kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
BEI ya kikombe cha dawa ya Mchungaji Mstaafu wa KKKT, Ambilikile Mwasapila inayopatikana kijijini Samunge,Wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha, imepanda na kufikia shilingi 1500 kwa wateja watokao nje ya nchi.
Dawa hiyo inayosadikiwa kutibu maradhi sugu likiwemo gonjwa la ukimwi huduma hiyo imepanda kwa wateja watokao nje ya nchi ya Tanzania.
Kwa mujibu wa Babu amesema wagonjwa watokao Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda watatakiwa walipe shilingi 1500 badala ya 500 ya awali na asipokuwa na hela hiyo basi atalazimika kulipa dola moja ya Marekani
Ongezeko hilo la bei halitawahusu wagonjwa wanaotoka ndani ya Tanzania na wataendelea kulipa shilingi. 500 kama kawaida.
Dawa hiyo imejipatia umarufu na watu kuzidi kumiminika Samunge kupata kikombe kwa minajili ya kupona maradhi yao sugu yanayowakabili na kudaiwa zaidi ya watu million 4 wameshakunywa dawa hiyo wakiwemo viongozi mbalimbali wa nchi