Bado Tanzania hatuna watetezi ambao wakitumbukia kwenye maslahi yao binafsi wanaweza kusimama kidete

Aug 31, 2011
35
27
Bado tanzania hatuna watetezi ambao wakitumbukia kwenye maslahi yao binafsi wanaweza kusimama kidete kuitetea nchi ikiwa inateketea.

"ni kuhusu posho za bunge la katiba na wajiitao watetezi wa watanzania ndani ya vyama vyetu vya siasa".

Natambua kuwa makala hii haita mfurahisha mbunge yeyote wa bunge la katiba, au mtu yoyote mwenye maslahi na binafsi na bunge la katiba,pia hata wale washabiki wa mambo bila kufahamu ukweli wa mambo. lakini nataka niseme tu kuwa sipo hapa kumfurahisha mbunge yeyote au mtu yeyote kwa cheo chake na mamlaka yake ya nchi.

nia yangu ni kueleza bayana tena kwa masikitiko makubwa kwamba bado taifa letu linasafari ndefu ya kuwapata watetezi halisi wa watanzania ambao wakitumbukizwa kwenye mfumo wa giza ambao unawanufaisha wao watasimama kupinga giza husika japo linawanufaisha wao na ndo msingi wangu wa makala hii.

Ni mbunge gani? wa chama gani? amehoji juu ya kufuru ya posho "300,000=@mp, per day"katika kutengeneza katiba ya watanzania.

Je, kutanguliza maslahi binafsi katika kutengeneza katiba ya kizalendo itawezekana?

Je, kwa sura hii watanzania tutegemee kupata katiba kwa mujibu wa maoni yetu au kwa mujibu wa maslahi ya wataotoa chochote kushinikiza itikadi zao na misimamo yao ya vyama ipite katika katiba hii.? nasema hili kwa sababu mpaka sasa tunaona vyama vinatoa misimamo yao kinyume na mapendekezo ya tume tuliyoipa mamlaka ya kukusanya maoni. na nasikitishwa na kauli za baadhi ya viongozi wakubwa kuwa tunaweza kuifuta kabisa rasimu husika na ikatengenezwa nyingine. wasomi amkeni ni wakati wetu sasa.

Binafsi nimesikitishwa sana na suala la kulipana posho husika kwa kila siku. huku n ikiona waliokuwa wanajiita watetezi wa wanyonge wakifumba midomo yao, wakishindwa hata kuthubutu kuhoji kufuru husika katika kutengeneza katiba ya watanzania.

Ninahofu kubwa kama tanzania tunawatetezi wanaotetea kitu ambacho hawanamaslahi nacho na kutotetea kitu ambacho wanamaslahi nacho kwa uchache wao na kupuuza maslahi ya watanzania walio wengi.
raisi wangu wa nchi, naomba nikutumie salam, nimeshindwa kuwa na lugha halisi ya kusema lakini ngoja nijaribu kusema kwa busara nilizojifunza katika harakati za kuwatetea wanyonge wa taifa hili kwa maswali yafuatayo:

Je, katiba hii inatengenezwa na watanzania wazalendo au tumekodi wageni toka nje kwa ajili ya kututengenezea katiba ya nchi?
Je, mchakato wa kufanya maamuzi ya kuwalipa wabunge wa bunge la katiba uliakisi uzalendo, deni la taifa linaloongezeka kila kukicha kwa sababu kuu ya kulipana posho za kufuru kwa wachache, uliakisi hali halisi ya umaskini wa watanzania. au bado tunaendelee kukuza gepu kati ya walionacho na wasionacho.

Bado ninaamini maslahi binafsi kwenye mchakato huu yamekuwa zaidi ya maslahi ya watanzania. mnachekelea kwa uchache wenu kuwa mumeokota dhahabu lakini laiti mioyo yenu ingethamini udongo huu wa nchi yetu msingethubutu kukaa kimya kwa posho mnazopata.

Kulikoni wasomi wa nchi hii? tumesahau wajibu wetu? woga hofu na shaka ni dhambi kuu zaidi ya mauti haswa katika mambo yanayohusu maisha ya watanzania. "ukimya wetu ni usaliti. natambua kuwa kunamikakati ya siri ya kuzika sauti za wanafunzi wa vyuo vikuu nchini lakini nasema ni hatari sana tukikubali kuzikwa.

Bapinduzi ya yoyote huanzishwa na wasomi. tukisimama kwa sauti moja, hakuna jambo litashindikana nchi hii kwa maslahi ya taifa let. students let us work up.

Nimejifunza pia kuwa wasomi wa vyuo vikuu tumekubali kuzika wajibu wa vyuo vyetu katika harakati za utetezi wa wanyonge. tumefumbwa midomo, tumeogopeshwa kuhoji, kukosoa, kutoa ushauri unapo bidi kwa maslahi ya taifa letu. mchakato mzima wa katiba ya nchi yetu umetekwa na wanasiasa, sijaona msimamo wa wanafunzi wa vyuo vikuu juu ya katiba ya nchi hii. sijaona wana mjadala wakijadili mijadala hii katika maeneo yao ya mjadala revolution square. wasomi tusikubali kulogwa na tukalogeka kwa sababu bado matumaini ya taifa lolote lile ni wasomi haswa wa vyuo vikuu kwani tunaaminika kuwa ni vyanzo vya fikra huru.

let freedom ring, rev. square udsm,
let freedom ring, revolution square udom,
let freedom ring, rev. square muhas,
let freedom ring rev.square to all universities premises.

Wasomi ndio wenye macho ya kuona,ndio wenye masiko ya kusikia na ndio wenye mahala pa kusemea kwa maslahi ya wanyonge wa taifa hili.

by emekha.
w.together@ yahoo.com.
unaweza kushare ili ujumbe huu uwafikie wengi nchini.
 
Nilijua tu kuwa suala la posho litakuwa kizungumkuti, kwani kosa kubwa lilifanywa ni muswaada wenyewe, ilitakiwa wajumbe tuwachague kwa kura zetu kutoka hata kila Tarafa, kwani hawa walioteuliwa wapo kimaslahi zaidi, ukiongeza na ulafi wa wabunge wa bunge la JMT ndiyo balaa linazidi. Kwakweli nchi hii inalaana kila mtu aakipata nafasi anataka ale ashibe kabisa.

Na hoja walizotoa eti 300,000 ni ndogo haiendani na hadhi yao! Lo! kwani hawa jamaa wao wanahadhi ipi au hapo Dodoma kumegeuka kuwa Hong Kong ambapo hoteli ni ghali zaidi?
 
tena mabunge ya CHADEMA ndio yameshupalia posho zaidi , huu ni uhuni na unafiki wa hali ya juu
 
zama za kibepari hizi.....
wakweli wachache zama hizi.
cdhani kama wabunge hao wameenda kujadili posho au katiba ???
 
Masomi ya tz sio yakuyaamini ndo mabwege kabisa hata unapoteza muda kuyafagilia mana humo kwenye bunge la katiba asilimia 80 ni wasomi unataka wasomi wa aina gani yani hilo bunge ni funika kombe mwanaharamu apite tafakari
 
Back
Top Bottom