Babu ataka dola moja kwa wagonjwa watokao nje ya nchi

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
BEI ya kikombe cha dawa ya Mchungaji Mstaafu wa KKKT, Ambilikile Mwasapila inayopatikana kijijini Samunge,Wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha, imepanda na kufikia shilingi 1500 kwa wateja watokao nje ya nchi.
Dawa hiyo inayosadikiwa kutibu maradhi sugu likiwemo gonjwa la ukimwi huduma hiyo imepanda kwa wateja watokao nje ya nchi ya Tanzania.

Kwa mujibu wa Babu amesema wagonjwa watokao Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda watatakiwa walipe shilingi 1500 badala ya 500 ya awali na asipokuwa na hela hiyo basi atalazimika kulipa dola moja ya Marekani

Ongezeko hilo la bei halitawahusu wagonjwa wanaotoka ndani ya Tanzania na wataendelea kulipa shilingi. 500 kama kawaida.

Dawa hiyo imejipatia umarufu na watu kuzidi kumiminika Samunge kupata kikombe kwa minajili ya kupona maradhi yao sugu yanayowakabili na kudaiwa zaidi ya watu million 4 wameshakunywa dawa hiyo wakiwemo viongozi mbalimbali wa nchi
 
Katika hao million 4 nnauhakika wapo wanatembelea JF, jee kuna awezea kutuambia kapona baada ya kupata "kikombe cha babu"? atueleze akiumwa nini na kapona, kwa uthibitisho wa vipimo, kabla na baada. Akitokea mmoja akafanya hivyo, ntamlipa gharama zake zote alizo gharamika kwenda mpaka kurudi kwa babu! Open Challenge.
 
Hivi kweli, mpango wa Mungu wa uponyaji unambagua mtu kwa nchi anayotoka? This is now a business not divine healing! Kwa mujibu wa maandiko, mbele za Mungu watu wote ni sawa! Haijalishi unatoka wapi. Kwanza wanaotoka mbali ndio wangehurumiwa maana wanatoka mbali na kutumia gharama kubwa kufika Loliondo! eh! mhh! Au mtoa mada anatutania. Hivi ni kweli?
 
Labda kapokea maono mapya ya kupandisha bei. Wanasema hii ni political game, 2sahau machungu 2concentrate na babu
 
Vipi TRA wana monitor mapato yake.

Na vipi Babu alipewa maono ya kutoza wageni pesa zaidi ya zile za wenyeji.

Hivi Kwa mungu kuna uzawa na ugeni?
 
Kuna jamaa alikuwa anakufa na kisukari na alienda Samunge, sasa hivi namuona anadunda na afya imerudi vizuri sana. Labda hii dawa inatibu kisukari tu. Kuna mwingine walienda wote yeye hajapona na hali yake hairidhishi kwa kweli, anasumbuliwa na mishipa ya fahamu.
 
babu anapenda wazawa na hii kitu inabidi hata wanasiasa wetu waige huu mfano sio mhindi anakuja au mkenya basi mnamsujudiaaa kumbe hana lolote
 
mtoa mada hajaweka chanzo cha habari yake naona ni habri ya kupikwa hii.
 
Katika hao million 4 nnauhakika wapo wanatembelea JF, jee kuna awezea kutuambia kapona baada ya kupata "kikombe cha babu"? atueleze akiumwa nini na kapona, kwa uthibitisho wa vipimo, kabla na baada. Akitokea mmoja akafanya hivyo, ntamlipa gharama zake zote alizo gharamika kwenda mpaka kurudi kwa babu! Open Challenge.

Usije ukaikana kauli yako baadae!!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom