Baba Askofu Dr. Bagonza: Mapenzi ya Mungu na Mapenzi yetu

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Anaandika Baba Askofu Dr.Benson Bagonza (PhD), daktari wa Falsafa na Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
_____________________________
MAPENZI YA MUNGU na MAPENZI YETU.

Siyo kila kifo ni mapenzi ya Mungu hata kama Mungu anajua kila kifo. Siyo kila ajali ni Mapenzi ya Mungu hata kama Mungu anaiijua kila ajali.

Tukumbuke alimuacha Mwana wake kuuawa hata kama alikuwa na uwezo wa kuzuia. Alimwacha Mwana wake kusalitiwa hata kama alikuwa na uwezo wa kumkomesha msaliti wake.

Hatua zote za maendeleo zina ukurasa wa majanga. *Dreamliner na Bombadier usiote janga lake. SGR janga lake ni kiama. Stiggler's Gorge ina janga la kuangamiza mamilioni kwa siku moja kingo za bwawa zikipasuka. Meli mpya ya abiria 2000 ni kaburi la halaiki linaloelea majini.*

Uwezo wetu upimwe kwa kushughulikia majanga, si kwa kuchochea majanga. Poleni wafiwa, Ugua pole majeruhi, Tufarijiane Watanzania.

#MyTake:
Falsafa ni somo gumu, halijawahi kueleweka kwa wote. Lakini pamoja na ugumu wake, tuzitafakari falsafa za baba Askofu Bagonza, na tujitahidi kuzielewa. Zina mengi ya msingi.!
 
Mwanasiasa aliyejificha kwenye dini.Afanye moja aeleweke.
 
Huyo anafanya siasa tu..kwa nini agusie miradi ya maendeleo ambayo chadema wanaipinga..?mbona mabasi yanapata ajali..boda boda na vingine..hata magari binafsi..mwanadamu huwa akikaa hafikirii mabaya..kwenye ndege kuna miamvuli ya kujiokoa lakini hata siku moja husikii ndege imepata ajali na kuna watu wawili walijiokoa kama ambavyo tunaagizwa kufanya tukiingia kwenye ndege ( hii ni kwa waliowahi kupanda)..inapotokea ajali watu hughafirika na unaweza usione hata hilo boya hususani kwa ajali ya mara moja na haraka...lakini ukiangalia hii ajali ilikuwa inaepukika..ni suala la uzembe na rushwa kwa wasimamizi wa kivuko..
 
Askofu ambaye kila akipanua kinywa anaongea siasa hatufai.Ajiunge tu na vyama vya siasa ili atambulike na sisi tumjadili kisiasa
 
Nina uhakika uelewi ata king kidogo kuhusu dini. Hakuna sehemu ata moja dini iliwahi kutengwa na siasa.

Soma story zote za mitume na manabii hawakuwahi kuficha nyuso zao kwa kuogopa watawala.
Unamaanisha walisahau jukumu lao la kuhubiri injili wakaanza kujadili siasa? Au sijakuelewa vzr
 
Kwanza ungetoa hiyo PHD maana msomi yeyote anajua maana ya disaster !! Sasa hayo aliyoyasema yanauhusiano gani na hii ajali?
 
Unamaanisha walisahau jukumu lao la kuhubiri injili wakaanza kujadili siasa? Au sijakuelewa vzr
Hawa miungu watu wa Afrika lazima wakemewe tuu, na manabii na mitume wa Mungu.

Haya ni maneno ya Yesu mwenyewe akimwambia Herode.

Luka 13:32
Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika.
 
Back
Top Bottom