TheMnyonge
JF-Expert Member
- Mar 25, 2022
- 739
- 1,871
Nimekaa na kutafakari sana baada ya kukutana na mama mmoja maeneo ya mitaa ya katikati ya mji wa Morogoro.
Huyu mama ana mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka kati ya 15-17, kwa maelezo ya mama yake ni kwamba kijana wake amelazimika kuacha shule kutokana na kukumbwa na maradhi yasiyoeleweka.
Kkufuatia hali hiyo, niliingiwa na roho ya huruma na kuamua kufuatilia uhalisia wa tatizo na kumsikiliza yule mama. Baada ya maelezo yake nilimchukua na kwenda naye mpaka shule anayosoma mtoto, nikastaajabu kuona matokeo ya mtoto ni mazuri mno, (yupo kidato cha tatu).
Sasa katika kujikwamua na hali ya mtoto wake, alienda kwa mtumishi anaitwa FRANK KILAWA, huyu jamaa alimwambia mama kwamba, "mtoto wako ametupiwa majini 4 na wanataka kumchukua msukule" akamwambia akichelewa kutekeleza maagizo aliyopewa basi soon atakuwa msukule!
Maelekezo aliyompa ni kwamba ili mtoto apone, huyo mama anatakiwa kununua pakiti kumi za chumvi (zile ndogo kabisa, zinauzwa sh.200 dukani) lakini huyu mchungaji analazimisha huyu mama anunue kwake, na yeye anauza pakiti moja sh.10,000/=
Hivyo ili mtoto aombewe, analazimika kutafuta sh. Laki moja! Hapa ndipo paliponifikirisha zaidi, hivi kweli mtu anayejiita "mtumishi wa Mungu" anaombea watu masikini kwa gharama kubwa kiasi hiki?
N'a mtu asiyekuwa na pesa hapati huduma ya maombezi? Huyu ni Mungu wa aina gani?
Pamoja na kwamba wanaokwenda wanakuwa na uelewa mdogo, wanachoangalia ni namna ya kutatua changamoto zinazowakabili tu, lakini kuna haja ya kutafuta udhibiti wa hawa watu kwa ustawi wa jamii.