Baba yangu mshirikina

kingwipa1

JF-Expert Member
Jul 2, 2008
334
51
Nasema, baba yangu ni mshirikina.
Mbona unaguna? Mimi nimeshasema, baba yangu ni mshirikina. Ninazo sababu za kusema hivyo kwani nina kila sababu za kuamini hivyo (baba yangu ni mshirikina).
Visa vya baba kuwa mshirikina vinaanzia pale alipokuwa akimfukuzia mama. Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika kwani kuna wengi waliokuwa wakimtaka mama na sisi tulitakiwa tuseme ni nani anafaa kuwa baba yetu. Mimi nikiwa mmoja wa wanafamilia nilifuatilia kwa karibu mno ni nani anafaa kuwa baba. Kila mmoja alikuwa na mbwembwe zake, mmoja alijifunga mbawa akawa anaruka juu na kutua, na mwingine alisema ana-uelewa mkubwa kwenye mambo ya uchumi kwa hiyo atatulea vema na kutuletea maendeleo kwenye familia yetu. Na wengine ambao kwa kweli nilishindwa hata kufuatilia nyendo zao, nao walikuwa na yao.

Vituko vya baba tuliyempokea ni vingi vingi mno, kimoja ni kudondoka mbele zetu wakati akitushawishi sisi watoto tumruhusu kuwa baba wa familia. Baadae alidai kuwa ilitokana na jitihada zake za kutuombea ili tuwe na maisha bora. Kuna watu walituambia nyie huyo anayetaka kuwa baba yenu ni mshirikina, lakini sisi tukakataa na baadae tukakubali kuwa yeye ndo awe baba yetu.
Siku moja akiwa nyumbani kwa kaka yetu mmoja aliyekuwa na kasherehe kake, baba huyu wa kufikia yalimpata yaleyale ya kudondoka na kupoteza fahamu. Vipimo vilionyesha kuwa hana tatizo isipokuwa ni uchovu tu wa kazi nyingi.
Baada ya tukio hilo mimi nilianza kujikumbusha yaliyojiri huko nyuma na nikakumbuka yale ambayo watu walikuwa wakituonya juu ya mababa watarajiwa.

Nikiwa katika tafakari mara likatokea zogo kubwa kati ya watu wa imani na jamaa mmoja maarufu huku mtaani kwetu (anaitwa Hayahaya). Huyu Hayahaya aliwapiga mkwara watu watakaojitokeza kumpinga baba mlezi wetu wa sasa kuwa watakufa ghafla. Baada ya mkwara huo mtu mmoja wa imani akamwamba Hayahaya kuwa afute kauli yake la sivyo yeye atakufa ghafla. Na hapo nikamuona Hayahaya akigeuka mbogo na kumuambia mtu wa imani kuwa yeye si mtoto, na kumuomba kama anataka kujua kazi zake basi aende kwenye kibanda chetu anamoishi baba ndo atajua kazi zake. Mi kwa mara ya kwanza nilidhani ni utani lakini baadae nikaja kugundua kuwa jamaa hakuwa anatania kwa kuwa anajua anachokifanya kibandani kwetu. Nilitegemea baba atakasirika na kumuonya Hayahaya juu ya kauli yake lakini nikaona kimya.

Atamkaripiaje mtu aliyemuwezesha yeye kuingia kwenye kibanda chetu na kuwa baba yetu? Inawezekanaje baba akae kimya juu ya kauli ya kukidhalilisha kibanda chetu?

Ndo maana nasema baba yangu ni mshirikina!!!!
 
Saaaaaafi sana mkuu fasihi imetulia saaaana. ubarikiwe

..................................
Amani yetu inatumiwa vibaya.
 
Pole hata angekuwa mwizi baba ni baba tuu! lakini angalia usije ukaridhishwa huo ushirikina kwani wanasema mtoto wa nyoka ni nyoka...
 
Kwa kuwa nyie watoto ni wakubwa mnaweza kumtoa baba yenu kirahisi kabisa, tena bila ugomvi. Tumieni makaratasi ya kisomo October 2010!!!
 
Someni kwa umakini, great thinkers...right!??
Duh, huyu baba sijui tumfanyaje! Labda tumfanyie visa aachane na mama yetu..
tatizo ni nani atamrithi baba? ama mama abaki mjane..siyo vizuri!
So, kabla ya kumtoa baba, tufikirie wa kumleta..kwani sitaki mama abaki ukiwa!

Hivi mama naye anampenda au basi tu kwa sababu anaogopa kuomba talaka?
 
Tatizo la baba wa kufikia hawezi kuwa bora, hata mngemchagua mwingine kati ya wale angekuwa na kasoro tu, kwahiyo mvumilieni tu, au ikibidi badili baba maana ni wa kufikia tu mna nafasi ya kumchagua mwingine ila muwe makini mjitahidi kasoro zake mzihifadhi msizitoe hadharani mwisho mtaonekana watt ndio mna matatizo maana kila baba atakuwa hawafai! tatizo la mtoto wa kulelewa na baba ya kambo huwa hanajema hata ukimpa roho yako...hatoacha kusema bora baba yangu angekuwepo
 
Hivi mama naye anampenda au basi tu kwa sababu anaogopa kuomba talaka?

Hata mama mwenyewe anasema basi! Ana haya ka nini cjui ila hawa watoto hawa ndo walimsemea mama eti huyu baba anakufaa. Jamani mi nshaona huyu baba atatufia humu ndani. Kaka zangu na dada zangu kama tunadhamira ya kweli basi huyu baba hamfai mama yetu!!!!
Naskia anarudi kwa Hayahaya karibia na mwezi wa kumi. Jamani eee mie nasema basiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
hapana mshirikina anapaswa kutolewa roho au kupatiwa mateso makali kama anavyofanya kwa wenzake. wewe unamtetea au unampenda aendelee kua baba yako?
 
mwanzo sikupata picha, nikaona mauza uza gani tena haya. ila baadae nimeona ndani

ni kazi nzuri
 
Back
Top Bottom