Baadhi ya wadau wa NGO's wataka unafuu wa kikodi ili kufikisha huduma zaidi kwa wananchi

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
"Kuna changamoto ya faini za fedha za kuleta 'return' kwenye mfumo, lakini kuna vifungu vya kisheria vya kufuata adhabu na nitoe wito kama kuna mtu ana adhabu iliyotokana na kutowasilisha return walete maombi na tutazifuta kwa wingi."

"Tunafuta ili kumpa Mwanga kufanya kazi sababu akiona mafaili mengi ya adhabu itamnyong'onyesha hata kulipa Kodi."

Hayo yamesemwa na Meneja TRA Kinondoni, Edmund Kawamala kwenye mkutano wa nusu mwaka baina ya mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO,s) na Mamlaka ya Mapato (TRA), ambapo mkutano umekutanisha wadau kutoka mashirika mbalimbali ukiwa umeandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)

Meneja huyo ameongeza kuwa "Uamuzi wa kufuta faini haimaanishi muendelee kutowasilisha return, nitayoa elimu ya jinsi ya kutoa return ili NGO's zisiwe zinafutwa kwa sababu hiyo.Pale kwangu hakuna appointment mje wakati wowote nitawasikiliza''

Pia Mwenyekiti wa Bodi ya NGO's, Mwantumu Mahiza akizungumza katika mkutano huo amewataka maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kutoa elimu zaidi ya ulipaji Kodi kwa mashirika hayo ili kukwepa migogoro ya kikodi.

"Mikutano hii inaendelea nchi nzima mpaka Agosti sababu Septemba tutakuwa na mkutano wa NGO's Dodoma, ningependa kila mkoa elimu ya mlipa kodi itolewe huenda ikaondoa manung'uniko. Sababu wengine wanaoingia kwenye kufutwa wanafutwa kwa sababu ya faini na adhabu, lakini nafarijika ipo nafasi waje wazunguzme." amesema Mwenyekiti huyo

Amesisitiza kuwa "Sio kwamba ninawatetea sana, bali hebu fungueni macho hizi NGO's ziko zaidi ya 8,000 tukisema tuzifute hali itakuaje? Kuna kazi zinafanywa kwa ufanisi na NGO's ambazo Serikali hatufiki kwa kiwango kinachokusudia"

Aidha Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa amebainisha changamoto nyingine ambazo zimekuwa zikikumba NGO,s kuwa ni pamoja faini kubwa ambapo ameshauri hilo litafakariwe.

"Changamoto nyingine ni muda wa malipo, ukichelewa kidogo kulipa au umekosea mfano Leo ni deadline kuanzia kesho faini ni Sh. 2 milioni ikikaa mwaka riba inakuwa kubwa, tunaomba TRA iangalie" amesema Olengurumwa.

Olengurumwa pia ametaja changamoto nyingine ambayo wadau hao wamekuwa wakikutana nayo wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao kwenye maeneo ya vijijini "Kuhusu masuala ya EFD inatupa changamoto NGO's wanalalamika wanafanya kazi maeneo ya vijijini lakini EFD imekuwa shida baadhi ya maeneo hakuna. NGO,s haitakiwi kuwa na EFD lakini unaofanya nao huduma lazima wawe na EFD Sasa shida maeneo ya vijijini hawana"

Lakini pia Olengurumwa amesema kuwa kuendesha NGO sio kazi rahisi hasa ikiwa inaanza hivyo ameshauri kuwepo na misamaha au utaratibu rafiki zaidi wa kikodi kwa NGO,s mpya kama ilivyo kwenye utaratibu wa kampuni huku akishauri kuwa wadau hao licha ya kuwa na wajibu wa kulipa kodi lakini ameshauri kutazamwa zaidi kama watoa huduma.

Hata hivyo baadhi ya washiriki wameshauri maswala mbalimbali, ikiwemo kwenye ofisini za TRA awepo mtu maalum ambaye anatashughulina na NGO,s, huku wengine wakishauri baadhi ya mifumo ya taarifa za kikodi kwa njia ya mitandao maelekezo yake yawekwe kwenye lugha ya Kiswahili.
 
Back
Top Bottom