivi low cost housing ni ipi na affordable housing ni ipi? A total confusion! Kwa definition yangu, low cost housing au affordable homes zinatakiwa zi-base kwenye kima cha chini cha mshahara, minimum wage-rate, then tuangalie huyu mtu akikopa bank atapata kiasi gani kutegemea na mshahara wake! From there we can establish a market price for those houses, but now kila mtu anapuyanga anavyotaka just because hatuna sera ya nyumba na hakuna sheria madhubuti na nobody is caring!
 
Attachments

  • slumoi.jpg
    slumoi.jpg
    69.1 KB · Views: 412
Last edited by a moderator:
kwa mfano pale magomeni kota, msimbazi, na temeke, kama vile vijumba vimeshaonekana havifai (kuchoka kutokana na umri na maendeleo ya jiji) basi vibomolewe na zijengwe flats aidha iwe ni mradi wa hizi taasisi zetu za kifedha, au NHC wa-initiate mradi wa kifedha unaofanana na NSSF, PSPF n.k. ambapo kwenye hizo flats wakazi wake watakuwa wanalipa kwa kukatwa kwenye mishahara kama zifanyavyo hizo taasisi za kifedha.

Hiyo hela inayokatwa ni ya pango let's say 70% na 30% subscriber's contribution kwenye mfuko wa nyumba. mfano unakatwa kwa mwezi 100,000, ni bora na naamini utakaa kwenye nyumba inayoeleweka isiyo na usumbufu na hutajutia

Na iwe ni kwamba mwanachama hata akihama mji, as long as bado ni mwanachama hai, basi akikuta nyumba za NHC ni kumuona meneja wa eneo husika na kuomba apewe nyumba ya kukaa (ni sera na mipango tu)

Ikitokea muda wa kustaafu unauziwa nyumba kwa nusu bei
 
Last edited:
nyumba ya mil 80 ambayo mtaan wewe mwenyewe unaweza ijenga kwa mil 40 ndugu zetu wa NHC wanakwambia eti hiyo ndio low cost housing!!!! alafu wanalalamika watu hawanunui
 
nyumba ya mil 80 ambayo mtaan wewe mwenyewe unaweza ijenga kwa mil 40 ndugu zetu wa NHC wanakwambia eti hiyo ndio low cost housing!!!! alafu wanalalamika watu hawanunui
Mtu NHC anaambiwa alipe Laki 9 kwa Mwezi je mshahara kazini ngapi anapata kwa Mwezi Si njia za kufukuza watu hizi kwenye nyumba? Nyumba watachukua wenye pesa nyingi za mishahara wakati hao wanauwezo WA kujenga au kupanga sehemu, Tanzania imefika muda Dodoma,Tanga, Na Mikoa ya Kati ifanyiwe ujenzi WA makazi Na ukaaji kwa miundo inayotakiwa Dar-es-Salaam kuwekwe usafi Na kupunguzwe wakazi waone bora kukaa mkono kwenye Kazi Na pakukaa kwa nafuu Na elimu kwa Watoto Na Salama.
 
nyumba ya mil 80 ambayo mtaan wewe mwenyewe unaweza ijenga kwa mil 40 ndugu zetu wa NHC wanakwambia eti hiyo ndio low cost housing!!!! alafu wanalalamika watu hawanunui

Kwa hiyo kuna jipu
 
slumoi-jpg.80801

Mipango miji Urban Planning kwetu bado ni mgogoro sana; hivi hushangai taasisi za huduma za jamii kama maji, umeme hazijui tathmini ya kiasi cha huduma kwa eneo husika! Yaani unajenga nyumba halafu unaungiwa bomba kwa style ya T; kuunganisha bomba katika bomba la maji yaendayo kwa mtu karibu yako. Vipi upimaji wa viwanja; ni nani hasa mwenye idhini - ni serikali au yule jamaa mwenye shamba lake anakukatia kisehemu kutoka kwako ambako hata hana hati wala kujua hasa eneo lake liko vipi?
Tusipojiweka vizuri bomoa bomoa itaendelea tu; usishangae ikaingia hata city center -Kha ...!
 
Dodoma imepangiliwa kwa asilimia zaidi ya 90,sehemu iliyobakia watu walivamia wakajenga holela kutokana na urasimu wa kupata viwanja lkn nayo maeneo hayo yanaboreshwa ili yakae kimpango mji kuna baadhi ya nyumba zinavunjwa ili kupisha miundo mbinu kv barabara,maji taka,maji safi,umeme n.k .na wamiliki wake kulipwa fidia na kupewa eneo jingine na hilo limefanikiwa. Mamlaka za nchi zije zikajifunze Dodoma
 
Shirika La Nyumba Ni Tatizo Sana
Wizi Umekithiri Hiyo Nyumba Inamshinda Mtumishi
Kota Unaambiwa Milioni 80
 
Mtu NHC anaambiwa alipe Laki 9 kwa Mwezi je mshahara kazini ngapi anapata kwa Mwezi Si njia za kufukuza watu hizi kwenye nyumba? Nyumba watachukua wenye pesa nyingi za mishahara wakati hao wanauwezo WA kujenga au kupanga sehemu, Tanzania imefika muda Dodoma,Tanga, Na Mikoa ya Kati ifanyiwe ujenzi WA makazi Na ukaaji kwa miundo inayotakiwa Dar-es-Salaam kuwekwe usafi Na kupunguzwe wakazi waone bora kukaa mkono kwenye Kazi Na pakukaa kwa nafuu Na elimu kwa Watoto Na Salama.
Kuna ujumbe upo hapa ingawa umepinda pinda sana..!
 
NHC wameomba serikali iwaruhusu wauze na kupangisha nyumba zao kwa wageni...
hii nchi shida tupu
 
NHC wameomba serikali iwaruhusu wauze na kupangisha nyumba zao kwa wageni...
hii nchi shida tupu

Wageni waende kwenye open market si wanalipwa vizuri kuliko Watanzania. Je, wanafahamu historia ya NHC kwa nini ilianzishwa?
 
Kuna Thread nilianzisha nafikiri mwaka jana au juzi kuhusu maswala ya nyumba. Kutokana na mabadiliko siwezi kuiona labda Mod wangeileta.
 
nyumba ya mil 80 ambayo mtaan wewe mwenyewe unaweza ijenga kwa mil 40 ndugu zetu wa NHC wanakwambia eti hiyo ndio low cost housing!!!! alafu wanalalamika watu hawanunui
Muheshima ni low cost kwa maiaha ya watu wa kawaida kama hiyo pesa unaiilipa up to almost 20 years, mimi nimechukua hiyo ya m60 nimekusanya millioni 3 nikakopa benki 3 nikawa na jumla ya m6 nikalipa down payment ya 10% then baada hapo nikikabithiwa na lipa laki mbili kwa mwezi mpaka namaliza,
Ukiangalia baada ya miaka mitatu thamani ya laki mbili itakua ndogo mno likewise as time goes value itashuka na maradhi yakua affordable kila mwaka wakati mtaani kodi ikipanda na value ya maeneo kuongezeka,
Yes the housing is affordable if are tolerant. Sijutii kama ambavyo nimekaribia kumaliza huo mkopo wa millioni tatu.
Tengeza hoja ukithibitisha kwa mtu mwenye pesa ndogo atawezo hivyo bila NHC usisahau na bei za viwanja, wakati kwa NHC unapata maji,umeme na Barbara za mtaani kwako
 
Sekta binafsi ishirikishwe ..
hivyo viwanja ni 'prime areas'...
serikali ishirikishe sekta binafsi.....wauziwe...halafu wasimamiwe kulipa fidia

zoezi lingekuwa so easy...
 
shirika la Nyumba wamejikita zaidi kujilipa mamilioni ya pesa badla ya kuangalia namna ya kuboresha huduma, hasa kujenga nyumba zenye gharama nafuu, mfano haa wote wnao bomolewa makazi yao ilitakiwa NHC iangalie namna ya kuwasaidia ikiwemo kuwakopesha nyumba kwa bei nafuu,. nafikrir Raisi anapaswa kupasua jipu la NHC maana huyu prof wa mboga aliliacha shirika likiwa hoi
 
Tatizo ni serikali yenyewe. Ardhi makao makuu ni jengo lenye gorofa kama 10 hivi lina wafanya kazi wengi sijui kazi zao ni nini, eti wao wanaandaa policy! shame on the policy zinaandaliwa kila siku? mji wa Dar haujapangwa wao wako ofisini wanasoma magazeti wanasubiri mwisho wa mwezi wapate mshahara.
Wange kuwa na plan ya kupangilia mji wanaweka ramani kila kata kusudi mtu atakeye hitaji kujenga asijenge eneo ambalo si salama na si barabara au maeneo yaliyo wazi. Nchi hii imejaa viongozi wasio na vision
 
Kinachapaswa hapo Serikali ijenge nyumba za makazi ya kudumu ya wananchi kabla ya kuanza mchakato wa kubomoa makazi yao hili ndilo jambo la kiungwana na la kiistaarabu
 
kwa mfano pale magomeni kota, msimbazi, na temeke, kama vile vijumba vimeshaonekana havifai (kuchoka kutokana na umri na maendeleo ya jiji) basi vibomolewe na zijengwe flats aidha iwe ni mradi wa hizi taasisi zetu za kifedha, au NHC wa-initiate mradi wa kifedha unaofanana na NSSF, PSPF n.k. ambapo kwenye hizo flats wakazi wake watakuwa wanalipa kwa kukatwa kwenye mishahara kama zifanyavyo hizo taasisi za kifedha.

Hiyo hela inayokatwa ni ya pango let's say 70% na 30% subscriber's contribution kwenye mfuko wa nyumba. mfano unakatwa kwa mwezi 100,000, ni bora na naamini utakaa kwenye nyumba inayoeleweka isiyo na usumbufu na hutajutia

Na iwe ni kwamba mwanachama hata akihama mji, as long as bado ni mwanachama hai, basi akikuta nyumba za NHC ni kumuona meneja wa eneo husika na kuomba apewe nyumba ya kukaa (ni sera na mipango tu)

Ikitokea muda wa kustaafu unauziwa nyumba kwa nusu bei

Naunga mkono hoja ila bei ya nyumba isiwe dola laki moja mbili au tatu....mil za kawaida tu ili watu waweze kununua
 
Back
Top Bottom