Mgombezi
JF-Expert Member
- Mar 23, 2009
- 610
- 178
Nimekuwa nikifuatilia maendeleo ya watu wanaoendelea kumiminika huko Loliondo na nimeanza kuziona fursa mbalimbali za kibiashara ambazo zikitumika vizuri zinaweza kutatua matatizo yanayojitokeza kwa sasa na vile vile kuinua uchumi wa wakazi wa maeneo hayo.
USAFIRI: Badala ya kila mtu kujiamulia kwenda mwenyewe huko, kungeweza kujitokeza kampuni mojawapo linalohusiana na usafirishaji (haswa hayo yanyofanya kazi za utalii) na kuratibu safari za huko; ambapo watu watahitajika kufanya booking na kutakuwa na idadi ya watu maalum ambao wataweza kwenda na kuhudumiwa kwa siku. Kutaweza kuwa na option ya wale watakaotaka kwenda na magari yao bali kuwe na utaratibu wa kujua idadi ya magari kwa siku na yote haya yataweza kuratibiwa na hii kampuni. Jambo la msingi ni kwa kampuni husika kuwasiliana na BABU aweze kutoa ridhaa ya huo uratibu.
MALAZI NA CHAKULA: Kutengeneza tents na wale wanaofanya catering services wanaweza kuhamia hilo eneo na kuwahudumia watu kwa chakula.
Fursa hii inaweza kuangaliwa kwa mapana zaidi!! (BUSINESS OPPURTUNITY), watu wa Arusha itumieni fursa hii vizuri.