Baadhi ya Wazanzibari wajiandaa kusherehekea 'uhuru' mapema

Kinyikani

Member
Dec 5, 2006
67
7
Baadhi ya Wazanzibari wajiandaa kusherehekea 'uhuru' mapema
Na Salma Said, Zanzibar

BAADHI ya wananchi wa Zanzibar wameandaa sherehe za kuadhimisha miaka 45 ya tangu Zanzibar ilipopata uhuru wake Disemba 10, 1963 kutoka kwa Waingereza na baada ya mwezi mmoja serikali iliyowekwa madarakani ilipinduliwa.


Hiyo itakuwa sherehe ya kwanza kufanyika kutokana Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyoitwaa madaraka Januari 12, 1964 kuifuta na kuifanya tarehe ya mapinduzi kuwa ndiyo hasa ya kuwakomba Wazanzibari kutoka katika uhuru bandia na utawala wa sultani.


Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kiongozi maandalizi ya sherehe hizo, Daud Jabil Seif, alisema wameamua kuadhimisha sikukuu hiyo ili kuwaenza waasisi wa uhuru wa Zanzibar wa mwaka 1963 ambao

hawakumbuliwi na serikali.


Serikali iliyopatikana katika uhuru wa Desemba 10, 1963 chini ya Waziri Mkuu wake, Mohammed Shamte, ilidumu kwa mwezi mmoja madarakani hadi Januari 12, 1964 ilipopinduliwa na kundi la wanamapinduzi lililoongozwa na Hayati Sheikh Abeid Aman Karume.


"Hivi karibuni tulimsikia Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha, akisema kuwa historia haiwezi kufutika, hivyo na sisi tunaadhimisha siku hii kwa kuwa ilitokea na imo katika historia ya Zanzibar. Ingawa haitajwa lakini ilitokea sio mapinduzi pekee, hivyo siku hii inafaa kuadhumishwa pia…," alisema Seif.


Alisema viongozi waliosimamia uhuru huo walijitolea nguvu zao, hivyo wana haki ya kukumbukwa na kuenziwa na pia vizazi vijavyo vinapaswa kufahamu umuhimu wa siku hiyo katika historia ya Zanzibar.


"Tulianza kufanya vikao vya matayarisho tangu Oktoba, mwaka huu na sehemu kubwa ya matayarisho yamekamilika lakini yatafanyika katika maeneo matano tofauti hapa Zanzibar," alisema Seif.


Hata hivyo, Sief alisema mikusanyiko ya maadhimisho hayo itafanyika katika nyumba za ibada (misikitini) kwa ajili ya kukwepa usumbufu wa Jeshi la Polisi na kwamba, itatanguliwa na maombi maalumu (hitima) ya kuwaombea wazee waliokwishafariki na baadaye kitatolewa chakula kama karamu na sadaka wa wazee hao waliotanguliwa mbele ya haki.


"Tumetayarisha chakula kama sadaka. Hapa mjini tutafanya shughuli hiyo kwa makombe ya halua ambayo imetugharimu kama Sh600,000. Tumaliza kisomo chetu tutakula na kupeana mikono na kuagana salama kwasababu sisis hatutaki fujo…" alisema Seif huku akitabasamu.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Bakari Khatib Shaaban, alipoulizwa kama ana taarifa hizo alisema hana habari zozote kuhusiana na suala hilo kwa sababu wakati mwingine taarifa kama hizo hupelekewa makamanda wa polisi wa wilaya.


"Mimi sijapata hizo taarifa, labda OCD amepata, ebu muulizeni kupitia kwenye simu yake, huenda yeye atakuwa anajua," alisema Kamanda Shaaban


Alipoulizwa OCD, Mkadam Khamis, pia alisema hajapata taarifa yoyote kuhusiana na sherehe hizo na kuahidi kufuatilia mkusanyiko huo ambao haujapewa kibali cha jeshi hilo.


Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema haizitambui sherehe hiyo kwasababu haimo katika mfumo wa sherehe za kitaifa.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma, alisema hana taarifa kuhusiana na sherehe hizo na kusisitiza kuwa kufanyika kwake ni uvunjaji wa sheria.
 
Bado kuna elements nyingi zinazoonyesha kukubalika kwa siku ya Uhuru huko Zenj... Ingawa ni Mapinduzi ndio yenye kukumbukwa zaidi
 
Last edited:
Back
Top Bottom